Sasa mwanamke gani mwenye akili anafurahia mume kufa na kumuachia mali katika hali ya ubibi? Atazifaidi vipi sasa ilhali kashakongoroka na uzee umepiga hodi? Kama ni kuwaua waume zao si bora wawaue ili wabaki wakitumia mali wakiwa mabinti?
Nani aliyekuambia KUWA Mwanamke amainjoi Mali na mumewe?
[emoji1787][emoji1787]
Mwanamke anainjoi MAISHA AKIWA na watu wanaompigia magoti na kumtii kama Zumaridi.
Mwanamke Akiwa MTU mzima ni mkorofi ZAIDI na anaona Kila MTU ni mtoto kwake . Hivyo Hata mumewe akitaka waelewane basi ajifanye Kama mtototo na akubali kufokewa Hata mbele ya vyombo Vya habari. Mwanaume akubaliane na masharti Yote anayotoa MKE ambaye anakua ni mama Wa Kila mtu. SASA AKIWA NA PESA Mwanamke mwenye uumri mkubwa anajiamini Kama Zumaridi,mume watoto na wake zao WOTE wanatakiwa wamsikilize na Wakiwa na shida wamwambie yeye Ndio atoe maamuzi . Na bahati nzuri wanwake hawapotezi kumbukumbu mapema.
Mwanamke kuinjoi MAISHA ni kujiona Yuko Juu ya vyote Sio KUWA tu na mume Tena Mzee . Unajua binadamu walivyo Kila mmoja akimwana mwenzake anaona amezeeka na kuchoka kuliko yeye, hivyo Mwanamke akimwangalia mumewe ameshavuka Miaka 60 anamuona kazeeka sana na amechoka hivyo anaona Hana uwezo Wa kutoa maamuzi sawasawa.
Hiví unajua mara nyingi wanawake Hata kwenye siasa hawapendi waume zao watoke madarakani!!
Hiví yule bwana Mkubwa Msataafu Wa kule nchini Tazamieni mkewe Ndio MTU Wa KUWA mbunge Tena Wa Mkoa na wilaya nyingine . Muda WOTE yupo Bungeni na jimboni wakati mumewe ni Rais Msataafu na ni bilionea na anasafiri Kwenda mpaka vikao vya UN. Tatizo nini mama anatafuta Heshima na KUWA na watu wanaompigia magoti.
Kumbuka Shetani hakuwa Mjinga kumdanganya binadamu kupitia Mwanamke . Alijua asingeweza kumdanganya Adam Kwa Mali mana Mali zote zilikuwa za kwake.
Shetani alijua wazi KUWA ya baada ya Eva kuwa na Kila kitu Bado alikua hajaridhika na kuinjoi ndani ya Bustani ya Edeni ambapo palikua na Kila kitu kizuri na cha kupendeza ,alimwingia Eva Kwa kumwambia KUWA atakapokula lile tunda atakua kama MUNGU . Eva akaingiwa na tamaa ya KUWA kama MUNGU Ili watu WOTE wampigie magoti yeye Sawa na Mungu . Angebahatika KUWA kama Mungu asingempa lile Tunda Adamu Bali angemlazimisha amwabutu na kusikiliza Amri zake kama MUNGU.
Kuna MKE Wa MTU lakini Kuna Harakati za Wanawake ambazo zilianzia Tangu Edeni na lengo na tamaa Yao ni KUWA Juu. Kinachowafanya wawe chini mara nyingi ni uchumi .Hizi harakati ni muunganiko Wa MKE Wa MTU Mmoja Mmoja PAMOJA na wanawake wasio wanaume.