Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,471
222,798
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Marry Chatanda ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alichokiita unyanyasaji na udhalilishaji wa watendaji wanawake kwenye maeneo yao ya kazi.

Chatanda ameyasema hayo leo Jumamosi, Mei 25, 2024 jijini Dodoma wakati wa semina ya wabunge wa viti maalumu, manaibu waziri, mawaziri, makatibu wa jumuiya ya wazazi ngazi ya mkoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Abdurahman Kinana

"Kuna 'clip' imezunguka kule Arusha, Longido haikuwa jambo jema wala sio zuri hata kidogo, kama wewe ni kiongozi mkuu wa Serikali na umemuona mtendaji wako amekosea ni vizuri ukakaa na kuzungumza nao, kwa suala la udhalilishaji wa wanawake siwezi kukubaliana nalo, tunaomba tuheshimiwe wanawake, tena sisi wanawake ni watendaji wazuri kuliko wanaume.

Chatanda amesema kuwa clip hiyo tayari ameshamtumia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Abdulrahmani Kinana.

Hatua hii ya UWT inafuatia matamshi ya Makonda katika kipande kifupi cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ambapo anasikika akisema, ...usiongee na mimi hivyo nina mke mzuri huongei na mchumba wako hapa.


PIA SOMA
- LHRC yamuonya Makonda kwa kumdhalilisha Mtumishi wa Kike mbele ya Umati wa Wananchi

UPDATES:
- Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti
 
Merry chatanda amepiga kelele kumhusu makonda ,lakini pia chini chini mahali anakopita huyu kiongozi watu wanapiga kelele ambazo hazisikiki, sauti zinazomsifia ni zile ambazo zimejaa hofu. Kuogopwa! Labda anawaongoza watu kwa kuwatisha!

Moyoni hata waliomteua hawajui chakufanya! Anaweza akafanya vizuri mambo matano akaharibu mambo 20! Akipewa maiki kuhutubia watu wanashika roho mkononi kwa sababu anaweza kuongea lolote wakati wowote!

Huyu mtu ana ulemavu wa ulimi tusimhukumu ,tumuombee mungu amponye ,popote ulipo ndugu Paulo christian makonda pokea uponyaji wa ulimi katika jina la YESU kristo ,Amina
 
CCM hailei ujinga. Kama CCM yote haimtaki, ni nani huyo anayembeba na kwa nini? Mtu anayetembea anatukana kila mtu, kila mahali.

Hatujaambiwa hayo magari nani anayajaza mafuta, na nani analipa posho ya safari.. Serikali ina utaratibu, kwa nini mtumishi wa umma anaenda nje ya utaratibu na serikali imekaa kama haioni? Haimuulizi
Screenshot_20240525-184108.jpg
 
Back
Top Bottom