Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,690
- 19,109
Ukiitazama mitaa Kwa haraka haraka imetulia Sana yaani watu wapo makazini kama kawaida,wengine wamelewa asubuhi tu, wengine wanasafiri, wengine wanaingia misikitini n.k
Yaani ni kama hakuna kinachoendelea lakini ukweli ni kwamba ukiingia mtandaoni unaweza sema Tanzania itahamia kisutu.
Kila mtu anaongea kama vile kanywa maji ya bendera.
Rai yangu ni kwamba kuna muda kunyamaza ni Bora zaidi kuliko kukaa kwenye PC na kuamrisha watu waandamane ikiwa wewe upo nje ya nchi au upo hapa nchini lakini huwezi kujitokeza kudai hicho unachokiita haki.
Mwenyekiti wa CDM Mh Tundu Lissu yupo ndani na Leo hii kagoma kesi isiendeshwe Kwa njia ya mtandao lakini atatoka tu.
Makamu mwenyekiti CDM Mh John Heche naye alikamatwa juzi akaachwa ,pia leo alikamatwa asubuhi lakini ataachiwa tu.
Katibu mkuu wa CDM John Mnyika naye amekamatwa asubuhi wakati akielekea huko mahakamani kisutu kusikiliza kesi ya mwenyekiti wa CDM taifa.lakini ataachiwa tu,
Hawa ni watu wanajulikana na ni vigumu kusota mahabusu Kwa muda mrefu. Hao ni unaowajua.
Lakini ukweli ni kwamba selo zimejaa watoto wa masikini wanaodanganywa na kundi la watu wachache wanaoendesha harakati kinadharia huku mbwa Koko na vijana wapenda sifa wakizolewa na kuwekwa Lockup haijulikani watatoka lini.
Watanzania wenzangu tuache harakati uchwara huku wenzenu wanaumia na nyinyi mnaendelea Kula maisha mtaani.
Tuseme wajinga ndiyo waliwao