Unadhani hawajisikii vibaya?

Unadhani hawajisikii vibaya?

Natumaini mtukufu Raisi anapita humu jukwaani atauona huu Ujumbe na kuufanyia kazi ...

Hata kama sio yy natumaini baadhi ya Viongozi wanapita sana humu kama wakiuona huu Ujumbe wasisite kumfikishia taarifa ...
Mtaani hali mbaya watu tunakula mpakani mwa mchana na usiku..
Atajali kweli?
 
Nimekutana na story ya kuumiza hisia ya binti mmoja kuhusiana na ahadi ya kazi inasikitisha mno! Nitaisimulia muda mwafaka ukifika
 
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini

Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi

View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA

Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.

Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao

Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684

tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani
Nilikumbana na hiyo hali kama miezi 6 baada ya kumaliza chuo..miezi 6 ilikuwa kama miaka!!
Hata ndugu ambaye nilikuwa nakaa kwake alionesha kunichoka, zile nauli za kwenda mjini nikawa sipewi tena..msosi wenyewe nyumbani nikawa naupata kwa manati!!
Kuna wakati nilifikiria kuwa dalali, yani nikiona watu mtaani wameandika nyumba zao zinauzwa..mi nachukua namba nakuja kuzipost JF..Napo sikuambulia kitu, kuna wakati nikahitaji laki mbili japo nianzishe banda la chipsi sikuipata...

Asikuambie mtu, ni kipindi kigumu sana hicho unaweza kuanza kujenga chuki na watu pasi na sababu!!
 
Naamini umepita salama hicho kipindi na sasa zimebaki story za kukumbuka, maisha hayana formula
 
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini

Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi

View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA

Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.

Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao

Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684

tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani
Serikali haiwezi kutoa ajira kwa kila mmoja.
 
Dah umeandika kwa hisia sana.. Ungesindikiza na ule wimbo ameimba darasa na lina.. jina siujui ila ktk korasi Lina anaimba kila kunapokucha afadhali ya jana.... Au ule wa Bellah na Banana.
Huo wimbo unaitwa mateso...kaimba Countryboy sio darasa...
Ila darasa ana wimbo wake unaitwa Sikati tamaa, nao ni mzuri unafariji sana!!
 
Nipo Kituo cha daladala hapa kuna tangazo la ajira na mshahara laki tatu sabini elfu kwa mwezi. Labda hii nayo inaweza kuwa fursa kwa we nye uhitaji wasting wakisubiria ajira ya ndoto yao!
Hao matapeli mkuu!!
 
nimecheza anga zote mbili..jaribu kuanzisha biashara yako leo hii ili ujikwamue kimaisha baada ya kukosa ajira uone mziki wake
Kupata tu nyaraka za kukutambua kama mjasiriamali unaweza kukata tamaa na kurudi kijiweni ukavute bangi
Michakato migumu kuanzia kupata mtaji mpaka kusimamisha biashara imewashinda wengi
Kweli mkuu ili nalo nishida kujiajiri michakato nimigumu sana ukitaka kuanzisha kitu unapitia mamlaka si chini ya tatu nazo vikwazo vingi mpaka unakata tamaa
 
Nashukuru kaka umeongea kuhusu hili. Lakini ngoja waje apa ambao wameajiriwa na maneno yao ya kejeli, kua eti wajiajiri hao wasio na kazi...iv mkuu nikuulize kwa hali ya huyo kijana uliemtolea mfano anajiajri vipi???
Wanasema kajiarili wakati wenyewe wameajiriwa
 
Mshana (doto)
Umetoa Maelezo ambayo yanaumiza sana fikra za watu sana hasa kwa watanzania. Gavana wa benki yetu ametoa report za kukua kwa uchumi kama ulivyoeleza.

Mie nina mtizamo tofauti wakifikra na wewe. Kwa maelezo yako inaonesha kwamba unategemea serekali ndio ilete maisha bora kwa watanzani, Viongozi wetu hawana utashi wa kweli kuwahudumia wananchi nia yao ni kwa ajili ya matumbo yao na familia zao, fikiria kidogo tu wewe unalipa payee kiongozi halipi,

Unakatwa Mafao leo wanaleta sheria ya kwamba mafao yako yakajenge viwanda hela utaipata ukifikisha miaka 65, wao hio sheri kwao haitumiki 5 years wakimaliza hela wanachukua bila makato. hivyo basi mfumo wa maisha kwa dunia nzima ni waudanganyifu na kukatisha tamaa sana.

Cha Msingi ni kubadili mtizamo tu, kufanya kazi kwa bidii na kwa malengo kwa wale walioajiriwa watambue hiyo kazi ni daraja la kumpleleka kwenye kazi za kujiajiri. kwa wale majasiriamali ni kujitahidi kwa bidii kufanya kazi sana ili uwe na maisha bora bila kuilalamikia serekali yetu sikivu..
We umeajiriwa ehee ???
 
Back
Top Bottom