Umri gani ni sahihi kumtahiri mtoto wa kiume? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umri gani ni sahihi kumtahiri mtoto wa kiume?

Discussion in 'JF Doctor' started by Paul S.S, Jun 21, 2010.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jamani wadau nisaidieni mwenye kujua haya mambo, ni umri upi unaoshauriwa kitaalamu kumtahiri mtoto wa kiume, na je kuna njia ngapi za kufanya hiyo kitu.

  Maana kuna maneno yanasema eti ukimfanyia akiwa bado mdogo kuanzia miaka 0 hadi mmoja eti atakuja kuwa dhaifu katika ile shughuli ya kikubwa, wengine wanasema ukimfanyia kakua ndio hiyo kitu itamtokea akiwa mkubwa

  Pia njia ipi ni salama zaidi mimi najua ya kukata na kushonwa naambiwa ipo nyingine yakufunga na plastiki, je ipi ni nzuri?

  Nategaemea msaada wenu waungwana, maana kunasehemu nilisoma eti matatizo mengi ya wanaume kushindwa kuwatimizia wepenzi wao tohara isiyo sahihi ni moja ya sababu
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  cdhani kama kuna umri sahihi wa kutahiri, nadhani inategemea na wewe mwnyewe, kwangu mie nilitahiri akiwa na mwaka 1, na alishonwa, rafiki yangu alimtahiri mtoto akiwa na miezi 3, mwingine 7...cdhani kama kuna umri sahihi...na hizo nyingine nadhani ni imani tu.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,997
  Trophy Points: 280
  Siku saba
   
 4. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kuwahi kutahiri na hizo imani ni vitu wiwili tofauti...

  Biblia inasema mtoto atahiriwe ndani ya siku 14... lakini ni vizuri akitahiriwa at least akiwa na miezi mitatu.... Hii itasaidia sana kwa sababu watoto wa kiume mara nyingi huugua sana UTI especially akianza kutambaa, na pia kwa umri huo anapona haraka sana, 7 days anakuwa amepona.
   
 5. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Lakini bado hamjajibu swali la akikuwa ataweza shughuli za kikubwa?
   
 6. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  Inategemea hata miaka miwili,
  Njia ya kushona ni nzuri zaidi
   
 7. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Anaweza
   
 8. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Jews ambao Wakristo wengi hufuata mila za kwao, wao humtahiri siku ya nane ambapo huwa wanamkabidhi mtoto hekaluni
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  siku 7 ni sahihi ni za kibibilia
   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kuongea na Dr mmoja juu ya issue hii, actually nilikwenda kumuomba ushauri kabla ya kumfanyia mwanangu tohara, na jibu lake lilikuwa hakuna specific number of days!

  Lakini kwa ushauri tu akaniambia ni vizuri zaidi kumtahiri mtoto akiwa tayari angalau ametimiza siku 7 au 8! Lakini kuwahi kabla ya hapo hakuna madhara, ila nadhani kuchelewa zaidi ndio kuna madhara hasa possibility ya maambukizi ya magonjwa!

  Kama nakumbuka vizuri manabii wengi walisisitiza mtoto kutahiriwa siku ya nane tangu azaliwe!
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo umenigusa sana, wangu mimi ana umri wa miezi 5 na anasumuliwa sana na UTI Na ndio maana wazo la kumtahiri likaja tatizo ikawa hizo myth za mtaani.

  na vipi kuhusu njia ya kushona au plastiki?
   
 12. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Njia ya kushona ni njia ambayo imedumu kwa muda mrefu, hii ya plastic ni njia mpya ambayo imejaribu kumuepusha muhusika na maambukizi ya magonjwa yanayotokana na kushirikiana vyombo vya tohara. Hivyo basi, nashauri utumie plastic kwani ni salama zaidi. Ila usafi ni wa kuzingatia ili kuepusha maambukizi.
   
 13. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  suala ni kuwa mwangalifu tu na usafi wa hali ya juu otherwise maambukizi yatakuwa palepale
   
 14. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Doctors hawashauri sana njia ya plastic, ile wanatumia tu kwa sababu wanadhani ni less painful na huuguzi kidonda... lakini madhara yake ni kwamba wakikosea kufunga, kwa mfano wakifunga kwa nguvu sana, basi inatokea Gangrine (sehemu ya juu ya uume unakosa circulation ya damu), panageuka peusi/blue na akicheleweshwa madhara yake ni mabaya zaidi... ila akiwekewa mpira inatakiwa close observation.
   
 15. Ngomo

  Ngomo Senior Member

  #15
  Jun 21, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  umri mzuri zaidi ni pale anapokuwa bado mdogo, kwasababu akishakua mtu mzima huwa wanapata tabu sana kupona kidonda. Angalau kabla hajafikisha miaka saba awe tayari kafanyiwa tohara
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,480
  Trophy Points: 280
  Sikujua kutahiri nako kuna uhusiano na pafomensi ya shughuli ya tendo la kujamiiana..... Leo ngoja nijifunze hapa.
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,480
  Trophy Points: 280
  Hili linahitaji jibu toka kwa wataalamu wa tiba na watumishi wa Mungu. Soma hili jibu hapa chini.
  Kuna swali jingine?
   
 18. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Uliza...
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,480
  Trophy Points: 280
  Mhashamu baba/mama askofu, ni umri gani sahihi wa kumtahiri mtoto wa kike?
   
 20. P

  Paul S.S Verified User

  #20
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  mimi simoooo. Askofu kazi kwako
   
Loading...