Wild Flower
Member
- Jul 20, 2023
- 80
- 96
Siku hizi idadi ya watoto wanaokwenda kumbi za starehe ni wengi mno. Na utawakuta wanakunywa pombe, kutumia madawa ya kulevya, kujiuza, kuvuta sigara, kufanya biashara haramu na mambo mengine yanayokiuka jamii.
Tatizo hili tunaweza tusione madhara yake sasa hivi lakini ndo tunavyokuza kizazi cha baadae.
Ni wakati sasa mamlaka husika kuchukua hatua za kudhibiti tatizo hili kwa kuanzisha utaratibu wa kuangalia vitambulisho vya wateja wanaohudhuria sehemu hizi kama nchi mbalimbali duniani zinavofanya. Na vitambulisho hivyo viwe na picha na umri ili kuthibitisha taarifa za kweli znazotolewa na mteja.
Hatua hii itasaidia kuhakikisha kuwa mazingira ya starehe yanabaki salama kwa wote wanaohudhuria na kuzuia uwepo wa watoto chini ya umri wa 18 ambao hawaruhusiwi kisheria kuingia katika maeneo hayo.