Unakubalije kuwa mwalimu?

Unakubalije kuwa mwalimu?

Ila hao waalimu walikufundisha na ukafika hapo ulipo. Labda uwe hujui kuandika na kusoma, huu uzi mtu kakuandikia.
 
Mi sio mwalimu kwa sasa , ndugu jasusi eli cohen.ila niliwahi kuwa na mpk sasa bado naona kwa ndugu na marafiki jinsi ambavyo hii kada haijabadilika. The worst ever, ukitaka professional poverty ingia kwenye ualimu.
Habari yako bhana Mpwayungu...kweli mwalimu analipwa 1,800,000/= (nimeona Mshikaji kaanza kazi 2010 na analipwa mihela yote hiyo)
Amejenga kamjengo kake kazuri tu na ka-forester kale ka misele,ukiniambia ualimu ni mbaya nitakushangaa! Ubaya sio ualimu, ubaya ni kile kilicho kwenye vichwa vya wanaoona ualimu kuwa mbaya!
 
Hii ndio the worst job ever, usikubali kuwa mwalimu liwalo na liwe ,bora ukaponde kokoto
1744479521136.png
 
Hivi huo Ualimu wenye dhiki mnaoongelea ni Ualimu upi huo?

Maana mimi kuna brother yangu ni Mwalimu yuko Tabora ana mkwanja kunizidi mimi niliyeajiriwa sekta nyingine serikalini. Pamoja na kwamba ana takehome ndogo ya 900,000/= ila ana mizinga ya nyuki kama 130, analima tumbaku hekari nyingi, na ana Shamba la miti ya mbao hekari 20. Mwaka juzi kavuna miti kadhaa kala milioni 70 simple tuu. Sasa ni Ualimu upi wa dhiki mnaouongelea nyie?
 
Acheni kukopa kopa ovyo kwenye mabenki&kausha damu, hata kazi mtaipenda na kuithamini.
Maisha myakosee wenywe halafu msingzie kazi yenu.
Jiongezeni, jishughulisheni nje ya field yenu mtafnikiwa.
NAUNGA MKONO
Moja ya chanZo cha stress /msongo wa mawazo miongoni mwa baadhi ya waajiriwa ni mikopo ya mabenki kwa watumishi haya mabenki NMB/CRDB n.k..ukikopa milioni 25 unalipa milion 50 ukikopa milioni 10 marejesho milioni 20 yani RIBA ni kubwa mno haistahimiliki.

Na watumishi ili waweze kufanya maendeleo KWA HARAKA wanalazimika kujiingiza katika hii mikopo ya watumishi ya haya mabenki NMB/CRDB N.K..wengi sana wamekopa na wengine wana top up..

SERIKALI ili iwasaidie watumishi wake napendekeza IPUNGUZE RIBA ZA MIKOPO YA WATUMISHI kwenye haya mabenki NMB/CRDB N.K ,itawasaidia pakubwa watumishi wa Umma.

kwenye mikataba ya hii mikopo riba yake inasomeka ni asilimia 16% iliyoandikwa ya kwenye makaratasi ya mikataba.
baada ya kukopa sasa
mwisho wa siku UKISHAKOPA kiuhalisia deni la marejesho ya mkopo wako utakalolikuta limeandikwa kwenye SALARY SLIP YAKO linakuja kusoma mara mbili DOUBLE ya ulichokopa.

Mfano ukikopa leo max milioni 25/26 deni lako utalipa milioni 50/52. makato ya shilingi laki 6 na point kwa kipindi cha miaka 7.

Na hii sasa ni moja wapo ya chanzo kikubwa sana cha stress kwa baadhi ya watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom