Unafungia mtandao wa X, lakini wewe upo na unatuma maudhui! 😳

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,335
Reaction score
3,140
Wakuu kuna jambo ambalo nimelitafakari bila kupata majibu toka serikali ilipofungia mtandao wa X almaarufu Twitter.

Nimeshindwa kuelewa hii serikali inaendeshwa na wendawazimu ama vichaa kwakuwa kwa yanayoendelea ni udhihirisho tosha kuwa ni watu wasio na weledi, reasoning na hata common sense ndio waliopewa mamlaka ya kufanya maamuzi.

Hili la kufungia mtandao wa X ni uthibitisho usio na shaka kuhusu hilo.

Yani serikali inafungia X, kwa maana hiyo hakuna mtanzania anaetakiwa kuweza ku access X (achana na VPNs, yani dhumuni la serikali ni kuwa hakuna Mtanzania anaetakiwa kuwa na access na X).

Hiyo sio shida iko sawa.

Sasa changamoto inaanza kuja kuwa hao hao waliofungia X wanaendelea kupost huko X kila siku, sio rais wa nchi, sio msemaji wa serikali, sio jeshi la polisi n.k

Sasa unajiuliza kama mamlaka zimezuia watanzania kutumia X je hizo post wanazotuma huko huwa wanatuma ili zisomwe na nani?

Kuna logic hapo?

Yani hapo ni sawa na, kwamfano. Wewe una mamlaka una kanisa lako na lina waumini halafu unawakataza waumini wako wasije kanisani halafu wewe unaenda kanisani unaanza kuhubiri penye hamna watu.

Hivi sisi hii nchi tupoje?
 
Hahaha hii nchi bhna, me nawaambiaga hii nchi inaendeshwa kiutani utani sana. Hatuna rais tusubiri 2030 labda watatuletea rais mwenye akili.
Alafu JWTZ mbona kama hawayajui majukumu yao? Si wapindue wachukue uongozi ili watu washike adabu
Kuna kuna vitu vya kijinga sana vinafanywa mpaka unajiuliza unashindwa kuelewa?
 
Wanasema kuna porno kule kwenye X ndio maana wameufungia. Tafsiri yake ni kwamba hizo porno wanataka iwatazame wao na bosi wao peke yao.
Sasa mbona matamko na taarifa za kiserikali wanaendelea kupost huko X ambako wamezuia watanzania kuwepo?

Wanampostia nani huko?
 
Wao wanaingia huko kutazama porno , si ndio maana yao kusema kule kuna porno
 
Raia wa kawaida Wana weledi kuliko walioko serekalini ,, Taifa Lina viongozi wajinga sana . Mitandao ya kijamii ni platform ya biashara kwa wengine ,ndiko wengine wanako patia riziki zao . Kuufungia ni kuwakosea watu sana.
 
Wakuu kuna jambo ambalo nimelitafakari bila kupata majibu toka serikali ilipofungia mtandao wa X almaarufu Twitter.

Nimeshindwa kuelewa hii serikali inaendeshwa na wendawazimu ama vichaa kwakuwa kwa yanayoendelea ni udhihirisho tosha kuwa ni watu wasio na weledi, reasoning na hata common sense ndio waliopewa mamlaka ya kufanya maamuzi.

Hili la kufungia mtandao wa X ni uthibitisho usio na shaka kuhusu hilo.

Yani serikali inafungia X, kwa maana hiyo hakuna mtanzania anaetakiwa kuweza ku access X (achana na VPNs, yani dhumuli la serikali ni kuwa hakuna Mtanzania anaetakiwa kuwa na access na X).

Hiyo sio shida iko sawa.

Sasa changamoto inaanza kuja kuwa hao hao waliofungia X wanaendelea kupost huko X kila siku, sio rais wa nchi, sio msemaji wa serikali, sio jeshi la polisi n.k

Sasa najiuliza kama mamlaka zimezuia watanzania kutumia X je hizp post wanazotuma huko huwa wanatuma ili zisomwe na nani?

Kuna logic hapo?

Yani hapo ni sawa na, kwamfano. Wewe una mamlaka una kanisa lako na lina waumini halafu unawakataza waumini wako wasije kanisani halafu wewe unaenda kanisani unaanza kuhubiri penye hamna watu.

Hivi sisi hii nchi tupoje?
Ni maajabu hayo!!
 
Hahaha hii nchi bhna, me nawaambiaga hii nchi inaendeshwa kiutani utani sana. Hatuna rais tusubiri 2030 labda watatuletea rais mwenye akili.
Alafu JWTZ mbona kama hawayajui majukumu yao? Si wapindue wachukue uongozi ili watu washike adabu
mkuu wa majeshi anateuliwa na nani
pigia mstari hapo
 
Back
Top Bottom