Tutaongea mengi lakini kinachosumbusa ni hali ya kutokujiamini kwa wanawake wengi "insecurities"
Unajua mwanaume ukishakuwa na pesa mafanikio inakuwa ni vyepesi sana kuvutia wanawake wengi wa nje, kiasi kwamba mke wako wa ndoa anakuwa na wasiwasi na nafasi yake kwakua walioko nje ni wengi kuliko yeye mmoja.
Inafikia hatua hata ukimkosea anahisi ni makusudi kwakua una kiburi cha pesa kumbe pengine ni ubinadamu wa kawaida kukosea, kukuonya anashindwa kwakuhofia kuwa utamuacha na unaweza pata mwingine kirahisi tu, kwahiyo anakaa na vinyongo moyoni na kuugulia.
Hapo sasa njia pekee ya kujihakikishia future ni kukuua tu ili amiliki pesa, maana kukuacha anajua haitakuwa pigo kwako badala yake atajitesa mweyewe.
NB: SULUHISHO ni kupata mwanamke anaejiamini juu yako asiyekuwa na wasiwasi wa kuachwa kila muda kwenye akili yake, au kama una utajiri kabla haujaoa hakikisha hauoi mwanamke mwenye hali ya chini sana kiuchumi (anaeona kuoelewa na mwenye pesa ni bahati)
Tajiri oa tajiri au mwenye kipato cha kati.
Nyinyi mkiona matajiri wanakataza watoto wao kuengage na malofa mnadhani ni wabaguzi, kumbe dunia ndivyo jinsi inatakiwa kuwa ili mambo yakae sawa na wao walishaliona hilo kitambo.
Cc
Carleen