UNAFIKI unatawala Bavicha...

Status
Not open for further replies.

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,019
7,223
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Miezi kadhaa iliyopita jumuiya ya vijana ya Chadema, Bavicha, ilitangaza kumvua uongozi na kumfukuza uanachama aliyekuwa makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bi. Juliana Shonza. Kosa lake lilitangazwa kuwa ni "usaliti".

Aliyefichua "usaliti" huo ni Ben Saanane a.k.a Mida Eight ambaye alielezwa kuwa alipewa kazi maalum ya kuspy vijana wenzake.

Katika katiba na kanuni za chama HAKUNA kazi hii ya uspy aliyopewa Ben Saanane.

Vijana wengi wa bavicha hasa hapa JF walimpongeza Ben Saanane na kumuona shujaa. Mpaka leo uspy huo alioufanya Ben Saanane ndio jambo pekee linalomfanya aonekane insider wa Chadema.

Mkakati wa siri wa kumpa Ben Saanane kazi ya kuspy ndani ya chama haukuhusisha vikao halali vya chama. Ndio maana viongozi wakuu wa Chama na wajumbe wa Kamati Kuu hawakuwa na taarifa yoyote juu ya kazi hii ya Ben Saanane. Hii ilikuwa ni kazi binafsi ya Dr. Slaa. Ben Saanane alikiri kwenye kikao halali cha Bavicha kuwa alifanya kazi ya uspy na kikao hicho kikampongeza kwa kazi nzuri!

Ni UNAFIKI wa hali ya juu kuona vijana waliounga mkono uwepo wa mikakati ya siri ya Dr. Slaa kumtumia Ben Saanane wakipinga mwanazuoni Dr. Kitila Mkumbo kuwa na mikakati ya siri.

Je, kuna mtu mwenye hati miliki ya mikakati ya siri ndani ya Chadema?

Jumuiya ya vijana katika chama chochote ndio nguzo na dira ya chama. Unafiki huu unaotawala Bavicha unadhihirisha kuwa Chadema sasa haina dira na nguzo yake imeliwa na mchwa.

-------------------------

ZeMarcopolo and WanajaJF,

Mosi,Hakuna mahali popote iwe kwenye vikao au mahali pengine nilipowahi kutamka haya yaliyoandikwa hapa.Labda mleta mada alete ushahidi hapa.JF ikiwa mleta mada hataleta ushahidi wa haya ikiwa ni pamoja na minutes za vikao achukuliwe hatua kwa kusema uongo.Nampa masaa 3 .

Pili,Tamko langu kuhusu PM-7 lipo huku.

Tatu,Kama nilipongezwa kwa kiwango anachodai mleta mada hapa sasa iweje nipewe adhabu ya kusimamishwa kugombea nafasi yoyote kwa muda wa mwaka 1 sambamba na onyo kali

Nashukuru Mungu uchaguzi haukufanyika mwaka huu kama ilivyopangwa maana ningekosa haki ya kuchaguliwa.Mipango ya Mungu si kama mipango yetu wanadamu

Nne,Naomba niweke hili very clear.Sijawahi kuwa au kutumiwa na Dr.Slaa au kiongozi yeyote wa CHADEMA kwa maslahi binafsi.

Hizi ni hoja mufilisi na visingizio vya washirika wangu wa Zamani katika mkakati haramu waliokasirishwa na kitendo changu cha kusimamia maslahi ya chama na kuwaanika hadharani baada ya mimi binafsi kufanya kazi kubwa ya kuwasihi waache mpango huo maana wangekivuruga chama

Kwa muda wa takribani siku 345 hadi leo hii wamekua wakinishambulia na kunitukana lakini mwisho wa siku walikiri kupanga njama chafu.Ukweli siku zote husimama juu ya unafiki,usaliti na njama ovu za kuuficha ukweli.Kilichotokea Alhamisi iliyopita ni Matokeo ya jitihada za ukweli uliofanikiwa kulipa kisasi baada ya kupuuzwa kwa muda mrefu

Tano,WANACHADEMA,Wapendamabadiliko na watanzania kwa ujumla nawaahidi kuendeleza mapambano na wale wote wanaozuia harakati za mabadiliko ndani na nje ya chama chetu

Nitaendelea kusimamia misingi ya chama chetu na taifa bila kuchoka hadi tone langu la mwisho la damu.Namuomba mwenyezi Mungu anipe nguvu na ujasiri katika mapambano haya.Tuwapuuze wale wote wanaojaribu kututoa katika mstari wa mapambano.

Katika harakati hizi za mabadiliko na malengo ya CHADEMA kitaasisi katika kuongoza vuguvugu hili Doctrine yangu ni 'It's either you are with us or against us'.Hakuna middleground hata kama dunia ni three dimension.Kipimo nitakachompimia msaliti yeyote wa mabadiliko haya ndani ya chama hakitakua na tofauti na kile nitakachotumia dhidi ya wapinzani na maadui wa mabadiliko nje ya chama.

CC: Invisible, Fang, Buchanan, Paw, PainKiller Moderator
 
Dr Slaa amesema suala la zitto na CDM limefugwa sasa tuongelee suala la rasilimali zetu kama gesi, Umeme kupanda, hali mbaya ya maisha na wizi wa mali , wabakaji kama yle mbunge wa huko Tabora. kwahiyo tusubiri siku 14 tusikilizie maamuzi magumu ya CC

Limefungwa huko kwenye saccoss yenu huku mitandaoni na mitaani ndio habari ya mjini. Cc Matola. Hizo rasilimali kajadili na mkeo.
 
Last edited by a moderator:
kumpeleleza mtu wewe kama sio afisa ambaye kwa mujibu wa sheria una mamlaka hayo ni KOSA LA JINAI,so far huwezi ukawa una spy kwa manufaa ya katibu mkuu,wewe utakua huna tofauti na mchonganishi kwa sababu always utapeleka habari ambazo zinam favor boss wako wa saccoss
 
dr. Slaa hata ule mjadala wa ufisadi alioufanya kwenye halmashauri kule Karatu kwenye mradi wa maji alisema umefungwa.

Kufunga mijadala ndio njia pekee ya Slaa kukimbia uwajibikaji. Mtu kama huyu HAFAI kuwa Rais wa nchi, ndio maana Mungu aliwaongoza watanzania wasimchague...
 
1424452_10153520600210273_239004554_n.jpg

Unadhani ni kweli Katibu mkuu wa CCM anajua hii kazi au ndio TUNADANGANYWA ili tuone wana uwezo wa kuongoza????Funguka kistaarabu
 
kumpeleleza mtu wewe kama sio afisa ambaye kwa mujibu wa sheria una mamlaka hayo ni KOSA LA JINAI,so far huwezi ukawa una spy kwa manufaa ya katibu mkuu,wewe utakua huna tofauti na mchonganishi kwa sababu always utapeleka habari ambazo zinam favor boss wako wa saccoss

Ni kweli kabisa.

Hata kile kitendo cha Lema kumpora Mwigamba kompyuta yake ni uvunjifu wa sheria.

Chadema hawaheshimu sheria za nchi.
 
Limefungwa huko kwenye saccoss yenu huku mitandaoni na mitaani ndio habari ya mjini. Cc Matola. Hizo rasilimali kajadili na mkeo.

Huyo ni mlaghaika. Baada ya ID yake ya Jason Bourne kugundulika ameona aje na hii ya Asha Mohamed wa Doha!

Huyu ni mtu wa ajabu anayestahili kuonewa huruma...
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Miezi kadhaa iliyopita jumuiya ya vijana ya Chadema, Bavicha, ilitangaza kumvua uongozi na kumfukuza uanachama aliyekuwa makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bi. Juliana Shonza. Kosa lake lilitangazwa kuwa ni "usaliti".

Aliyefichua "usaliti" huo ni Ben Saanane a.k.a Mida Eight ambaye alielezwa kuwa alipewa kazi maalum ya kuspy vijana wenzake.

Katika katiba na kanuni za chama HAKUNA kazi hii ya uspy aliyopewa Ben Saanane.

Vijana wengi wa bavicha hasa hapa JF walimpongeza Ben Saanane na kumuona shujaa. Mpaka leo uspy huo alioufanya Ben Saanane ndio jambo pekee linalomfanya aonekane insider wa Chadema.

Mkakati wa siri wa kumpa Ben Saanane kazi ya kuspy ndani ya chama haukuhusisha vikao halali vya chama. Ndio maana viongozi wakuu wa Chama na wajumbe wa Kamati Kuu hawakuwa na taarifa yoyote juu ya kazi hii ya Ben Saanane. Hii ilikuwa ni kazi binafsi ya Dr. Slaa. Ben Saanane alikiri kwenye kikao halali cha Bavicha kuwa alifanya kazi ya uspy na kikao hicho kikampongeza kwa kazi nzuri!

Ni UNAFIKI wa hali ya juu kuona vijana waliounga mkono uwepo wa mikakati ya siri ya Dr. Slaa kumtumia Ben Saanane wakipinga mwanazuoni Dr. Kitila Mkumbo kuwa na mikakati ya siri.

Je, kuna mtu mwenye hati miliki ya mikakati ya siri ndani ya Chadema?

Jumuiya ya vijana katika chama chochote ndio nguzo na dira ya chama. Unafiki huu unaotawala Bavicha unadhihirisha kuwa Chadema sasa haina dira na nguyo yake imeliwa na mchwa.
Mijitu mingine bana,
We ulitaka huyu Spy awekwe hadharani pamoja na kazi zake atakazofanya ziainishwe na viongozi wote wa chama, hapo kuna u-spy tena??
Spy anatakiwa awe wa siri siri hivyohivyo ili wanaochunguzwa wasijue, maana wanaweza wakaharibu upelelezi. Yaani mfano Dr.W.Slaa amwambie Zitto kua namuagiza Ben Saanane akuchunguze kama hua unawasilianaga na Jack Zoka?? Chekecha akili Mkuu
 
Last edited by a moderator:
Chadema kimejimaliza na kinaonesha ni jinsi gani viongozi wake wakuu na washauri wao wamepungukiwa na busara Nilikitegemea sana chama hiki kuleta mabadiliko ya kweli lakini kwa mwendo huu imani hiyo imepungua sana. Mie sijui tusubiri tuone watakavyojitoa katika mporomoko huu
 
Mijitu mingine bana,
We ulitaka huyu Spy awekwe hadharani pamoja na kazi zake atakazofanya ziainishwe na viongozi wote wa chama, hapo kuna u-spy tena??
Spy anatakiwa awe wa siri siri hivyohivyo ili wanaochunguzwa wasijue, maana wanaweza wakaharibu upelelezi. Yaani mfano Dr.W.Slaa amwambie Zitto kua namuagiza Ben Saanane akuchunguze kama hua unawasilianaga na Jack Zoka?? Chekecha akili Mkuu

Je, ulitaka Kitila aweke hadharani mkakati wa kumshinda Mbowe kwenye uchaguzi ujao? Huo ungekuwa mkakati?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom