Unajua pesa ya Tanzania inatengenezwa wapi?

Unajua pesa ya Tanzania inatengenezwa wapi?

Wakitengeneza watengeneze pesa zenye ubora

Ova
 
View attachment 3319531

Najua watu wengi walikua wanajiuliza sana Pesa ya Tanzania inatengenezwa wapi ? Ni maswali ambayo mimi na wewe tulia tunajiuliza sana? Je Tanzania Ina kiwanda cha kutengeneza pesa zake ??

View attachment 3319532

Maswali yote Leo utaweza kupata majibu yake kwa ufupi TU kupitia makala hii 😋, kwanza inapaswa kujua Pesa huwa azitengenezwi nchi moja TU hutengenezwa kupitia nchi mbalimbali hapa Duniani.

View attachment 3319533

Pesa zinatengenezwa kwenye nchi zilizoendelea kama vile Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uswizi, Saudi Arabia, Sweden na Uingereza. Ila kwa upande wa Afrika nchi zinazotengeneza pesa ziko Saba pekee
• misri
• Morocco
• Nigeria
• Ghana
• South Africa
• Ethiopia na Zimbabwe ilikuwepo lakini baadae ilizuiliwa kutokana na sheria maalum za kimataifa zinazo husika na taratibu za kumiliki kiwanda cha kutengeneza pesa.

View attachment 3319534

Nchini Kenya kuna kiwanda cha kutengeneza pesa lakini sio Cha Kenya ni Cha nchi toka Uingereza kwaiyo Kenya kipo kama Tawi kwa upande wa Afrika mashariki.

View attachment 3319535

Je pesa ya Tanzania inatengenezwa wapi sasa ?? Pesa ya Tanzania kamwe haitengenezwi nchini Tanzania mwanzoni baada ya uhuru ilikua inatengenezwa Nchini Uingereza kuanzia sarafu na Noti ambapo serikali ya Tanzania ilikua inaipa Tenda nchi ya Uingereza.

View attachment 3319536

Kwa sasa pesa za Tanzania haitengenezwi Tena Uingereza isipokuwa Ujerumani ndio inatengeneza pesa Za TANZANIA aina ya Noti ambazo ni;
⚡ ELFU KUMI
⚡ ELFU TANO

Wakati nchi ya Sweden inatengeneza Pesa za nchi ya Tanzania ambapo kuanzia NOTI na SARAFU;
⚡ ELFU MBILI

⚡ELFU MOJA
⚡SARAFU

Ulikua unajua hii au lah tuachie maoni yako??
Pumbavu kabisa. Hayo mapicha ya huyo kibibi unaweka ili iweje.
 
akha! ngojeni niwaelimishe!.
Pesa inatengenezwa kwa pesa inamaana BOT wanapotaka pesa mpya wanaipa tenda kampuni fulani halafu hiyo kampuni inalipwa na BOT, na malipo yatafanyika kutokana na pesa zinazohitajika, ubora unaohitajika maana pesa hutengenezwa na madini fulani na kwa kiwango fulani ili isiwe rahisi ku gushi so hizo zote ni gharama!.
Na malipo yatafanyika vile ambavyo wamekubaliana na ni kwa pesa ipi italipwa hiyo kazi!.. haiwezi kulipwa pesa ileile iliyotengenezwa kwa maana ile pesa iliyotengenezwa inakuwa haiwezi kutumika mpaka ipelekwe BOT ipewe namba na ichapwe saini!, so unakuta pesa zipo BOT ila hazina namba na hazina sign hizo hata ukiiba huwezi kuzitumia na pia hao wenye viwanda hawawezi kuprint fedha nyengine kwasababu itahitajika namba na sign na haiishii hapo!, kuna material ambayo yanahitajika yakae kwenye hizo fedha so pia ni gharama na vilevile ku run kiwanda Kutengeneza hizo fedha ni gharama pia!.. yani kiufupi watakaozalisha fedha bila wenye wenyewe kujua watakuwa wameingia hasara wao wenyewe maana mteja unaenda kumuuzia ndio anaeidhinisha hiyo bidhaa na yeye ndie anaetakiwa kufanya special order sio unazalisha kama nguo ya kwamba atajitokeza yoyote tu atanunua!, bali anaenunua ndio anaenda kuipa chapa hiyo bidhaa ili itumiwe!. so ikibainika umefanya uchapishaji bila nchi husika kufanya order hiyo ni kesi nzito mno kwani unacheza na uchumi wa nchi husika!.

Kiujumla pesa inatengenezwa nakutumiwa kwa uangalifu mkubwa na inalindwa sana maana haitakiwi kuzidi kwani ikizidi basi inflation inawalamba na fedha yenu inapoteza thamani!, na nchi nyengine zote wataacha kutumia fedha yenu ktk ku exchange hivyo mtakuwa mnajichoma na ndio maana fedha hufuatiliwa kwa utaratibu na hesabu na sio hivyo tu!, ni lazima ujue namna yakudhibiti pesa fake maana zinaweza kukuharibia uchumi so hata kama zitakuwepo basi kwa kiwango ambacho hakitaathiri maana ni ngumu kudhibiti fedha fake kwa 100%.

Naona watu wanauliza sana juu ya Kutengeneza fedha hewa!, fedha hewa hutengenezwa lakini kwa hesabu ambayo haitaleta shida! na anaeweza Kutengeneza fedha hewa ni serikali na taasisi ya fedha kama BOT.
serikali hutengeneza fedha hewa kwa kupitia mikopo na taasisi ya fedha inaweza Kutengeneza fedha hewa kupitia pesa za floating!, yani pesa za kimtandao ila kwa hesabu maalumu sio kwa kukurupuka!.
 
Shukrani mkuu, nilijua zinatengenezwa Mbagala Kizuiani.
 
Back
Top Bottom