Wakati ukihuzunika huna kandambili kuna watu hawana miguu na wanamshukuru Mungu kwa uhai!!
Mungu ni Mwema sana kila kitu anatupa kwa sababu!! Ni ubinadamu tu unatufanya tushindwe kumwambia ASANTE!
Hakika.
Kila Siku tunalalamika Maisha magumu, Mambo hayaendi sawa, na mifano mingine mingi sana ya manung'uniko.
Tujiulize?!
Je mara ya mwisho ni lini tulikaa kitako, tulipiga magoti, tulichuchumaa, kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zile Neema alizotujalia?
Kuna wangapi tunawafahamu, tunaowafahamu, hivi sasa tunavyoongea wapo Vitandani mwao hawawezi hata kujinyanyua?
Kuna wangapi tunawafahamu, tunaowafahamu, hivi sasa tunavyoongea wanatembelea Magongo, wakati mwanzoni hawakuwa wanatembelea Magongo?
Mifano ni mingi sana.
Tuwe na utaratibu wa KUSHUKURU, kwa kila jambo na kwa kila hali yoyote itakayotukumba/tutakayokutana nayo Kimaisha.
Waungwana Mungu ni mwema sana