ZeMarcopolo and WanajaJF,
Mosi,Hakuna mahali popote iwe kwenye vikao au mahali pengine nilipowahi kutamka haya yaliyoandikwa hapa.Labda mleta mada alete ushahidi hapa
Pili,Tamko langu kuhusu PM-7 lipo huku.
Tatu,Kama nilipongezwa kwa kiwango anachodai mleta mada hapa sasa iweje nipewe adhabu ya kusimamishwa kugombea nafasi yoyote kwa muda wa mwaka 1 sambamba na onyo kali
Nashukuru Mungu uchaguzi haukufanyika mwaka huu kama ilivyopangwa maana ningekosa haki ya kuchaguliwa.Mipango ya Mungu si kama mipango yetu wanadamu
Nne,Naomba niweke hili very clear.Sijawahi kuwa au kutumiwa na Dr.Slaa au kiongozi yeyote wa CHADEMA kwa maslahi binafsi.
Hizi ni hoja mufilisi na visingizio vya washirika wangu wa Zamani katika mkakati haramu waliokasirishwa na kitendo changu cha kusimamia maslahi ya chama na kuwaanika hadharani baada ya mimi binafsi kufanya kazi kubwa ya kuwasihi waache mpango huo maana wangekivuruga chama
Kwa muda wa takribani siku 345 hadi leo hii wamekua wakinishambulia na kunitukana lakini mwisho wa siku walikiri kupanga njama chafu.Ukweli siku zote husimama juu ya unafiki,usaliti na njama ovu za kuuficha ukweli.Kilichotokea Alhamisi iliyopita ni Matokeo ya jitihada za ukweli uliofanikiwa kulipa kisasi baada ya kupuuzwa kwa muda mrefu
Tano,WANACHADEMA,Wapendamabadiliko na watanzania kwa ujumla nawaahidi kuendeleza mapambano na wale wote wanaozuia harakati za mabadiliko ndani na nje ya chama chetu
Nitaendelea kusimamia misingi ya chama chetu na taifa bila kuchoka hadi tone langu la mwisho la damu.Namuomba mwenyezi Mungu anipe nguvu na ujasiri katika mapambano haya.Tuwapuuze wale wote wanaojaribu kututoa katika mstari wa mapambano.
Katika harakati hizi za mabadiliko na malengo ya CHADEMA kitaasisi katika kuongoza vuguvugu hili Doctrine yangu ni 'It's either you are with us or against us'.Hakuna middleground hata kama dunia ni three dimension.Kipimo nitakachompimia msaliti yeyote wa mabadiliko haya ndani ya chama hakitakua na tofauti na kile nitakachotumia dhidi ya wapinzani na maadui wa mabadiliko nje ya chama.
CC:
Invisible,
Fang,
Buchanan,
Paw,
PainKiller Moderator