Unaishi vipi na jirani anayependa dezo na kuombaomba?

Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwenye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
Watu mna dhambii
 
Bora nyie wanawaomba wenyewe jamani sisi tunaoshinda maofisini nyumnba inabaki na dada, akibaki dada wataombana watapeana na hodi zitagongwa.
NIkiwa nipo home husikii hodi wala kuombana.
Yaani kuna siku wameombana kisamvu ile nimefika kisamvu kimeingizwa na dada ndani.
Kumuuliza anasema nilikuwa na hamu nacho.
Nikamuuliza ulishindwa nini kuchuma ukatwanga na kupika ili tule nyumba nzima?je na wewe huwa unampa nini hadi yeye akupe kisamvu?na kama unampa hivi vitu ni vyako?

Mind you kisamvu nimepanda uwanjani kwangu, nazi na karanga zipo ndani.
huyo ni balaa alimpa mpka kisamvu marinda yalipona kweli
 
Someni hapa chini Mnaoomba ombaView attachment 1987768

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
Kumbe hata vtabu vya Mungu vinajua? Kuna wahuni walikua wanakuja gheto wanashika remot zote hata nikiwa kazin wananipigia sim nawaachia funguo mwsho wa siku mazoea yakazidi wakaanza had kuamisha baadhi ya vtu vyangu kutoka sehem moja had nyingine
Sahiv nimewakinai ni full ukauzu had wanajiuliza hivi huyu mwana ndo yule?

Maana ilifika hatua nilikua nikiwa nimelala mchna wanagonga mlango nisipoitika wanafungua wanaingia ndan wanawasha Tv hiyo ndo iliniuma zaid, pia Kuna siku demu alikuja kunitembelea wanaona Niko na demu lakin nao wamekaza hawaondok wamekaa hapohapo had muda ukaisha daah

Kwa Sasa nimewakinai balaa stak mazoea maana kwa mazoea yalipokua yamefikia ipo siku hata nikioa watakua wanakuja kwa mke wangu kunyang'anyana nae remote hawana mipaka wakat mm nina mipaka na uhuru wao
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwenye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
Duuh! 😂😂
 
Najua jirani ni ndugu wa karibu ila kuna mengine yamezidi.

Jirani alikuwa anakuja kuomba chaji nikaona sio kesi nimenunua nyingine nikamuachia atumie.

Bado basi yake imeharibika hana mpango wa kuitengeneza wala kununua nikaona sikesi usumbufu umezidi nichukue nyingine, sasa naona haajiongezi, chaji ile sijui imekuaje anakuja tena kugonga nimuwekee chaji, waungwana ujirani huu unafanyaje?
 
Bora nyie wanawaomba wenyewe jamani sisi tunaoshinda maofisini nyumnba inabaki na dada, akibaki dada wataombana watapeana na hodi zitagongwa.
NIkiwa nipo home husikii hodi wala kuombana.
Yaani kuna siku wameombana kisamvu ile nimefika kisamvu kimeingizwa na dada ndani.
Kumuuliza anasema nilikuwa na hamu nacho.
Nikamuuliza ulishindwa nini kuchuma ukatwanga na kupika ili tule nyumba nzima?je na wewe huwa unampa nini hadi yeye akupe kisamvu?na kama unampa hivi vitu ni vyako?

Mind you kisamvu nimepanda uwanjani kwangu, nazi na karanga zipo ndani.
Alooo hadi kisamvu kinatafutwa kwa uvumba
 
Kumbe hata vtabu vya Mungu vinajua? Kuna wahuni walikua wanakuja gheto wanashika remot zote hata nikiwa kazin wananipigia sim nawaachia funguo mwsho wa siku mazoea yakazidi wakaanza had kuamisha baadhi ya vtu vyangu kutoka sehem moja had nyingine
Sahiv nimewakinai ni full ukauzu had wanajiuliza hivi huyu mwana ndo yule?

Maana ilifika hatua nilikua nikiwa nimelala mchna wanagonga mlango nisipoitika wanafungua wanaingia ndan wanawasha Tv hiyo ndo iliniuma zaid, pia Kuna siku demu alikuja kunitembelea wanaona Niko na demu lakin nao wamekaza hawaondok wamekaa hapohapo had muda ukaisha daah

Kwa Sasa nimewakinai balaa stak mazoea maana kwa mazoea yalipokua yamefikia ipo siku hata nikioa watakua wanakuja kwa mke wangu kunyang'anyana nae remote hawana mipaka wakat mm nina mipaka na uhuru wao
Hayo ndio maisha ndugu hakuna mkamilifu kama uwezo wa kumsaidia kila akiomba unao we toa tu .
Akuna mtu anapenda kuomba omba , alie kupa wewe ndiye huyo huyo aliye mnyima mwenzio.
Kwaiyo ni kuvumiliana tu na kuoneana huruma madhali unacho basi we toa tu.
 
Kwa mujibu wa Imani yangu naamini ya kuwa
"Ukijivisha vazi la kuombakuomba Mungu anakuvisha vazi la ufukara"

Kusaidiana ni kitu kizur lakin unaposaidiwa usijisahau kiasi Cha kuwa kero kwa anaetoa msaada hiyo pia ni dhambi, haiwezekan mtu anakufanyia wema had inafika hatua unajisahau unauona msaada wake kuwa ni kitu Cha lazma ww kuupata yan inakua kma vile unamuwajibisha mtoa msaada

Wakat huo huyo unaemuombaomba kila siku yeye anajitahidi kutokua kero kwako tena hakuombiombi had kiasi Cha ww kujiskia kero, jamii zinatakiwa zibadilike, ikiwa mtu anakufanyia wema wa msaada Basi na ww mfanyie wema wa kutokumuombaomba sana
 
Najua jirani ni ndugu wa karibu ila kuna mengine yamezidi.

Jirani alikuwa anakuja kuomba chaji nikaona sio kesi nimenunua nyingine nikamuachia atumie.

Bado basi yake imeharibika hana mpango wa kuitengeneza wala kununua nikaona sikesi usumbufu umezidi nichukue nyingine, sasa naona haajiongezi, chaji ile sijui imekuaje anakuja tena kugonga nimuwekee chaji, waungwana ujirani huu unafanyaje?
Mbona maisha hayo yalishapitwa sana na wakati jamani?

Maisha ya kuazimana nguo, viatu makoti, sijui chaja and the like ni ya kizamani!

Hayo ni mazoea ya ndani sana na ni dharau pia.

Halafu usije ukafikiri ni wema huo, kuzoea ku share vitu baadaye huleta majungu na kubweteka kwa utegemezi pamwe lawama.

Ujirani ni kusaidiana ndiyo, lakini kwa issue kubwa kubwa za dharula tu na si mambo ya kizembe yanayochukua muda kuyatanzua kama ya hilo la pasi na chaja.

Vitu ambavyo ni vya lazima katika maisha ya mtu ni muhimu kuvinunua na kuwa navyo.

Vinginevyo wakati mtu anajiandaa kuvinunua, avumilie, awe na subira na si lazima ku expose dhiki zake na kusumbua watu.

Tatizo usiyapodhibiti mazoea mapema hasa unapohamia sehemu kuanza maisha, baadaye mazoea hayo hugeuka na kuwa adha kubwa na kupoteza uhuru wako wa falagha.

Ukitaka kubadilika, weka kanuni kwa familia kwamba, kila jirani anapokuja kuazima kitu, atolewe nje kwa kuelezwa kwamba kitu hicho hakipo, kauli fupi na bila blah blah.

Halafu vitu vyote vinavyotamanisha kuazimwa vikae ndani ama store.

Akifanyiwa hivyo mara mbili hawezi kuendeleza mazoea yake kwako na ataacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nimemuachia mungu karibia mtaa mzima simu wanachaji kwangu bure maji wanaleta chupa niwawekee kwenye friji bule mniombee tu
 
Kuomba siyo mbaya ila kuna kuomba kimazoea ,mtu akikwama sawa ila siyo kila siku,mpaka mtu anakuachia hiyo kitu bado hujiongezi kwamba namsumbua?.

Nyumbani kuna jirani anapenda sana kuja kuomba jiko la mkaa ingawa sisi tunatumia la gesi ila mkaa kwa ajili ya vitu kama maharage na nyama maana vinachukua mda kuiva.

Basi akiomba atakaa nayo hata week mpaka we uhitaji sometimes unaweza kuta hata hayupo,tukamwachia tukanunua nyingine kwa ajili ya usumbufu ,baadaye anakuja kuomba tena ile eti ile tuliyomwachia ni ndogo. Basi wife anaonaona aibu utakuta tamthiliya ya Azam ikifika kama haupo wamama watu wazima wamejazana sebuleni hata hamna sehemu ya kupitisha mguu.

Siku moja nimepiga zangu tungi nimelala nashtuka natoka na kiboxer kifupi wamama wamejazana sebuleni wanaangalia tamthiliya ,na Ile wengi la pombe niliwachana kwamba sisi kama familia humu kuna mambo mengi na tunataka Uhuru sipendezwi na usumbufu wa kila siku hapa .

Hawajarudi tena
 
Mkuu haya maisha ya kuomba omba hakuna anaye yapenda inafikia kipindi unapigika haswaa unakosa hata pesa ya kununua mboga,

Wavumilie tu ndugu yangu maisha yanabana sana
Mkuu kuomba ni tabia ya mtu na Wala sio shida, kuna mtu ana shida.na bado haombi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom