Umuhimu wa michezo kwa Watoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Michezo ina umuhimu mkubwa sana katika ukuaji na ustawi bora wa mtoto. Wataalamu wa malezi wanatuambia kuwa mtoto asiyecheza huwa ni mwenye kuzubaa muda wote na mara nyingi huwa mgumu sana katika kuelewa mambo.

Pale watoto wanapocheza michezo ya viungo huwawezesha kuimarika misuli na kuwafanya wawe na afya bora kila siku. Watoto wanapocheza pia huwawezesha kutoshambuliwa na maradhi nyemelezi mara kwa mara hali inayowezesha kuwa na afya bora Zaidi.

Michezo ni nyezo ya burudani na furaha kwa watoto kwani mara nyingi michezo ya Watoto hutawaliwa na vicheko na tabasamu. Watoto wanapocheza husahau yote waliyoyapitia na hujihisi wenye furaha Zaidi.


SemaTanzania
 
Wekeni tu bayana mnakusudia michezo gani hapa MMU!

Sisi tunaijua vema michezo ya watoto, na tumeicheza kweli kweli.
 
Back
Top Bottom