Unadhani hawajisikii vibaya?

Nashukuru mkuu mshana Jr kwa kuliona hili,hii hali ndio napambana nayo sasa,jamani maumivu yake hayavumiliki,,,,,,,,ila pia mlioko maofisini Tafadhali msijisahau mkaanza kutudharau tunapozunguka maifisini kutafuta kazi kiukweli kauli zenu kavu sana na kwangua misuli ya moyo na kuumiza
Ni Mara nyingi hii kitu nakutana nayo walioajiriwa wanajisahau sana hatuombeani mabaya ila maisha yanabadilika sana,juz nilfanikiwa kupata chance kwenye kampuni fulan baada ya kuhangaika sana japo ni nafasi sales ila si mbaya wakaniambia niwapelekee cheti nikishndwa sana basi nipeleke transcript,nikaenda chuoni nikaambiwa HELSB hawahaletea ada zetu kwa maana hyo siwez kupewa hayo majibu yalitolewa na Dada aliyekuwa akizunguka kwenye kiti akionekana hana shida wala hajawahi kuhisi shida "hatuwezi kukupa transcript kwan hatujalipwa ada yetu" nilipo mdogelea ili nimuelezee how important was it alinaambia "usinisogelee nmeeleweka sihitaji maelezo,hata kama inatakiwa kazin hyo ni non of my business" nilijisikia vbaya sana akili ilinijia tugawane majumba ya serikali yeye aende ICU nami nikafie jela,ila MUNGU akaepusha

Oohhh jaman pole mkuu lkn Mungu bado. I mwaminifu sana ipo siku yako yote uliokutana nayo na kupitia vitabak kuwa story Mungu ni mwaminifu sana
 
00140055-9b452b6b54855733808a28c20ff4f619-arc614x376-w614-us1.jpg

Post sent using JamiiForums mobile app
 
View attachment 411685
Ni asubuhi ya siku nyingine tena, harakati zimeshaanza na nyingi Zikiwa ni kuwahi kazini au mishemishe pamoja na uchovu wa jana lakini huna budi kuamka na kujiandaa ili uwahi kazini

Ni katika kipindi hiki kwenye hizi harakati za kuwahi kibaruani kuna mtu yuko kitandani muda huu si kwa kupenda la hasha! Anaumia hana kazi naye angetamani muda huu awe anapasi nguo za kazini au yuko barabarani kuwahi

View attachment 411686
Anaumia sana akikumbuka alivyosoma kwa tabu na sasa ni mwaka wa tatu huu hana ajira huku washkaji zake wakipeta(mawazo mabaya huanzia hapa)kwanini na si mimi?kwanini wao wapate na mimi nikose? Kwani tunatofautiana nini? INAUMIZA SANA

Huwezi kuendelea kulala siku nzima utaumwa unaamua kutoka uende kijiweni au ukajaribu bahati yako popote lakini du mfukoni huna hata mia!inauma sana.

Siku yako inapita hivyo hivyo kimungu Mungu na jioni inapokaribia unaanza kuwaona watu wakirudi toka makazini, kwenye magari yao na wengine kwenye usafiri wa jumuiya wengine wamechoka wengine wanapiga story inaumiza mno unatamani na wewe ungekuwa mmoja wao

Unavuta picha jinsi ulivyochomekea na tai yako jinsi ulivyohudumia wateja wako kazini changamoto ulizokutana nazo..unajikuta kabisa ukitumika na kuhudumia kwa furaha unapotelea kabisa mawazoni mpaka unatabasamu, na ghafla unashtuka kumbe uko kijiweni honi ya mshikaji uliyesoma naye inakushtua yuko kwenye altezza anatoka job INAUMIZA SANA
View attachment 411684

tatizo la ajira ni la dunia nzima lakini hii isiwe kisingizio cha serikali...kila mwaka vijana wetu wanamaliza elimu zao wakitegemea kupata ajira...na idadi inaongezeka kila mwaka.. ! Hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi hali ni mbaya sana mitaani
Serikali yetu haina maono na sekta binafsi na wala haijali iliyowaajiri. Inawaza kubuni kodi kila siku bila kuwapa wigo sekta binafsi wa kutanua miradi yao ili na ajira za kudumu ama za muda ziongezeke.

Serikali yetu imewaweka wasiokuwa na ajira kama misukule yao wakati wa kusaka kura. Kujuana kumekuwa kwingi mno. Kama wewe hujulikani na ulikuwa unachezea GPA ya 3 basi umekwisha Tanzania hii.

Kujuana pia kumekuwa kwingi mno. Leo hii Mkuu wa Jeshi la Polisi MSTAAFU anakuwa Balozi badala ya kupumzika na kuachia ajira mpya moja, leo hii Mke wa Rais Mstaafu badala ya kupumzika na mumewe wauishi uzee wao vizuri ndiyo kwanza anapewa shavu la Ubunge wa Kuteuliwa na kuziba nafasi ya kijana mwenye fikra mpya. Mifano kama hii ni mingi mno, kutishiana ni kwingi hata Bank zinazotakiwa ziwakomboe watu zinaogopa kukopesha; Je! Hapa utatengenezaje ajira kama tafsiri ya Kujenga kiwanda ni vyerehani vinne?
 
Kaka hili suala ni zaidi ya atomic bomb.. Ni suala la muda tu,kama hakutakua na jitihada za makusudi kutatua hili tatizo basi habari yake tutaipata soon..
 
serikali ifunge vyuo kwa muda hahahahahaha vimekuwa sehemu ya kuzalisha watu wenye msongo wa mawazo
Kama ikiwezekana tusitishe uamuzi wa kununua ndege zaidi na hizo pesa zitumike kwenye nyanja ambazo zitatoa ajira kwa wingi hasa kilimo na usindikaji
 
Kama ikiwezekana tusitishe uamuzi wa kununua ndege zaidi na hizo pesa zitumike kwenye nyanja ambazo zitatoa ajira kwa wingi hasa kilimo na usindikaji
mkuu anaangalia maendeleo ya vitu na si watu, ushauri wa kuacha kununua ndege hawezi ukubali maana kwake maendeleo ni vitu na si watu.

ijapokuwa hazijawahi tengeneza faida ila kwake ni bora.
 
mkuu anaangalia maendeleo ya vitu na si watu, ushauri wa kuacha kununua ndege hawezi ukubali maana kwake maendeleo ni vitu na si watu.

ijapokuwa hazijawahi tengeneza faida ila kwake ni bora.
Hapana ushahidi wa faida huu hapa
downloadfile-1.jpg
 
Back
Top Bottom