Unafiki wa mitandao,na nguvu yao ya soda

Unafiki wa mitandao,na nguvu yao ya soda

Hakuna haja ya maandamano, kesi iko Mahakamani. Watu ilikuwa twende kumpa sapoti ya kusikiliza kesi, wao ndiyo waoga wakabadilisha usiku kuwa itatumia kuendesha kesi mtandaoni.

Hakuna aliyetaka kuleta vurugu, kwenda kusikiliza kesi kuna ubaya gani? Wewe ulitaka maandamano yafanyike ya nini? Wao waliogopa hiyo sapoti tungeionyesha pale Kisutu.

Hawana lingine, fikiria pesa zilizotumika wiki nzima kwa policcm kabla ya kesi, zingetumika kwenye mambo ya kutatua kero za kijamii. Waache uoga na kuona TAL ataonekana anapendwa ni anapendwa kuliko yeye.
Kaeni nyumbani mtulie, viherehere vyenu tu na hamjaitwa
 
Ni upotevu wa muda na Majanga ya kujitakia kushindana na Dola , hata Uislamu umesisistiza watu wasitoke dhidi ya mtawala hata akiwa muovu kutokana na madhara ya Hilo jambo kwa mtu mmoja mmoja , machafuko na kuondoka kwa Amani katika eneo husika.
Jambo linalokera zaidi ni kwamba mtu yupo mtandaoni halafu anahamasisha fujo na asilimia ya waandamanaji wengi huwa ni masikini
 
Ukiitazama mitaa Kwa haraka haraka imetulia Sana yaani watu wapo makazini kama kawaida,wengine wamelewa asubuhi tu, wengine wanasafiri, wengine wanaingia misikitini n.k

Yaani ni kama hakuna kinachoendelea lakini ukweli ni kwamba ukiingia mtandaoni unaweza sema Tanzania itahamia kisutu.
Kila mtu anaongea kama vile kanywa maji ya bendera.

Rai yangu ni kwamba kuna muda kunyamaza ni Bora zaidi kuliko kukaa kwenye PC na kuamrisha watu waandamane ikiwa wewe upo nje ya nchi au upo hapa nchini lakini huwezi kujitokeza kudai hicho unachokiita haki.

Mwenyekiti wa CDM Mh Tundu Lissu yupo ndani na Leo hii kagoma kesi isiendeshwe Kwa njia ya mtandao lakini atatoka tu.

Makamu mwenyekiti CDM Mh John Heche naye alikamatwa juzi akaachwa ,pia leo alikamatwa asubuhi lakini ataachiwa tu.

Katibu mkuu wa CDM John Mnyika naye amekamatwa asubuhi wakati akielekea huko mahakamani kisutu kusikiliza kesi ya mwenyekiti wa CDM taifa.lakini ataachiwa tu,

Hawa ni watu wanajulikana na ni vigumu kusota mahabusu Kwa muda mrefu. Hao ni unaowajua.

Lakini ukweli ni kwamba selo zimejaa watoto wa masikini wanaodanganywa na kundi la watu wachache wanaoendesha harakati kinadharia huku mbwa Koko na vijana wapenda sifa wakizolewa na kuwekwa Lockup haijulikani watatoka lini.

Watanzania wenzangu tuache harakati uchwara huku wenzenu wanaumia na nyinyi mnaendelea Kula maisha mtaani.

Tuseme wajinga ndiyo waliwao

Mada imekaa kidalali dalali. Vipi ina udhamini wa mama au g-55?
 
Kaeni nyumbani mtulie, viherehere vyenu tu na hamjaitwa

Screenshot_20250306-183123_1.jpg
 
Kwanza unatype ukiwa wapi isije kuwa upo ofisini ama nyumbani kwako?

Watu tunajua uko CDM headquarter
Naweza kuwa nyumbani , ofisini au Chadema HQ.

Ila swali ninalokuuliza hawa Chadema mnaowaona mitandaoni ni watu halisi au maroboti?

Ikiwa Chadema Ina idadi kubwa ya wafuasi mtandaoni ni kitu kizuri Sana kwakuwa hao wafuasi sio maroboti ni real human being.
 
Mada imekaa kidalali dalali. Vipi ina udhamini wa mama au g-55?
Nawaonea huruma watoto na vijana wa kitanzania ambao wanazidi kujaza selo na hawajulikani watatoka lini.

Kama maisha yako unaendesha Kwa njia ya udalali pole Sana huna tofauti na anayebet
 
Naweza kuwa nyumbani , ofisini au Chadema HQ.

Ila swali ninalokuuliza hawa Chadema mnaowaona mitandaoni ni watu halisi au maroboti?

Ikiwa Chadema Ina idadi kubwa ya wafuasi mtandaoni ni kitu kizuri Sana kwakuwa hao wafuasi sio maroboti ni real human being.
Pole
 
Nawaonea huruma watoto na vijana wa kitanzania ambao wanazidi kujaza selo na hawajulikani watatoka lini.

Kama maisha yako unaendesha Kwa njia ya udalali pole Sana huna tofauti na anayebet

Kwani wewe ni gombe?

Screenshot_20250306-183123_1.jpg
 
dunia nzima inakutana kwa mtandaoni lakini chedema hawataki kuskia habari ya tehama kabisa dah :pedroP:
Mtandao upi huu ambao mawakili wa jamhuri muda wote wanasema kuwa hawasiikii vizuri ifikie mahali mkubali ccm ni kukundi Cha wahuni
 
UKIONA UNA FIKRA KAMA HIZO BASI WEWE HATA KUISHI HUKUTAKIWA
NI KAMA MAITI
BINADAMU LAZIMA UWE NA CHANGAMOTO YA KUWA NA MSIMAMO NA MAISHA YAKO NA YA VIZAZI VIJAVYO.
SUSTAINABILITY-------------------------
We umechukua hatua gani?......
au ndio hichi ulicho andika ukiwa chumbani?
 
Wewe baba yako au mama yako walijitokeza wakati Nyerere anapigania Uhuru??
Wote wanaopigania uhuru hawagi wengi, ila sasa hivi wewe unakula matunda ya Uhuru ambao Nyerere alipigania.

Lisu ana nia na atafika-----------hamna wa kumzuia lbda muueni na hauliki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Unatoa kauli hii ukiwa chumbani unajichubua.
Kama wewe hauwezi unategemea nani ataweza?
 
Mtandao upi huu ambao mawakili wa jamhuri muda wote wanasema kuwa hawasiikii vizuri ifikie mahali mkubali ccm ni kukundi Cha wahuni
relax gentleman changia bila kuropoka 🐒
 
Jack Ganiel Kama ilivyo Pombe haijaeahi kuleta utimamu was Akili.
Bado kipara Mpya ni Cancer nayo.
 
Mabadiliko ndivyo yanavyoanza, usitegemee leo kesho mambo kulipuka ila yatalipuka tu.
 
Back
Top Bottom