Umuhimu wa uchaguzi mdogo na hatma ya upinzani kuelekea 2020 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa uchaguzi mdogo na hatma ya upinzani kuelekea 2020

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by zitto junior, Feb 15, 2018.

 1. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Kwanza ningeomba mods msiunganishe uzi huu na nyuzi nyingine za kuhusu uchaguzi wa kinondoni sababu nataka wanamabadiliko wote wausome

  Toka mwanzo nilipinga CHADEMA kurudi kwenye hizi chaguzi maana kila siku CCM inakuja na mbinu mpya za kuhujumu chaguzi ila nachoshangaa kwanini toka 2015 wapinzani hawapambani kupata katiba mpya?? Ilitakiwa wakati uchaguzi umeisha tu kaingia magufuli wangeanza pressure kudai katiba mpya ili izae mfumo bora wa uchaguzi ila huu mfumo wa sasa unaifavor CCM kushinda chaguzi hizi ndogo

  Kitakachotokea ni CCM kutangazwa mshindi majimbo yote 2 hata kma atakayepata kura nyingi atatokea upinzani.... Na hili upinzani wanalifahamu hivyo inabidi baada ya hapa waitafute katiba mpya au angalau mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi yabadilishwe kupitia bungeni ili waweze kufikia malengo otherwise wakianguka uchaguzi huu matokeo ni haya yafuatayo;

  1. Morali kwa wafuasi wa upinzani utashuka maana itaonekana kila vita wanayopambana haiwezi kufanikiwa awamu hii hivyo itasababisha wanachama wengi kukata tamaa na kuacha kuisupport hivyo kupungua kwa uungwaji mkono kuelekea 2020.

  2.Viongozi wa CHADEMA hata bila kununuliwa watahamia CCM sababu ndio wataona sehemu pekee ambako ushindi unapatikana sababu kama kila uchaguzi upinzani wanazidiwa ujanja na CCM wa rafu za kihuni wataona hakuna namna ya kushinda jimbo kma haupo CCM 2020 hivyo wataondoka wengi sana

  3. Wabunge madiwani mameya n.k wa upinzani wengi watahamia CCM kwa kujiuzulu bila uwoga tena sababu watajua hata wakijiuzulu na kuhamia CCM watarudi tu bungeni kwa namna yoyote ile hivyo tabia ya kuhamahama itaongezeka mara 100 maana kuna wengi wanataka kuhama ila wanaogopa kupoteza nafasi zao za uwakilishi hivyo matokeo ya uchaguzi huu yataongeza au kumaliza tabia hii.

  4. 2020 ndio upinzani utazikwa rasmi hapa Tanzania sababu CCM ikiona inafanya uhuni wote huu na wanashinda chaguzi itawapa picha kwamba hata 2020 wanaweza kuiba na wasifanywe lolote ila ikitokea upinzani umeshinda basi CCM itajenga hofu kwamba hawawezi kuwapangia wananchi kiongozi na hivyo kuweka heshima kwa upinzani na kuepusha dhahma hizi na rafu kufanyika 2020.

  5. Wapiga kura watakuwa wachache kabisa 2020 maana wataona hata wakimchagua mpinzani hatangazwi.

  NINI KIFANYIKE
  1. Kwa kuwa mnajua miaka yote tume sio huru na mmeamua kushiriki basi hatutegemei rafu zikifanyika muishie kulalamika (of course CCM wanategemea hivyo!!). Ila mjiandae kupambana yaani mvumilie virungu mapanga na mabomu ya machozi mpaka muhakikishe kura haibiwi yaani nachosema tuione nguvu ya umma sio diplomasia tena..... Hata kenya chama tawala wanamheshimu odinga sababu wanajua wakimuonea huwa nguvu ya umma inatumika hivyo na sisi tuione keshokutwa!! kma wataita vurugu na machafuko haya ila ikitokea uonevu mpambane nao kisawasawa ili huu uhuni uishe sio mnaona wakala anatolewa nje mnaitisha press conference.... Mnaenda vituoni in numbers kama hawataki kumuingiza basi liwalo na liwe uchaguzi usifanyike kma hilo hamuwezi basi msishiriki maana mkianguka kwa rafu za CCM mnavunja moyo wafuasi wenu

  Hitimisho langu ni kwamba uchaguzi huu unabeba taswira pana Sana kuelekea 2020 hivyo upinzani muupe uchaguzi huu uzito mkubwa maana ndio utatoa picha halisi ya uchaguzi 2020 hivyo mkipambana na kutoka na ushindi mtamaliza hamahama na hata 2020 wataogopa kutumia mbini hizi ovu

  Uchaguzi mwema wanamabadiliko,
   
 2. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2018
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 47,540
  Likes Received: 30,166
  Trophy Points: 280
  Umeandika kisomi sana .
   
 3. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Mkuu Erythrocyte huu uchaguzi umebeba hatma ya upinzani.... Kwa mliopo dar hakikisheni njama ovu zote hazifanikiwi kwa hali na mali lasihivyo itakuwa REJEA mbaya kwa chaguzi zijazo hasa 2020
   
 4. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2018
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 9,764
  Likes Received: 14,179
  Trophy Points: 280
  Mimi nilidhani utasema, TUPAMBANE kumbe ni wale wale keyboard/keypad warriors wanaosema, MPAMBANE wakati yeye yuko chumbani kwake akiangalia TV.

  Karibu kwenye uwanja wa mapambano kama unataka kusimamia hoja yako na sio kuwafanya wengine mbuzi wa kafara!
   
 5. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2018
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 10,337
  Likes Received: 8,359
  Trophy Points: 280
  Kihistoria Kinondoni ni jimbo la CCM, hata huyu Mtulia 2015 alichaguliwa na wanaccm waliochukizwa na kitendo cha CCM kumrejesha muuza ngada ulingoni. Kwahiyo kuupima upinzani kwa majimbo ya CCM Siha na Kinondoni ni kujidanganya!
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,998
  Likes Received: 5,830
  Trophy Points: 280
  Mkuu zitto junior nimekusoma vizuri, hapa CCM walipotufikisha siyo tena kulalamika kwani kila uhuni wanaofanya wameandaa majibu ya malalamiko ya Chadema. Ni wakati wa kupambana na hawa makaburu weusi,hakuna jinsi nyingine kwani wao wanategemea bunduki na mabomu ya polisi lakini hayo siyo mengi kuliko idadi yetu tukiamua watanyoosha mkono tu.
   
 7. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,537
  Likes Received: 4,859
  Trophy Points: 280
  Pia Kinondoni ndio jimbo tajiri kuliko majimbo mengine hivyo CCM ina mkakati wa kulifanya jimbo hilo liwe ndio chanzo kikuu cha mapato mkoani Dar-es-salaam.

  Ili kuliendeleza jiji la Dar inabidi kudhibiti vyanzo vya mapato vya uhakika ambavyo tayari CCM na Serikali yake wanavifahamu kwa asilimia 100.

  Kinondoni ni jimbo la kimkakati hivyo mwaka huu na baada ya 2020 jimbo hili haliwezi kwenda upinzani na Mtulia tayari anayo "dossier" ya "mkakati Kinondoni".
   
 8. N

  Ndugu wa Trump JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2018
  Joined: Nov 9, 2016
  Messages: 696
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 180
  Masikini bavicha !
   
 9. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Mkuu hoja yangu sio kushinda ama kushindwa kwa upinzani kwenye sanduku la kura ila nachoongelea ni kushindwa kwa sababu ya rafu za uchaguzi alafu wanaishia kulalamika

  Wakishindwa kihalali hamna shida ila sio mambo ya kutolewa mawakala na rafu zingine hyo ndio hoja yangu
   
 10. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Siko Dar mkuu kwa nafasi yangu nmechangia sana kwenye siasa za kupambana kukikuza chama hasa nikiwa chuoni nlijitoa sana.... Ndio maana nmesema KWA WALIOPO DAR kina Erythrocyte na salary slip wahakikishe kura haibiwi wala rafu za NEC hazifanikiwi
   
 11. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Hii mada ni kwa wapenda mabadiliko ila kama unaona demokrasia haina faida yeyote basi una haki ya kutukejeli
   
 12. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Mkuu Richard heshima kwako na ahsante kwa kuchangia..... Ingawa napingana na mtazamo wako ila naheshimu mawazo yako na labda nikuulize

  unaposema jimbo la kinondoni lipo kimkakati ili kukuza uchumi ina maana mbunge akitokea upinzani anawezaje kuathiri mipango hiyo??

  2. Je kwanini unaamini CCM wanajua sana mapato ya hiyo wilaya ndio maana wataweza kuliendeleza sasa swali linakuja kwanni miaka 50 walijua hivyo vyanzo hawakuweza kulitumia kimkakati ila unaamini miaka 50 baadae yaani 2017 ndio wataweza kulitumia kimkakati ili kuijenga dar?? Kwani hamuwezi lidhibiti kwa kutimia halmashauri ya kinondoni ambayo ipo chini ya CCM

  Ni hayo tu
   
 13. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2018
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,537
  Likes Received: 4,859
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu.

  Ni kwamba kwanza, jimbo likiwa ni la CCM litakwenda na sera na ilani ya uchaguzi ya CCM.

  Pili, ingawa Kinondoni ni jimbo tajiri lakini mapato yake yamekuwa si yale yanayokuwa yanatarajiwa kwamba fedha za mapato kutoka channels zote, kuanzia vituo vya kujazia mafuta, kodi za wafanyabiashara, mahoteli, majumba ya starehe, na vyanzo vingine vya kuaminika havikuwa vikidhibitiwa ipasavyo.

  Hivyo chini ya uongozi wa Mwenyekiti raisi John Magufuli wilaya ya Kinondoni itakuwa ikifuata kitu chaitwa kwa kiingereza time-frame kwamba fedha zinatumika zinakotakiwa, miradi inakwenda sambaba na thamani ya fedha zitolewazo au "money for value" na Mbunge wa jimbo hilo ni yule wa CCM.

  Pia mapato halisi yatatakiwa yawe wanajulikana kwani kumekuwa na sintofahamu kubwa baina ya wabunge na madiwani kutoka vyama tofauti hivyo kufifisha malengo la kauli mbiu moja ya kuleta maendeleo.

  Huo ndio utafiti wangu wa kizungumkuti cha jimbo la Kinondoni.
   
 14. m

  msege Senior Member

  #14
  Feb 16, 2018
  Joined: May 21, 2016
  Messages: 189
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mawazo mfu. Mchakato wa katiba mpya, hata ukireshwa mambo yatakuwa haya haya coz utapigiwa kura na wanaccm ambao kihesabu ndiyo wengi bungeni na uraiani. Ok, unashauri wapambane na wavumilie virungu je, umeambiwa kuwa virungu ndiyo vitakavyotumika peke yake kuwadhibiti? Wakilambwa shaba watu 2, unadhani kuna atakayevumilia? wote watakimbilia majumbani na kijificha na waking'ang'ani basi vijana wanaweza kuitwa ili kufanya usafi mitaani ili tuone kama kuna atakayebaki mtaani.

  Wewe bado bwana mdogo sana, tulia ukue, mambo haya yanazidi kimo chako cha kufikiri.
   
 15. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Hoja yako ni nini hasa mbona jazba tupu!! Mbona 2015 mlivunja watu miguu pale biafra na mabomu ha machozi pamoja na risasi mlitumia ila vijana walikomaa hadi mtulia akatangazwa!!!

  Mkuu hakuna kitu kinaweza zidi nguvu ya umma tumeona wote zimbabwe afrika kusini na ethiopia bila nguvu ya umma wale viongozi wasingejiuzulu..... Sasa kma huko imewezekana pamoja na hapo hapo kinondoni 2015 nguvu ya umma ilitumika kwanni ishindikane mwaka huu???

  Nguvu ya umma ndio suluhisho la huu ushenzi wa CCM
   
 16. m

  msege Senior Member

  #16
  Feb 16, 2018
  Joined: May 21, 2016
  Messages: 189
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Endelea kuota
   
 17. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Sawa tukutane jumapili asubuhi usikimbie tu
   
 18. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2018
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,537
  Likes Received: 4,859
  Trophy Points: 280
  Mkuu Zitto Junior upo?

  Haya, mimi napita tu.
   
 19. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2018
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,479
  Likes Received: 7,205
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilionya kuwa haya yatatokea naona wametuzidi ujanja hivyo tumejizika rasmi

  Kuanzia wiki ijayo wabunge zaidi watahama hii ndio ilikuwa turning point ya hamahama..... Wameshajua kumbe hata tukihama hatuwezi shindwa so tutegemee upinzani kumeguka zaidi

  I expected this thus i concede defeat kilichobaki ni kupigania tume huru wakishindwa na hilo basi 2020 hata tusihangaike kuingia mzigoni tutaambulia 10%
   
 20. Heri lee

  Heri lee JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2018
  Joined: Aug 16, 2013
  Messages: 878
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 80
  Iko ivi Mkuu hakuna haja ya kuumiza kichwa rais wa nchi ya Tanzania amerudisha mfumo wa chama kimoja itafika mahali hapa nchi hakutakuwa na uchaguzi wa multiparty tena aa
  Huko Tanzania itabidi wawemakini. Sana
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...