zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,065
- 28,707
Toka mwanzo nilipinga CHADEMA kurudi kwenye hizi chaguzi maana kila siku CCM inakuja na mbinu mpya za kuhujumu chaguzi ila nachoshangaa kwanini toka 2015 wapinzani hawapambani kupata katiba mpya?? Ilitakiwa wakati uchaguzi umeisha tu kaingia magufuli wangeanza pressure kudai katiba mpya ili izae mfumo bora wa uchaguzi ila huu mfumo wa sasa unaifavor CCM kushinda chaguzi hizi ndogo
Kitakachotokea ni CCM kutangazwa mshindi majimbo yote 2 hata kma atakayepata kura nyingi atatokea upinzani.... Na hili upinzani wanalifahamu hivyo inabidi baada ya hapa waitafute katiba mpya au angalau mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi yabadilishwe kupitia bungeni ili waweze kufikia malengo otherwise wakianguka uchaguzi huu matokeo ni haya yafuatayo;
1. Morali kwa wafuasi wa upinzani utashuka maana itaonekana kila vita wanayopambana haiwezi kufanikiwa awamu hii hivyo itasababisha wanachama wengi kukata tamaa na kuacha kuisupport hivyo kupungua kwa uungwaji mkono kuelekea 2020.
2.Viongozi wa CHADEMA hata bila kununuliwa watahamia CCM sababu ndio wataona sehemu pekee ambako ushindi unapatikana sababu kama kila uchaguzi upinzani wanazidiwa ujanja na CCM wa rafu za kihuni wataona hakuna namna ya kushinda jimbo kma haupo CCM 2020 hivyo wataondoka wengi sana
3. Wabunge madiwani mameya n.k wa upinzani wengi watahamia CCM kwa kujiuzulu bila uwoga tena sababu watajua hata wakijiuzulu na kuhamia CCM watarudi tu bungeni kwa namna yoyote ile hivyo tabia ya kuhamahama itaongezeka mara 100 maana kuna wengi wanataka kuhama ila wanaogopa kupoteza nafasi zao za uwakilishi hivyo matokeo ya uchaguzi huu yataongeza au kumaliza tabia hii.
4. 2020 ndio upinzani utazikwa rasmi hapa Tanzania sababu CCM ikiona inafanya uhuni wote huu na wanashinda chaguzi itawapa picha kwamba hata 2020 wanaweza kuiba na wasifanywe lolote ila ikitokea upinzani umeshinda basi CCM itajenga hofu kwamba hawawezi kuwapangia wananchi kiongozi na hivyo kuweka heshima kwa upinzani na kuepusha dhahma hizi na rafu kufanyika 2020.
5. Wapiga kura watakuwa wachache kabisa 2020 maana wataona hata wakimchagua mpinzani hatangazwi.
NINI KIFANYIKE
1. Kwa kuwa mnajua miaka yote tume sio huru na mmeamua kushiriki basi hatutegemei rafu zikifanyika muishie kulalamika (of course CCM wanategemea hivyo!!). Ila mjiandae kupambana yaani mvumilie virungu mapanga na mabomu ya machozi mpaka muhakikishe kura haibiwi yaani nachosema tuione nguvu ya umma sio diplomasia tena..... Hata kenya chama tawala wanamheshimu odinga sababu wanajua wakimuonea huwa nguvu ya umma inatumika hivyo na sisi tuione keshokutwa!! kma wataita vurugu na machafuko haya ila ikitokea uonevu mpambane nao kisawasawa ili huu uhuni uishe sio mnaona wakala anatolewa nje mnaitisha press conference.... Mnaenda vituoni in numbers kama hawataki kumuingiza basi liwalo na liwe uchaguzi usifanyike kma hilo hamuwezi basi msishiriki maana mkianguka kwa rafu za CCM mnavunja moyo wafuasi wenu
Hitimisho langu ni kwamba uchaguzi huu unabeba taswira pana Sana kuelekea 2020 hivyo upinzani muupe uchaguzi huu uzito mkubwa maana ndio utatoa picha halisi ya uchaguzi 2020 hivyo mkipambana na kutoka na ushindi mtamaliza hamahama na hata 2020 wataogopa kutumia mbini hizi ovu
Uchaguzi mwema wanamabadiliko,