Eti baada ya machafuko ya Iraq Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa United States of Amerika wapo against any genocide hapa duniani hivyo wakaenda Iraq kutuliza amani.
Swali
Kinachotokea huko Gaza sio genocide? kwanini Marekani Polisi wa dunia ameshindwa na hatuoni meno yake katika kutuliza au kuwapunish Israel kwa wanayoyafanya?
Imani yetu binadamu inatufanya tusiwaone wale watoto na wazazi wanaofariki Gaza kama ni wanadamu, utakuta mkristo anasema waache wafe tu.
Mimi ni mkristo kwa imani ila kamwe sintokubali haya mauaji ya waisrael wanayoyafanya eti kisa imani kwanza wewe kama ni mkristo halafu unasupport mauaji kwa kweli wewe ni mkristo jina.
Tuupinge huu unafIki wa Wamarekani na washirika wake katika kutuliza amani na demokrasia ya dunia.
Unapoanzisha uzi humu JF jifunze kuwa mtafiti wa jambo husika kwanza na si kuandika kwa mlengo fulani au kelele za watu fulani.
Israel hawalengi kuua raia isipokuwa magaidi wa Palestina wanawatumia raia-watoto na wanawake zaidi kama kinga ya kulinda roketi zao wazirushazo kuwaua wa-israel...Israel mara zote hutoa taarifa maeneo ambayo inadhani kuna magaidi na muda wa kupiga- soma
Thousands flee Gaza homes after Israeli warning of large-scale bombing | World news | The Guardian lakini raia wajinga hudanganywa kuwa wanapigania nchi yao na dini ndiyo maana hufumuliwa mara zote, BINAFSI NAWASAPOTI ISRAEL.
Wakristo jina,hawatakuunga mkono.
wakristo wote ni wa majina,imani dhahiri iko nafsini kwa mtu binafsi na si kwa maandishi, kwani hata matendo mema vile vile yaweza kuwa ni ya kinafki-ajuae ukweli wa nafsi zetu ni Mungu pekee-ambaye ni wetu sote(wakristo,waislam na wengine)
ni washenzi sana ha wa U.S.A
Wawaona washenzi lakini huishi kuwalamba miguu kuomba misaada.
haha,, hebu weka imani pembeni shirikisha ubongo wako, kwahyo bible inasema ni ruksa kwa waisrael kuwaua wengine wasiokuwa wayahudi...kwani Mungu si Mungu wa wote iweje apitishe kikundi kimoja cha watu kiwauwe wengine na kiwe juu na kipewe heshima zadi ya wote???kwann asingewaumba waisrael peke yao
Hata magaidi hawakuambiwa wawaue wengine. Mungu hakutupatia uhai ili tujiue (kujitoa muhanga) bali tuishi kwa amani,tumjue,tumtumikie na mwisho tufike kwake tena.
pole sana kaka kwa kuongozwa na udini na imani iliyokujengea chuki kubwa mno kiasi cha kutoona mabaya hadi kuuwawa kwa wanadamu wenzetu,, naomba utambue kuwa Mungu wa kweli hajawahi kuthibitisha mauaji ya watu wake na kikundi kinachotumia jina lake maana sote ni wana wa Mungu kabla ya imani zetu, kingine ni kuwa hizo picha za watoto zinaonyeshwa na mashirika ya washirika wa waisrael na marekani nikimaanisha BBC, skynews, Cnn na wengineo, M
Fanya tafiti kwanza,usi-comment kwa kuongozwa na emotions zako...unaweza ku-google,sikiliza habari n.k halafu pima pande zote kabla hujafanya unfair judgements zako hapa.
Ni kweli mkuu. Hawa jamaa wameshatuona sisi kama watoto wadogo. wanavyosema tunakubali. Lakini yana mwisho haya. Dunia sasa imechoka na uuu ujinga wa mmarekani na muyahudi. Watu wengine wanashabikia eti kwakuwa imeandikwa israel ni taifa la mungu. Lakini hawaelewi kilichoandikwa kwenye Biblia kina maana gani.
Wamemuua yesu, eti waacheni ni taifa la mungu. Wanaua watoto eti ni taifa la mungu. Wana classes. wanabagua waisrael wenye asili ya black, eti ni taifa la mungu.......LOL
Wakuone wewe mtoto ili wafaidike na nini?acha kujijaza ujinga tu.
Kwanini usikatae wanachosema na rais wako anaenda huko marekani kila kukicha,unasema nini...acha unafki.
Wewe wauona ujinga wenzako kwao maarifa.Yasiyokuhusu achana nayo-utapasua kichwa bure.
wakristo wengi haatutaki kufuatilia ukweli halisi nje ya biblia, tunasoma biblia kama hadithi halafu tunashabikikia mauaji ya wenzetu, hii ni aibu maana huko middle east pia kuna wakristo kibao
umekurupuka wewe...wakristo hatukariri biblia wewe,unaisoma,unaielewa na kuitekeleza kulingana na mazingira husika.
Hata biblia insema jipiganie nami nitakupigani...fuatilia ujue kwanza nani aliamza kumshambulia mwenzie.