Utoaji wa Vitambulisho vya Machinga waanza kukwama nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Utoaji wa vitambulisho vya wamachinga umebaki kizungumkuti kutokana na kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya kuhuishwa kwake, ikiwa ni miaka tangu vitolewe na Serikali.

Desemba 2018, Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alizindua vitambulisho vya machinga kila mkoa ukikabidhiwa vitambulisho 25,000.

Licha ya kuahidiwa mara mara kadhaa, tangu vitolewe vitambulisho hivyo vilivyotakiwa kudumu kwa mwaka mmoja, hakuna vipya vilivyotolewa wala kuwepo taarifa za lini vitapatikana.

Wakati hali ikiwa hivyo, imefahamika kuwa uhamisho wa kundi la wamachinga kutoka chini ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu umechangia kuchelewa vitambulisho hivyo.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikuwa inaendelea na maandalizi ya vitambulisho vya kidigitali chini ya mfumo maalumu kwa waombaji wa waliothibitishwa na Tamisemi, lakini baada ya mabadiliko ilisitisha.

“TRA imesitisha hadi wizara ya Tamisemi ihamishie majukumu ya kusimamia machinga kwenda Wizara hiyo ya jinsia na makundi maalumu. Sasa hatua hizo zinafanyika kisheria ili wapate instruments na TRA,” kilieleza chanzo chetu.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Zainab Chaula alipoulizwa alisema mfumo huo ulikosa taarifa zenye mahitaji ya msingi, hivyo kusubiri takwimu za Sensa ya Watu na Makazi.

“Ni kweli mfumo upo, sasa baada ya matokeo ya sensa tulianza kushirikiana na TRA, Tamisemi, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakala wa Serikali Mtandao na machinga wenyewe. Tumezigawanya taarifa zao katika makundi, huyu anafanya biashara gani, yuko wapi,” alisema Dk Zainabu.

“Pia tumewaunganisha na mfumo wa taasisi za kifedha, machinga wanaotakiwa kusajiliwa ni milioni 1.68, lengo ni kuwarasimisha, kuwalea na kuwakuza ili wachangie pia maendeleo ya Taifa lao. Tuko hatua za mwisho kukamilisha marekebisho hayo mwezi huu, tutawajulisha pia wanalipia shingapi kadi hizo.”

Endapo kila machinga atalipia ada ya Sh 20,000 kwa mwaka kama ilivyokuwa awali, Serikali itaingiza mapato ya Sh33.6 bilioni kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2023.

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 44 ya bajeti ya mradi wa Sh76 bilioni uliotolewa wiki iliyopita kusambaza umeme katika mikoa minane ya pembezoni.

Januari 25, 2022, Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza machinga nchini kama kundi maalumu kuwa chini ya wizara ya Jinsia huku akiagiza wapewe vitambulisho hivyo baada ya kukamilika Sensa ya Watu na Makazi pamoja na ujenzi wa masoko mapya ya Jangwani, Karume na Kariakoo.

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo itaanza kutoa vitambulisho itakapopatiwa uthibitisho na wizara husika.

“Wizara husika itakapothibitisha, tutaanza kutoa vitambulisho,” alisema bila kufafanua.

Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Taifa, Steven Lusinde alisema “vitambulisho tulipata awamu moja tu ya mwaka 2018/19, mwaka 2020 vikauzwa nusu na kusitishwa hadi leo hakuna machinga aliyepata kitambulisho.”

“Hadi sasa tunatumia vitambulisho vya vyama vyetu katika maeneo tunayofanyia kazi,” alisema Lusinde.

Itaongeza mapato

Hatua ya kuitambua kada hiyo inaelezwa kuwa itaongeza mapato ikiwa sehemu ya sekta isiyokuwa rasmi, kwa mujibu wa Lucas Katera, mtafiti mwandamizi wa Repoa.

Katera alisema kundi hilo ni sehemu ya asilimia takribani 30 ya sekta isiyokuwa rasmi inayotakiwa kufikiwa na kutambuliwa.

“Kwa Serikali (hatua hiyo) litaongeza mapato na pia itajenga uwezo wa kutambua wengine wote ili kupanua wigo wa kodi,” alisema

Mawazo ya Katera yanaungwa mkono na Dk Constantine George, mtafiti wa sekta isiyokuwa rasimi aliyetoa mfano wa Rwanda, kuwa ilianza kutambua na kurasimisha kundi hilo mwaka 2000 kwa kutoa ujuzi na mitaji kwa vyama vya wahusika kabla ya kuanza kukusanya mapato.

Dk George alishauri pia Serikali kuwa na takwimu sahihi za mchango wa kundi la machinga katika pato la Taifa na katika sekta isiyo rasmi.

Takwimu za Wizara ya Viwanda na Biashara, machinga ni sehemu ya wajasiriamali milioni 3.1 wanaochangia asilimia 23.4 ya nguvu kazi nchini.

Vinasubiri sensa

Januari mwaka huu, katika mkutano wake na wafanyabiashara hao, Rais Samia aliahidi kuandaa kwa umakini vitambulisho vipya baada ya kukamilika Sensa ya Watu na Makazi pna ujenzi wa masoko makubwa ya machinga hao ikiwamo ya Jangwani, Kariakoo na Karume jijini Dar es Salaam.

“Tunasubiri tumalize sensa itakayotupatia anuani zote za makazi vitongoji na vichochoro vyote halafu ndipo tutengeneze vitambulisho kuendana na maeneo hayo.

“Kwa hiyo tutakapotoa kitambulisho tutakuwa tunajua kabisa, Lusinde kituo chake cha kazi Jangwani, umri wake, biashara yake, idadi ya watoto wake (kitambulishoa) kitakachokuwa chako daima, utakwenda nacho popote, kufanyia kazi au kupata huduma kwa hiyo mtupatie muda.”

MWANANCHI
 
Nchi yetu inachekesha yani kila kiongozi anakuja na sera zake.kesho utasikia ili
 
Kuumbeee ndio maana nimejaza kuomba kitambulisho kipya sijapatiwa na nimelipa dah! Sasa pesa hii si imepotea bure kama ndo hivyo
 
Back
Top Bottom