Hapana bado hajafikia umri wa shule, ana miezi mitano!
Mtoto kupata UTI ni kutokuwa makini kumbadilisha anapojisaidia. wanangu siwatahiri chini ya miaka miwili na hawajawahi kuugua UTI. Na kama mtu hauko makini utashangaa mtoto katahiriwa na bado anasumbuliwa na UTI.
Baada ya mimi kukosa jibu la kitaalamu kuhusu lini mtoto anapaswa kutahiriwa niliamua kuamini tu ushauri wa kitaani kuwa kutahiri mtoto mchanga kunamfanya awe na kibamia.
Mwanangu nimemtahiri na miaka miwili na alipona in a week. Tena nilinfanyia pale Regency wana wataalamu wazuri kuanzia wa nusu kaputi, doctor wa watoto na bingwa wa operation; hivyo hakuna mistake anakuwa amezungukwa na wataalamu.
Tena hakuwahi kuvaa kanga kama wengi niwaonavyo...yani doctor kanambia mvalishe kaptula kama kawaida...na hakulia hata kidogo zaidi ya kulia sindano ya nusu kaputi...katoka hapo kaendelea na mishe mishe zake za michezo. Baada ya wiki tukatoa nyuzi.
Mkuu Regency wanacharge sh. ngapi kwa operation hiyo?
Dah...... Uzi umerudi tena
Anyway napenda kuthibitisha kuwa baada ya kupata maoni anuai ya wataalamu hapa JF na kwa DRs njia sahihi na salama zaidi ya kumtahiri mtoto katika dunia yetu ya leo ni ya plastick
Kama atafungwa vizuri njia hii inatoa maumivu na kuuguza kidonda kwa sailimia 99
Haihitaji uangalizi mkubwa kama ya kukata na kushona kunakopelekea kidonda kuuguzwa na kusafishwa mara kwa mara kunako msababishia mtahiriwa mateso makubwa
ya maumivu.
Kuhusu umri hili swala ni mtambuka, nionavyo mimi umri mzuri ni akiwa mdogo inapendeza zaidi na salama zaidi kwa kupona haraka
Dhana ya kibamia ni maneno ya mitaani tu na haishauriwi kutahiriwa ukiwa umebalehe maana utaathiri baadhi ya mishipa ambayo imekomaa na kusababisha kupunguza ufanisi wa shughuli
Pia kutahiri ukiwa umebalehe ni tatizo kwa uponaji wa kidonda maana kila mara uume ukisimama utasababisha kutanuka na kusumbua jeraha hasa wakati wa asubuhi au pindi usikiapo muwasho wa kidonda husababisha uume kusimama mara kwa kwa mara.
Tujitahidi kuwatahiri watoto mapema ndani ya mwaka mmoja na tutumie njia ya kufunga plastick ambayo ni salama zaidi
, inga pia kama hutajali kumpunguzia mateso ya kuuguza kidonda na kuvaa kanga mwanao waweza tumia njia ya kukata
umri mzuri zaidi ni pale anapokuwa bado mdogo, kwasababu akishakua mtu mzima huwa wanapata tabu sana kupona kidonda. Angalau kabla hajafikisha miaka saba awe tayari kafanyiwa tohara
Teh teheeeeeeeePaulss, wale mapacha wako ni kiume au wakike?