Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 53,270
- 72,464
Kila mtu ana kitu kile ambacho mwenzake hana na kila mmoja anatumia kipawa chake kwa usahihi kabisa kuliko mwenzake.
Kipawa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile ambacho kinaweza kuwa kigumu kwa baadhi ya watu/mtu (Kipaji)
Naamini kila mmoja anajua kipawa chake hadi sasa kama huna kipawa basi pole sana na Mungu akuoneshe kipawa chako na jinsi ya kukitumia.
Kwangu mimi nina kipawa cha USHAWISHI nasema hili kwa uhakika sana ninaweza kushawishi pande mbili kuwa sawa au pale ambapo hakuna amani kukawa na amani, naweza kubadilisha mtu mawazo yake na akaenda vile navyotaka kwa muda mfupi sana.
Kwangu mimi Najivunia sana kuwa na kipawa hiki wote ambao wamekuwa na mimi wamejikuta wanapita njia yangu, marafiki, wapenzi, ndugu na jamaa.
Kwako wewe una kipi unachoweza kushukuru Mungu kuwa amekupa kitu cha kipekee kuliko yeyote?
Karibu.
Thibitisha mkuu hapo nilipo bold