Unaishi vipi na jirani anayependa dezo na kuombaomba?

Ujirani mgumu sana, hasa kama unatumia akili zako sawasawa.

Ngoja nikupe hii leo, mwambie simu huwa unachajia kazini hata kama anakua ni kweli una chaja nyingine.

Ila kama ni aina ya jirani anayenijia akilini mwangu, dawa yake ndogo sana. Ustaarabu mwingi ni utumwa kwa jamii za sasa.
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
itakuwa yeye ndiye anaipasi pasi
 
Una njia tatu utachagua ipi inafaa zaidi
1. Mpe makavu, anunue charger yake hamna haja ya kucheka na nyani.
2. Siku muwahi ujifanye umesahau kama amekurudishia charger yako maana huioni anzisha vurugu mdai charger yako mapaka iwe kesi.
3. Anza kuvuta bangi, mimi majirani mpaka wanawaambia watoto wao wasikatize karibu na kwangu wasijifunze tabia mbaya.
Haa haa kuna watu mmepinda
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
Acha roho mbaya wewe.. kwani kwenye katiba si imeandikwa Tanzania ni nchi ya kijamaa? Sasa wewe huo ubinafsi utakuwa raia wa nchi gani wewe?
 
Najua jirani ni ndugu wa karibu ila kuna mengine yamezidi.

Jirani alikua anakuja kuomba chaji nikaona sio kesi nimenunua nyingine nikamuachia atumie.

Bado basi yake imeharibika hana mpango wa kuitengeneza wala kununua nikaona sikesi usumbufu umezidi nichukue nyingine, sasa naona haajiongezi, chaji ile sijui imekuaje anakuja tena kugonga nimuwekee chaji, waungwana ujirani huu unafanyaje?
Wewe na yeye ni jinsia mbili tofauti? If yes jiongeze mkuu!
 
Natengwa na majirani sababu ya mmea, kuna kisa fulani nikikumbuka mpaka nacheka kuna siku nilikuwa naelekea dukani usiku kununua mkate maana kesho yake nilikuwa nawahi asubuhi sana kutoka.

Kuna mama fulani wa makamo alikuwa anaelekea njia moja na mimi ila yupo mbele yangu ndio anaenda nyumbani kwake sasa nikiongeza mwendo na yeye anaongeza mwendo nisimkaribie mpaka akakata sandals alizokuwa amevaa.

Kumsemesha namuona ana hofu kama anatetemeka na hasira, alibahatisha kuna toyo ilikuwa inapita akaichukua na kwenda nayo umbali haufiki hata nusu kilomita kesho yake nilikuja kusikia stori mtaani eti alinusurika kukabwa na wavuta bangi wa mtaani duh nikajua kumbe najulikana mtaani na na kuogopwa kabisa, hamna mtu mwenye time na mimi wanajua ni mhuni tu anayepuliza mmea kila saa, na mimi nawaacha wanichukulie hivyo hivyo sitaki mazoea

Mkuu haya maisha ya kuomba omba hakuna anaye yapenda inafikia kipindi unapigika haswaa unakosa hata pesa ya kununua mboga,

Wavumilie tu ndugu yangu maisha yanabana sana
Hujakaa na mgogo wewe,ana kazi nzuri tu lkn ataomba omba kila kitu from chaji,chumvi,nyanya,tomato sauce et
Huo ni ujinga unamuambia huna, mtu anayefaa kusaidiwa ni mwenye kipato cha chini
 
Kuna watu nafikiri hiyo iko damuni. Hivyo wachukulie tu hivyo hivyo ukiona its too much mute.
 
Mkuu haya maisha ya kupmba omba hakuna anaye yapenda inafikia kipindi unapigika haswaa unakosa hata pesa ya kununua mboga,

Wavumilie tu ndugu yangu maisha yanabana sana

Huo ni ujinga unamuambia huna, mtu anayefaa kusaidiwa ni mwenye kipato cha chini
Nakwambia hivi wanapenda sana tu,Kama wengine wanakufa na Tai zao shingoni kwanini wao wajifanye omba omba?
 
Najua jirani ni ndugu wa karibu ila kuna mengine yamezidi.

Jirani alikua anakuja kuomba chaji nikaona sio kesi nimenunua nyingine nikamuachia atumie.

Bado basi yake imeharibika hana mpango wa kuitengeneza wala kununua nikaona sikesi usumbufu umezidi nichukue nyingine, sasa naona haajiongezi, chaji ile sijui imekuaje anakuja tena kugonga nimuwekee chaji, waungwana ujirani huu unafanyaje?

Dah Mzee mimi nilipata Jirani isee ni zaidi ya Omba omba kila kitu anaomba as if ndo uliyemleta mjini anaomba kuanzia chakula, pasi, charger, sabuni, chai , mafuta mara nikopeshe hela dah nilimchoma kwa kweli ikafika stage hata cm yake sipokei cz nimemchoka ukiona cm yake au kagonga mlango basi jua unaombwa hii tabia inanikera watu wa namna hii sijui hawanaga mshipa wa aibu isee kuomba ndo kitu siwezag
 
Natengwa na majirani sababu ya mmea, kuna kisa fulani nikikumbuka mpaka nacheka kuna siku nilikuwa naelekea dukani usiku kununua mkate maana kesho yake nilikuwa nawahi asubuhi sana kutoka.

Kuna mama fulani wa makamo alikuwa anaelekea njia moja na mimi ila yupo mbele yangu ndio anaenda nyumbani kwake sasa nikiongeza mwendo na yeye anaongeza mwendo nisimkaribie mpaka akakata sandals alizokuwa amevaa.

Kumsemesha namuona ana hofu kama anatetemeka na hasira, alibahatisha kuna toyo ilikuwa inapita akaichukua na kwenda nayo umbali haufiki hata nusu kilomita kesho yake nilikuja kusikia stori mtaani eti alinusurika kukabwa na wavuta bangi wa mtaani duh nikajua kumbe najulikana mtaani na na kuogopwa kabisa, hamna mtu mwenye time na mimi wanajua ni mhuni tu anayepuliza mmea kila saa, na mimi nawaacha wanichukulie hivyo hivyo sitaki mazoea🐒
Hahahaha kabsa chief hakuna mazoea unakata kbsa mazoea nao wakikuzoea wataanza kuleta dharau
 
Kuna mpangaji mwenzangu hapa ana mume wake bodaboda hajamaliza hata wiki picha linaanza asubhi anamtoa mtoto wake aje kuomba uji au chai yaan yy hapiki sana sana ataenda kununua chai au uji, ukifika mchana hapiki chochote mnachopika anataka mumpatia na yy , yaan wiki tu tushamchoka namuonea huruma sana binti yao maana wakat mwingine hata hawajui amekula nn na Yuko wapi....

Wanaume tuangalie sana wanawake wa kuoa jamani.
 
Hapa ninavo type kuna jirani yangu yupo ndani kashika na remote zote za screen na king’amuzi yani imebidi nitoke tu nje nimwache lakini ikifika mida ya mechi za mpila naenda kumtoa..yan mtu ukimcheki mnaheshimiana lakini mambo yake ukiyatafakari unakuwa unajiuliza inamaana yeye haoni majirani zake wanaishi vipi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom