Unajua kuongea lugha ya kabila lako?

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Baada ya miaka michache ijayo nadhani lugha za makabila mengi zitakufa kama si kufutika kabisa.
Kwa mfano:
Wewe umezaliwa Dar ila origin yako wewe ni mtu wa songea ukakuwa Dar ukasomea hapo.
Kijijini wengi wanakwenda kwa ajili ya kuwasabai bibi na babu sasa unakuta hawa kwa bahati mbaya wameshafariki,Hivyo kijijini unakwenda kwa nadra sana hata lugha ya kabila umejifunza kama vile umejifunza kiingereza na haujui vizuri.
Ukaja kuoa mwanamke wa kabila tofauti na wewe mkapata watoto, watoto wakitaka kwenda kwa bibi na babu ni hapo hapo Dar. Wewe mwenyewe hujui kikwenu vizuri kwa sababu ulizaliwa mjini.

Swali linakuja unadhani watoto wako watajuaje lugha ya kwenu kama hata wewe baba na mama hamuijui?
Na ili tatizo limeshaanza kujitokeza sana wengi waliozaliwa miaka ya 80s ni watupu sana kwenye lugha zao.

Sasa kama wewe unajua walau kidogo ebu tuambie ukitaka kumwambia mtu "ASANTE NIMESHIBA"
Unasemaje ki kwenu?
 
Kweli mkuu,kwani huko kijijini hawazaliani? hizo lugha hazijaanza leo na bado zipo, Tunaomba mwanzisha mada afute kauli yake
zimeanza zamani sawa lakini usisahau lugha 1.Inakuwa 2.Inakufa pia, sasa labda inataka kutufia mikononi mwetu ama.
 
Back
Top Bottom