Nimejifunza mambo kadhaa kama ifuatavyo:
1.Nimehuzunika sana na tukio hilo,iwe ni hadithi au kweli.
2.Napata funzo kuwa kuna matatizo mengi sana kati yetu sisi binadamu.Hivyo,tunahitaji kusaidiana kila mara pale unapokuwa na uwepo,si tuu kwa fedha bali hata kwa hali.Angalia kuna watu wanamsaidia huyo mtoto baada ya kuona haki hiyo.
3.Haijalishi,unashida kiasi gani bado tusikate tamaa.Hata kama huwezi kupumua bado kuna mashine ya oxygen inaweza kukusaidia kupumua na maisha yakaendelea.
4.Kuwa omba omba si kigezo cha kukosa utu.Pamoja na umasikini wa kijana ombaomba bado ameguswa sana alipomuona mgonjwa,kiasi cha kuoata mshtuko na kutoka machozi.
5.Kuna baadhi yetu(members wa jamii forum) wameguswa na wengine kukejeli.Haidhuru,kwa vile jukwaa hili ni huru naheshimu maamuzi yao.Nimejifunza kuwa ni vyema pia kuheshimu maoni ya wengine hata kama hayafurahishi,cha msingi ni kuendelea kuwa pamoja na kuzidi kuchat tukiwa kama marafiki kundi na hata familia.Niko tayari kukosolewa kwa mchango wangu.Aksante na pongezi kwako KAJOLIJO kwa kuleta uzi huu.