Unafahamu kuwa nchi ya Urusi imepitisha siku maalumu ya kupeana mimba?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Katika hotuba yake ya Hali ya Taifa hilo ya mwaka 2006, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitaja janga la idadi ya watu kuwa ni tatizo la dharura zaidi linaloikabili Urusi na akatangaza jitihada za kuongeza kiwango cha idadi ya watu na kuongeza uzazi kwa Urusi, ikiwa ni pamoja na kutoa motisha ya pesa taslimu kwa familia ambazo zina zaidi ya mtoto mmoja, ili zihamasike kuongeza watoto.

Septemba 12 kila mwaka ni siku muhimu sana Urusi hasa eneo la Ulyanovsk, ambapo wanaipa heshima kama 'siku ya kupeana mimba kwa raia wa Urusi. Utamaduni huu kawaida unazungumzia wenza kukupata muda maalumu wa faragha ya ndoa na uzazi kwa njia ya kipekee. Hivyo Serika ikaanzisha siku ya mapumziko kwa umma maalumu kwa ajili ya kuwapa wanandoa muda wa faragha kwa matumaini kwamba watashika mimba. Wazazi ambao watoto wao huzaliwa miezi tisa baadaye wanaweza hata kushinda zawadi kwa kusaidia kuwa mstari wa damu kuendelea damu ya Urusi. Watoto wanaozaliwa Septemba 12 hupata zawadi kutoka kwa Mamlaka.

Mnamo mwaka wa 2005, Gavana Sergey Ivanovich Morozov wa Ulyanovsk, eneo lililoko kilomita 800 Mashariki mwa Moscow, aliongeza kipengele cha kufurahisha kwa kampeni ya kitaifa kwa kutangaza Septemba 12 kama Siku ya Kupeana mimba na kuwapa wanandoa likizo ya kazi ili kupata fursa ya faragha kwa ajili ya kutengeneza kizazi kijacho.

Tuzo kuu ya 2007 lilikwenda kwa Irina na Andrei Kartuzov, ambao walipokea UAZ-Patriot, gari la kifahari huko Ulyanovsk. Washiriki wengine walizawadiwa kamera za video, TV, friji na mashine za kufulia. Urusi imeamua kutenga siku hiyo na zawadi zingine kama hamasa kutokana na viwango vya uzazi nchini humo kupungua pamoja uwiano usio sawa kati ya wanaume na wanawake na maisha mafupi ya wanaume wa Urusi yanaleta wasiwasi mkubwa kwa jamii.

images (9).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom