Umri huu ni kete yako ya mwisho, ukikosea ni majuto hadi unaingia kaburini

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
Nina miaka 37, katika umri huu nimekuwa nafanya mambo mengi ya kiuchumi na kijamii hivyo najikuta nakutana na watu wengi sana tunaobadilishana nao mawazo yanayohusu mambo mengi ya uchumi na jamii, nilichokibaini wengi wa watu wanajutia makosa yao na wameshindwa kuyarekebisha makosa yenyewe ni haya -

1. Ndoa wanaume wengi na wanawake wengi wanajutia ndoa zao na wanaona walikosea kuzaa ama kuishi na wenza wao , wengi hujiona wenye hatia na kuona hawakufanya chaguo sahihi , hata waliofanikiwa kuvunja ndoa zao hujutia vile wameshindwa kulea watoto wao pamoja na mwisho wa siku inabaki kuwa ni lawama isiyokwisha

2. Makosa ya kukimbia shule, kukosea kuchagua masomo na kazi wanazofanya ,hapa pana majuto sana , wengine hulaumu mamuzi yao ama wazazi wao kutowapatia elimu sahihi na matokeo yake wanajikuta either hawana elimu sahihi , wengine wanajiiona kazi wanazofanya sio sahihi nk na mbaya muda wakubadili kazi ama kusoma tena haupo,

3. Aina ya uwekezaji , kuna uwekezaji mzuri na uwekezaji mbaya , bahati mbaya sana kipindi tunawekeza tunakuwa hatuna clear mind, mtu ananunua kiwanja maeneo hayakuwa sahihi, mwingine anajenga nk unajikuta umetumia pesa nyingi na huwezi kuja kuipata tena hili ni tatizo na linaleta sana majuto, nina mtu huwa anajutia sana kwa nini alipoanza kazi tu akaoa, akajenga na kuingia kwenye majukumu mapema na kujikuta hana uwezo tena wa kujipanga tena labda akifika uzeeni

4. Kutomjua MUNGU ujanani wapo walioharibu afya na wapo walioharibu uchumi kwa sababu hawakumjua MUNGU , wengi hujutia mamuzi na sifa wanazotambulika nazo

6. Mahali pa kuishi , wengi wanajutia mahali wanapoishi na aina ya mazingira wanayoishi , wengi husema ningejua kipindi kile viwanja, mashamba nk vilikuwepo na bei zilikuwa rafiki ila sikufanya, wengine hujutia aina ya nyumba walizojenga na miji yao walivyoipanga nk na mwisho kabisa ni

8. Umri wa kupata watoto, wapo wanaojuta kwa nini hawakupata watoto mapema, wengine husema ningejua mtoto wa kwanza ningempata atleast na miaka 30 ila ndio hivo nilichelewa, wapo wanaoujuta kwa nini walizaa watoto wachache, sijakutan na mtu anayejuta kuzaa watoto wengi watu wanajutia umri na uchache wa watoto
 
1. ndoa wanaume wengi na wanawake wengi wanajutia ndoa zao na wanaona walikosea kuzaa ama kuishi na wenza wao , wengi hujiona wenye hatia na kuona hawakufanya chaguo sahihi , hata waliofanikiwa kuvunja ndoa zao hujutia vile wameshindwa kulea watoto wao pamoja na mwisho wa siku inabaki kuwa ni lawama isiyokwisha
Ndoa ni upuuzi.
 
Content nzuri sana

Ila uandishi bro. Ungetuachia ata nafasi kidogo. Yani umeshindwa hata kuruka mstari kwa kila point mpya..

Nimesoma tu kwasababu nayaelewa madini, ila andiko halivutii kusoma
 
Nina miaka 37, katika umri huu nimekuwa nafanya mambo mengi ya kiuchumi na kijamii hivyo najikuta nakutana na watu wengi sana tunaobadilishana nao mawazo yanayohusu mambo mengi ya uchumi na jamii, nilichokibaini wengi wa watu wanajutia makosa yao na wameshindwa kuyarekebisha makosa yenyewe ni haya -
Duh 🙄 hii imeenda chief
 
Hapo namba 2 umeniongelea mimi kabisa. Nilikosea sana kuchagua career na siwezi kurudisha muda nyuma ili nirekebishe makosa.
 
Back
Top Bottom