Gaga
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 4,558
- 1,968
kweli kabisa, mtu yupoyupo tu, analoliongea kila siku watu hawamwelewi, pumbapumba tu, na bado anataka watu wamthamini fo who she/he is haoni kama inabidi atumie nguvu ya ziada ili apate thaminiwa na jamii?Ni kweli kujithamini au kuthamini wengine kunatokana na kujitambua wewe binafsi. Na hili kujitambua wewe binafsi inabidi ujue tamaduni za jamii inayokuzunguka iwe kazini, familia au hata Pub. Kwa kujua hilo ndio utaweza kushusha au kupandisha vigezo kutokana na maisha ya jamii hiyo.
Mara nyingi ukijishusha kwa kiasi fulani utakuwa na uwezo mzuri wa kujitambua na kujichaganya na kukubalika na jamii sehemu yeyote hile..hata pale nyumbani kwako jaribu kujishusha na kuthamini kazi za House girl au Houseboy wako..jaribu kumfanya kama mdogo wako na uone matokeo yake.... Pia tukumbuke hakuna kipimo cha thamani..sio cheo, wala hela, wala mavazi, wala mikogo..wala kutoa misaada..vyote hivyo havisaidii kupandisha thamani yako ..Thamani ni kukubalika..na kuheshimika kwa kujishusha kwako albeit ilibidi uwe juu... Hata walevi wanathamani na kuthaminiwa wakikutana kwenye jamii za walevi wenzao..ni utamaduni na vigezo vyao. Hapo utaona thamani inakuja yenyewe na wala sio wewe unayeiweka au kuilazimisha... kikubwa.. Jitambue..jishushe ili wale wanaokuzunguka ndio wakupandishe..