Mkuu hutaki hata mtu wa kukubebea briefcase? Mabegi? Mtaani kwamoto.Tumeuanza mwaka mwingine tena ajira zimezidi kuwa tatizo
Rai yangu Linda kibarua chako kwa wewe uliyebarikiwa kukipata lakini pia usichoke kuwaombea na wale wanaohangaikia kazi
Vipi wa kukuandalia kahawa hutaki mkuu? Sizonje kabana kinoma.[emoji15] [emoji144] uje pm tafadhali ila mabegi tabeba mwenyewe
Mimi nahitaji wa kuvuna pambaVipi wa kukuandalia kahawa hutaki mkuu? Sizonje kabana kinoma.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Maelewano tu.Mimi nahitaji wa kuvuna pamba
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini
Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi
View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA
Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.
Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao
Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684
tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani
Duu pole sanasana[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]Nashukuru mkuu mshana Jr kwa kuliona hili,hii hali ndio napambana nayo sasa,jamani maumivu yake hayavumiliki,,,,,,,,ila pia mlioko maofisini Tafadhali msijisahau mkaanza kutudharau tunapozunguka maifisini kutafuta kazi kiukweli kauli zenu kavu sana na kwangua misuli ya moyo na kuumiza
Ni Mara nyingi hii kitu nakutana nayo walioajiriwa wanajisahau sana hatuombeani mabaya ila maisha yanabadilika sana,juz nilfanikiwa kupata chance kwenye kampuni fulan baada ya kuhangaika sana japo ni nafasi sales ila si mbaya wakaniambia niwapelekee cheti nikishndwa sana basi nipeleke transcript,nikaenda chuoni nikaambiwa HELSB hawahaletea ada zetu kwa maana hyo siwez kupewa hayo majibu yalitolewa na Dada aliyekuwa akizunguka kwenye kiti akionekana hana shida wala hajawahi kuhisi shida "hatuwezi kukupa transcript kwan hatujalipwa ada yetu" nilipo mdogelea ili nimuelezee how important was it alinaambia "usinisogelee nmeeleweka sihitaji maelezo,hata kama inatakiwa kazin hyo ni non of my business" nilijisikia vbaya sana akili ilinijia tugawane majumba ya serikali yeye aende ICU nami nikafie jela,ila MUNGU akaepusha