Uchaguzi 2020 Umuhimu wa uchaguzi mdogo na hatma ya upinzani kuelekea 2020

Mtoa post toa ufafanuzi unaposema Tume huru una maanisha nini?
Namaanisha Tume isiyolalia upande wowote wa vyama vinavyogombea kwa ufupi iwe HURU dhidi ya serikali ili ifanye mambo yake kwa uhuru zaidi at least kama CAG.

Mfano Rais asiteue yeyote huko NEC bali utengenezwe mfumo utakaopata Wakurugenzi au wajumbe wa NEC bila mkono wa serikali ambayo kwa namna moja ama nyingine huwa ina Rais aliye mwenyekiti wa chama

Sasa kwa mazingira ya sasa unategemea mwenyekiti wa chama kinachoshiriki uchaguzi atachagua wenyeviti wa NEC ambao sio watiifu kwake??

Nakumbuka kikwete 2015 alifanya mabadilko ya wakurugenzi wa NEC siku 3 kabla ya uchaguzi...... Sasa kwa staili hiyo unategemea chaguzi ziwe huru na haki kwa mtazamo wako??
 
Kujifunza kutoka kwa nani? Na wapi?
Kujifunza kutoka NEC inavyoendesha chaguzi zake kilaghai.... Unajua NEC inaendeshwa kma enzi za chama kimoja mfano wagombea wa upinzani wakirudisha fomu zinakataliwa mara mkurugenzi anazima simu n.k nilitegemea upinzani uje na mbinu mpya na sio kurudia kushiriki chaguzi za NEC ileile alafu wanategemea miujiza kushinda.

Ilitakiwa wajifunze either waende mahakamani kupinga hizi tume, au waende bungeni wadai mabadiliko ya sheria au watumie njia mbadala kama odinga ili kuifuta hii tume mbovu kabisa maana inakatisha sana tamaa sisi wapiga kura tunaenda kwenye vituo tunapanga foleni kuifuta CCM alafu tunaona CCM inatangazwa, inaudhi mno na inauwa morale maana tunajua hata tukipiga kura atatangazwa CCM

Kwa staili hii 2020 watapiga kura watu wachache sana na hakuna mpinzani atashinda jimbo.... Na wategemea wengi zaidi kuhama maana sidhani kuna mtu atabaki kwenye chama ambacho anajua 2020 hakiambulii kitu.
 
SWALI: Kwani uhuru wa kitu unapimwaje?
 
Kwa hiyo wabunge wote wa upinzani wameingia bungeni kilaghai?
 
Uhuru wa kitu unapimwa kwa kiwango cha kujitegemea kimaamuzi,kimsimamo,maoni,mifumo n.k bila kuingiliwa/kupangiwa na mtu mwingine.

Ok, umesema uhuru unapimwa kwa kujitegemea kwa hayo uliyoyataja!!

Naomba majibu ya hoja zako

1. Lini na wapi NEC ilitegemea maamuzi kutoka taasisi yoyote?
2. Ni maoni gani ambayo wewe unadai yanaendesha shughuli za tume?
3. Umeitaja mifumo, Je unaweza kueleza aina ya mifumo inayotumika ambayo ni tegemezi?
4. Je ni kwa namna gani na ni lini NEC imeingiliwa au kupangiwa shughuli zake na mtu mwingine, kwa mifano.

Asante.
 
Kwa hiyo wabunge wote wa upinzani wameingia bungeni kilaghai?
Wengi wameingia kwa nguvu ya umma hakuna mpinzani aliyetangazwa usiku ule wa uchaguzi bila kwanza mabomu kupigwa,watu kutishia kuchoma vituo n.k ndipo wametangazwa. Ukilala lala kma kafulila na wenje ndio unapigwa goli la mkono huku unaangalia!!

Nakumbuka hata huku ujiji Ali mlee wa CHADEMA alikuwa anaongoza kura kwa mbali dhidi ya serukamba ila CCM wakadai kura zirudiwe kuhesabiwa..... Kibaya zaidi zimekaa humo usiku kucha na watu walishaingia ndani na kutoka bila control masanduku yakabaongezwa kinyemela mwisho wa siku Imerudiwa tu ikaonekana Serukamba ndio anakura nyingi

Such ujanja ndio wanatumia CCM so ukicheka cheka tu inakula kwako
 
Kwa ufahamu wangu Uchaguzi wowote ni mchakato unaohusisha Vyama vya Siasa, Wagombea, Taasisi za usimamizi wa mchakato husika na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi ambao ndio watoa maamuzi. Hivyo wagombea wote walioshinda na kutangazwa katika nafasi walizo nazo wamepita kwa kupigiwa kura halali/ maamuzi ya wananchi/ nguvu ya wananchi/umma kupitia SANDUKU LA KURA. Hakuna nguvu ya umma kwenye Demokrasia au kwenye uchaguzi zaidi ya KURA, na ukiona hao wabunge unaowataja wanaendelea kutekeleza majukumu yao ujue ni kwa sababu walipata ridhaa ya umma na si vinginevyo na ndio maana TUME ya Uchaguzi yenye mamlaka ya Kusimamia na kuendesha Uchaguzi nchini Tanzania iliwatangaza na kuwapa vyeti vya Ushindi.
 
Ok, umesema uhuru unapimwa kwa kujitegemea kwa hayo uliyoyataja!!

Naomba majibu ya hoja zako

1. Lini na wapi NEC ilitegemea maamuzi kutoka taasisi yoyote?
2. Ni maoni gani ambayo wewe unadai yanaendesha shughuli za tume?
3. Umeitaja mifumo, Je unaweza kueleza aina ya mifumo inayotumika ambayo ni tegemezi?
4. Je ni kwa namna gani na ni lini NEC imeingiliwa au kupangiwa shughuli zake na mtu mwingine, kwa mifano.

Asante.
1. Lini 2015 na wapi Mlimani city!!...... Still uchaguzi wa 2015 wa Rais matokeo waliokuwa wakitangaza NEC yalikuwa yanatoka mlimani city badala ya kwenye vituo ndio maana kura zilishapigwa toka tarehe 25 ila wakatangaza majimbo mawili tu within the following 20 hours. Yaani CCM na CHADEMA wakawa na matokeo yao ya nchi nzima ila NEC eti bado!!

2 & 3. Mfumo wa sasa wakurugenzi wake na wajumbe kibao wanateuliwa na Rais ambaye naye ni mwenyekiti wa chama cha siasa hivyo ana ubavu wa kuweka watu wake kama alivyofanya kikwete wakati wa uchaguzi 2015 sasa hapo kuna uhuru kweli. Na kwa namna yeyote tume inabanwa na mfumo hivyo kujikuta inaegemea upande mmoja tu maana kama mnachaguliwa na mwenyekiti wa CCM je unategemea mtu anayekuchagua umuangushe???

4. Uchaguzi 2015 nakumbuka ulinikutia mbagala mgombea wa CUF alikua anaongoza kwa mbali kabisa ila moments later wakaja kina ridhiwan wakishinikiza mgombea wa CCM bwana mangungu atangazwe mbunge kwa namna yeyote..... Baadae wakatuhadaa kuwa uchaguzi umefutwa ile tumesepa tu wakabandika kuwa mshindi ni CCM kwa mbali sana. Mifano pia ipo mingi mfano uchaguzi wa kwela magharibi kwa daniel ngogo kule nako tume walipewa maelekezo kuzuia kutangaza matokeo ambaye mgombea wa chadema alikuwa akiongoza kwa mbali sana.... masaa machache baadae akatangazwa CCM ndio mshindi.
 
Kwa ufahamu wangu Uchaguzi wowote ni mchakato unaohusisha Vyama vya Siasa, Wagombea, Taasisi za usimamizi wa mchakato husika na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi ambao ndio watoa maamuzi. Hivyo wagombea wote walioshinda na kutangazwa katika nafasi walizo nazo wamepita kwa kupigiwa kura halali/ maamuzi ya wananchi/ nguvu ya wananchi/umma kupitia SANDUKU LA KURA. Hakuna nguvu ya umma kwenye Demokrasia au kwenye uchaguzi zaidi ya KURA, na ukiona hao wabunge unaowataja wanaendelea kutekeleza majukumu yao ujue ni kwa sababu walipata ridhaa ya umma na si vinginevyo na ndio maana TUME ya Uchaguzi yenye mamlaka ya Kusimamia na kuendesha Uchaguzi nchini Tanzania iliwatangaza na kuwapa vyeti vya Ushindi.
Mkuu ambacho huelewi ni kipi??? Kwa Tanzania ili uwe mbunge ni mpaka tume ikutangaze which is correct lakini mchakato mpaka utangazwe ndio huwa hauamuliwi na tume bali nguvu ya umma hasa kama umetoka upinzani

Mfano silinde kwenye mchakato ikaonekana ana kura nyingi sana kuliko CCM ila HAKUTANGAZWA na tume sababu bado CCM walitaka kura zirudiwe kuhesabiwa ambapo masanduku yalipangwa kuongezwa ila wananchi wakaja juu na kutishia kuchoma vituo vya kuhesabia kura ndipo NEC ikatangaza tu silinde kashinda..... Ndio hapo naposema hakuna mpinzani alitangazwa sababu alishinda tu maana walioshinda ni wengi sana ila kuna wengine hawakutangazwa why??? Sababu ni NGUVU YA UMMA kama uliitumia ndio unatangazwa kama huitumii ndio basi imekula kwako

Kwahiyo usijikite sana kwenye sheria njoo kwenye uhalisia
 
1. Lini 2015 na wapi Mlimani city!!...... Still uchaguzi wa 2015 wa Rais matokeo waliokuwa wakitangaza NEC yalikuwa yanatoka mlimani city badala ya kwenye vituo ndio maana kura zilishapigwa toka tarehe 25 ila wakatangaza majimbo mawili tu within the following 20 hours. Yaani CCM na CHADEMA wakawa na matokeo yao ya nchi nzima ila NEC eti bado!!

2 & 3. Mfumo wa sasa wakurugenzi wake na wajumbe kibao wanateuliwa na Rais ambaye naye ni mwenyekiti wa chama cha siasa hivyo ana ubavu wa kuweka watu wake kama alivyofanya kikwete wakati wa uchaguzi 2015 sasa hapo kuna uhuru kweli. Na kwa namna yeyote tume inabanwa na mfumo hivyo kujikuta inaegemea upande mmoja tu maana kama mnachaguliwa na mwenyekiti wa CCM je unategemea mtu anayekuchagua umuangushe???

4. Uchaguzi 2015 nakumbuka ulinikutia mbagala mgombea wa CUF alikua anaongoza kwa mbali kabisa ila moments later wakaja kina ridhiwan wakishinikiza mgombea wa CCM bwana mangungu atangazwe mbunge kwa namna yeyote..... Baadae wakatuhadaa kuwa uchaguzi umefutwa ile tumesepa tu wakabandika kuwa mshindi ni CCM kwa mbali sana. Mifano pia ipo mingi mfano uchaguzi wa kwela magharibi kwa daniel ngogo kule nako tume walipewa maelekezo kuzuia kutangaza matokeo ambaye mgombea wa chadema alikuwa akiongoza kwa mbali sana.... masaa machache baadae akatangazwa CCM ndio mshindi.

" Lini 2015 na wapi Mlimani city!!...... Still uchaguzi wa 2015 wa Rais matokeo waliokuwa wakitangaza NEC yalikuwa yanatoka mlimani city badala ya kwenye vituo ndio maana kura zilishapigwa toka tarehe 25 ila wakatangaza majimbo mawili tu within the following 20 hours. Yaani CCM na CHADEMA wakawa na matokeo yao ya nchi nzima ila NEC eti bado!! "

JIBU - HUO SIO UTHIBITISHO TOSHA kuhusu madai yako, bado hujatoa ushahidi wa kutosha wa madai yako unifanye niamini unachokisema, mimi mwenyewe nilikua mpiga Kura mwaka 2015 na nilifuatilia sana matokeo kwa ukaribu , Ukumbi wa Kutangazia Matokeo uliotumiwa na NEC ulikua pale UKUMBI WA KIMATAIFA WA MWL. JULIUS JULIUS NYERERE na SIO MLIMANI CITY vyombo vya Habari, Waangalizi wa Uchaguzi, Wagombea wa vyama wote walikua pale na ushahidi wa picha na kumbukukmbu kutoka TV na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi upo, Jambo la ufahamu tu ninavyojua mimi mshindi hatangazwi kwa kupata ushindi wa kituo kimoja cha kupigia Kura bali hutangazwa kwa ushindi alioupata katika eneo zima alilogombea kama ni Udiwani - Jumla ya Kura za vituo vya Kata nzima, Kama ni Jimbo ni jumla ya kura za Kata zote zinauzounda jIMBO husika na Kama ni Urais ni jumla ya matokeo ya majimbo yote kwa nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar.

JIBU - MIMI ni muumini wa Sheria na nina heshimu Sheria, Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Ibara 74 (1) na kuendelea utaona wazi namna hii taasisi tunayoizingumzia inavyopata viongozi wake kuanzia Mwenyekiti na Watendaji wengine, jipe muda usome plz. Walau mimi nakupa rejea, ukisoma Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa Tume katika kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba haitalazimika kupokea maelekezo au amri kutoka kwa mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au kufuata maoni ya Chama chochote cha Siasa.

JIBU - Kama nilivyotangulia kuchangia katika post zangu mimi nikiwa mdau wa Siasa za Tanzania na muumini wa Sheria za nchi nachojua mshindi hutangazwa mara baada ya kupata kura nyingi halali kuliko wagombea wengine sasa unaposema alishinda huyu akatangazwa mwingine sio sahihi, hata hivyo sheria iko wazi inatoa nafasi kwa Mgombea ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi kwenda Mahakamani mifano ipo mingi kumbuka kesi ya STEPEHEN WASIRA (CCM) dhidi ya ESTER BULAYA( Chadema) katika kesi hii Wasira alishindwa, Mahakama zipo zitumike.
 
Mkuu ambacho huelewi ni kipi??? Kwa Tanzania ili uwe mbunge ni mpaka tume ikutangaze which is correct lakini mchakato mpaka utangazwe ndio huwa hauamuliwi na tume bali nguvu ya umma hasa kama umetoka upinzani

Mfano silinde kwenye mchakato ikaonekana ana kura nyingi sana kuliko CCM ila HAKUTANGAZWA na tume sababu bado CCM walitaka kura zirudiwe kuhesabiwa ambapo masanduku yalipangwa kuongezwa ila wananchi wakaja juu na kutishia kuchoma vituo vya kuhesabia kura ndipo NEC ikatangaza tu silinde kashinda..... Ndio hapo naposema hakuna mpinzani alitangazwa sababu alishinda tu maana walioshinda ni wengi sana ila kuna wengine hawakutangazwa why??? Sababu ni NGUVU YA UMMA kama uliitumia ndio unatangazwa kama huitumii ndio basi imekula kwako

Kwahiyo usijikite sana kwenye sheria njoo kwenye uhalisia

NGUVU YA UMMA kwenye uchaguzi ni nini hasa? Au kuna nguvu ya Umma kwenye uchaguzi zaidi ya KURA?
 
Mkuu kuwa realistic basi tuache bureaucracy ya kimakaratasi...... Nguvu ya umma kwenye uchaguzi maana yake pale ambapo una uhakika umepata kura nyingi kwa ushahidi wa fomu za NEC lakini tume haikutangazi basi ndio unatumia nguvu za kimwili kuwalazimisha NEC kutangaza matokeo.
 
Mkuu napata confusion na maelezo yako yaani unasema unasema mgombea amepata kura nyingi kwa ushahidi wa fomu za NEC, lakini Tume (NEC) ambayo ndiyo imekupa hizo fomu za ushahidi haikutangazi? is it realistic?

Maoni yangu: Kutokujua Sheria kunatugharimu wengi sana hivi kama mgombea ana ushahidi wa fomu wa kupata kura nyingi kwa nini asiende mahakamani kufungua kesi?
 
" Lini 2015 na wapi Mlimani city!!...... Still uchaguzi wa 2015 wa Rais matokeo waliokuwa wakitangaza NEC yalikuwa yanatoka mlimani city badala ya kwenye vituo ndio maana kura zilishapigwa toka tarehe 25 ila wakatangaza majimbo mawili tu within the following 20 hours. Yaani CCM na CHADEMA wakawa na matokeo yao ya nchi nzima ila NEC eti bado!! "

JIBU - HUO SIO UTHIBITISHO TOSHA kuhusu madai yako, bado hujatoa ushahidi wa kutosha wa madai yako unifanye niamini unachokisema, mimi mwenyewe nilikua mpiga Kura mwaka 2015 na nilifuatilia sana matokeo kwa ukaribu , Ukumbi wa Kutangazia Matokeo uliotumiwa na NEC ulikua pale UKUMBI WA KIMATAIFA WA MWL. JULIUS JULIUS NYERERE na SIO MLIMANI CITY vyombo vya Habari, Waangalizi wa Uchaguzi, Wagombea wa vyama wote walikua pale na ushahidi wa picha na kumbukukmbu kutoka TV na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi upo, Jambo la ufahamu tu ninavyojua mimi mshindi hatangazwi kwa kupata ushindi wa kituo kimoja cha kupigia Kura bali hutangazwa kwa ushindi alioupata katika eneo zima alilogombea kama ni Udiwani - Jumla ya Kura za vituo vya Kata nzima, Kama ni Jimbo ni jumla ya kura za Kata zote zinauzounda jIMBO husika na Kama ni Urais ni jumla ya matokeo ya majimbo yote kwa nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar.

2 & 3. Mfumo wa sasa wakurugenzi wake na wajumbe kibao wanateuliwa na Rais ambaye naye ni mwenyekiti wa chama cha siasa hivyo ana ubavu wa kuweka watu wake kama alivyofanya kikwete wakati wa uchaguzi 2015 sasa hapo kuna uhuru kweli. Na kwa namna yeyote tume inabanwa na mfumo hivyo kujikuta inaegemea upande mmoja tu maana kama mnachaguliwa na mwenyekiti wa CCM je unategemea mtu anayekuchagua umuangushe???

JIBU - MIMI ni muumini wa Sheria na nina heshimu Sheria, Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 Ibara 74 (1) na kuendelea utaona wazi namna hii taasisi tunayoizingumzia inavyopata viongozi wake kuanzia Mwenyekiti na Watendaji wengine, jipe muda usome plz. Walau mimi nakupa rejea, ukisoma Ibara ya 74(11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa Tume katika kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba haitalazimika kupokea maelekezo au amri kutoka kwa mtu yeyote au Idara yoyote ya Serikali au kufuata maoni ya Chama chochote cha Siasa.

4. Uchaguzi 2015 nakumbuka ulinikutia mbagala mgombea wa CUF alikua anaongoza kwa mbali kabisa ila moments later wakaja kina ridhiwan wakishinikiza mgombea wa CCM bwana mangungu atangazwe mbunge kwa namna yeyote..... Baadae wakatuhadaa kuwa uchaguzi umefutwa ile tumesepa tu wakabandika kuwa mshindi ni CCM kwa mbali sana. Mifano pia ipo mingi mfano uchaguzi wa kwela magharibi kwa daniel ngogo kule nako tume walipewa maelekezo kuzuia kutangaza matokeo ambaye mgombea wa chadema alikuwa akiongoza kwa mbali sana.... masaa machache baadae akatangazwa CCM ndio mshindi.

JIBU - Kama nilivyotangulia kuchangia katika post zangu mimi nikiwa mdau wa Siasa za Tanzania na muumini wa Sheria za nchi nachojua mshindi hutangazwa mara baada ya kupata kura nyingi halali kuliko wagombea wengine sasa unaposema alishinda huyu akatangazwa mwingine sio sahihi, hata hivyo sheria iko wazi inatoa nafasi kwa Mgombea ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi kwenda Mahakamani mifano ipo mingi kumbuka kesi ya STEPEHEN WASIRA (CCM) dhidi ya ESTER BULAYA( Chadema) katika kesi hii Wasira alishindwa, Mahakama zipo zitumike.
Ushahidi siwezi kuwa nao wa kimakaratasi wa kushikika ila niliona kwa macho yangu hayo yakifanyika ila mkifanya uchunguzi huru mbona utabaini ni kweli lakini ni lini NEC imewahi kubali madai ya upinzani na kuunda tume ya kuchunguza? Kama hawajawahi kwanini mdai ushahidi kwa sisi tunaolalamika?? Kwenye makinikia tulijua tunaibiwa ila hatukua na ushahidi ndio maana tukaunda tume sasa kipi kigumu kuunda tume kama walivyoshauri wapinzani kwa miaka zaidi ya 20 sasa?? Tuache huu utaratibu wa muibua tuhuma kuleta ushahidi maana Acacia na wenyewe wangesema mlete ushahidi kabla ya tume mngesemaje?? Ingekuwa haki??

Kuhusu kwenda mahakamani same problems ..... Wanataka uje na uthibitisho kuwa uliibiwa kura au ulishinda hivyo matukio kama masanduku kuibwa kma uliona kwa macho ila hauwezi kuthibitisha ndio imekula kwako..... Hoja sio kwenda mahakamani ilitakiwa NEC iunde ofisi maalum ya kufanyia kazi malalamiko kama hayo na wenyewe kufanya uchunguzi ili watumishi wake wasio waaminifu wawajibishwe na kama kuna mtu kaonewa basi apate haki yake ila kusema uende mahakamani bado kuwa na ushahidi wote ni changamoto ni sawa na mtu akuambie uthibitishe Mungu au shetani yupo mahakamani utaweza?? Je usipoweza ina maana Mungu na shetani hawapo??

Alafu pia katiba inachosema ni kingine na inavyotekelezwa ni jambo jingine...... Ssa mkuu unasoma tu katiba alafu unaconclude ndio hali ilivyo?? Je kwa staili hii si hata Tume ya haki za binadamu utasema inapigania haki za wanyonge ilihali kuna wafungwa mwaka wa 10 huu wanaozea mahabusu bila kesi zao kuitwa mahakamani!!! So tusijikite kwenye sheria tu bali uhalisia maana kma katiba ingekuwa inafuatwa kama ilivyo kusingekuwepo na malalamiko ya upinzani kwenye kila chaguzi

Embu jikite kwenye utekelezaji wa sheria sio sheria kama sheria pekee
 
Mkuu napata confusion na maelezo yako yaani unasema unasema mgombea amepata kura nyingi kwa ushahidi wa fomu za NEC, lakini Tume (NEC) ambayo ndiyo imekupa hizo fomu za ushahidi haikutangazi? is it realistic?

Maoni yangu: Kutokujua Sheria kunatugharimu wengi sana hivi kama mgombea ana ushahidi wa fomu wa kupata kura nyingi kwa nini asiende mahakamani kufungua kesi?
Kafulila alikuwa nazo mbona hakutangazwa?? Kesi zina mlolongo wake na pia ushahidi wanaokuwa nao wagombea ni mdogo sana ili kuifanya korti kutengua matokeo..... Ndio maana nikasuggest huu mtindo wa wagombea kusaka ushahidi sio suluhisho bali kiwepo kitengo maalum either NEC huko au polisi ambacho ndio kipewe kazi ya kusaka ushahidi maana wagombea hawawezi kuwa na access na nyaraka zite nyeti za tume ila hicho chombo cha uchunguzi kinaweza kuingia hta kwenye mawasiliano ya hao viongozi wa NEC ili kama kuna madai kwamba wanapokea maelekezo ya CCM itajulikana huko ila mkiwa mnaletewa tuhuma kama hizi then mna conclude kuwa twende mahakamani ilihali mnajua wagombea hawana ushahidi wa kutosha ni kuhadaa watu kuwa watapata haki mahakamani
 
Back
Top Bottom