Unaishi vipi na jirani anayependa dezo na kuombaomba?

Maleven

Senior Member
Sep 8, 2019
141
1,000
Najua jirani ni ndugu wa karibu ila kuna mengine yamezidi.

Jirani alikuwa anakuja kuomba chaji nikaona sio kesi nimenunua nyingine nikamuachia atumie.

Bado basi yake imeharibika hana mpango wa kuitengeneza wala kununua nikaona sikesi usumbufu umezidi nichukue nyingine, sasa naona haajiongezi, chaji ile sijui imekuaje anakuja tena kugonga nimuwekee chaji, waungwana ujirani huu unafanyaje?
 
bwii

JF-Expert Member
May 24, 2014
1,262
2,000
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwenye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
6,679
2,000
Una njia tatu utachagua ipi inafaa zaidi

1. Mpe makavu, anunue charger yake hamna haja ya kucheka na nyani.

2. Siku muwahi ujifanye umesahau kama amekurudishia charger yako maana huioni anzisha vurugu mdai charger yako mapaka iwe kesi.

3. Anza kuvuta bangi, mimi majirani mpaka wanawaambia watoto wao wasikatize karibu na kwangu wasijifunze tabia mbaya.
 
fundi bishoo

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
7,468

Hahahaa kisa unavuta bangii
 
danielhipoliti

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
819
1,000
Mkuu mbona kama unanisemea?

Aiseee watu watasema maisha magumu sijui nini?

Ila Mkuu trust me asilimia kubwa watu wa ivyo ni kujiendekeza Tu.

Kuna jirani yangu kaolewa leo katoka kumuambia wife eti Mtoto wake awe anampa chakula yeye kaondoka na anarudi Jmosi

Mtoto mwenyewe sio kusema mtoto ni Dogo tu mkubwa na Baba yake yupo na hajaacha chochote ,.

Anafosi mazoea ya kipuuzi tu swala la chaji niliwatolea nje maana mtu ukitaka chaji mpaka mfate na ni yako
 
Fredy Frank360

Senior Member
Dec 25, 2018
126
250
Una njia tatu utachagua ipi inafaa zaidi
1. Mpe makavu, anunue charger yake hamna haja ya kucheka na nyani.
2. Siku muwahi ujifanye umesahau kama amekurudishia charger yako maana huioni anzisha vurugu mdai charger yako mapaka iwe kesi.
3. Anza kuvuta bangi, mimi majirani mpaka wanawaambia watoto wao wasikatize karibu na kwangu wasijifunze tabia mbaya.

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
6,679
2,000
Hahahaa kisa unavuta bangii
Natengwa na majirani sababu ya mmea, kuna kisa fulani nikikumbuka mpaka nacheka kuna siku nilikuwa naelekea dukani usiku kununua mkate maana kesho yake nilikuwa nawahi asubuhi sana kutoka.

Kuna mama fulani wa makamo alikuwa anaelekea njia moja na mimi ila yupo mbele yangu ndio anaenda nyumbani kwake sasa nikiongeza mwendo na yeye anaongeza mwendo nisimkaribie mpaka akakata sandals alizokuwa amevaa.

Kumsemesha namuona ana hofu kama anatetemeka na hasira, alibahatisha kuna toyo ilikuwa inapita akaichukua na kwenda nayo umbali haufiki hata nusu kilomita kesho yake nilikuja kusikia stori mtaani eti alinusurika kukabwa na wavuta bangi wa mtaani duh nikajua kumbe najulikana mtaani na na kuogopwa kabisa,

hamna mtu mwenye time na mimi wanajua ni mhuni tu anayepuliza mmea kila saa, na mimi nawaacha wanichukulie hivyo hivyo sitaki mazoea🐒
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom