Umoja wa Ulaya (EU) wagawanyika mafungu matatu juu ya vikwazo vya mafuta na gesi ya Russia

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,921
15,612
Baada ya Russia kuivamia kijeshi Ukraine, Russia imewekewa vikwazo kadhaa na nchi mbali mbali zikiwemo US, UK na nchi kadhaa zinazounda Umoja wa Ulaya (EU). Ktk vikwazo vya hivi karibuni zaidi ni vikwazo vilivyotangazwa na US dhidi ya nchi hiyo kununua mafuta ya Russia na ikaahidi kutangaza vikwazo vingine dhidi ya nishati nyinginezo za Russia ikiwemo gesi huko mbeleni.

Kwa upande wa Umoja wa Ulaya, fikra ya kuweka vikwazo dhidi ya mafuta na gesi ya Russia imezua mtafaruku mkubwa kutokana na utegemezi mkubwa wa nchi za EU kwa bidhaa hizo za Russia kiasi kwamba vikwazo hivyo wakivipitisha vitawaathiri vibaya wao wenyewe. Ktk mjadala wa kuweka vikwazo hivyo, Umoja wa Ulaya umegawanyika ktk mafungu matatu yafuatayo:

1) Wanaosapoti vikwazo hivyo: Poland, France, Spain

Poland
ndiye kinara anayetaka kila aina ya vikwazo viwekwe dhidi ya Russia hata kama vikwazo hivyo vitaathiri uchumi wa nchi za Ulaya. Pamoja na kuwa nchi hiyo inawezaathirika na maamuzi ya vikwazo hivyo, Poland yaamini kuwa imejiandaa vizuri kutokana na ongezeko lake la kununua gesi asilia toka US, pamoja na ujenzi wa bomba la kuingiza gesi ya Norway kwenye nchi hiyo (Poland).
  • Mwaka jana, 2021, Poland ilinunua tani milioni 8.3 za makaa ya mawe toka Russia, yenye thamani ya zaidi ya Euro milioni 625most of
  • Mwaka 2019, 61.5% ya mafuta yote nchini Poland yalinunuliwa toka Russia.
  • 55% ya gasi itumikayo Poland hununuliwa toka Russia.
France (Ufaransa) imesema ipo tayari kuweka vikwazo ktk nishati za Russia lakini vile vile yapendelea kuweka wazi mlango wa majadiliano na Russia. Lakini pia Waziri wa maswala ya Biashara wa Ufaransa bwana Franck Riester akasema kuwa lazima tuangalie vikwazo vitavyowekwa na athari zake kwa Umoja wa Ulaya na wanachama wake.
  • 17% ya gesi yote itumikayo Ufaransa hununuliwa toka Russia
  • 7% ya mafuta yatumikayo Ufaransa hununuliwa toka Russia.
  • 30.2% ya makaa ya mawe yatumikayo Ufaransa hununuliwa toka Russia.
Spain nayo yasapoti vikwazo hivyo ingawa haivifanyi vikwazo hivyo kuwa agenda muhimu kisiasa.

2) Wapingaji wa vikwazo hivyo: Ujerumani, Hungary, Bulgaria na Finland

Ujerumani
, mtumiaji mkubwavwa mafuta ya Russia kwa Ulaya, anapinga vikali tena moja kwa moja vikwazo vyovyote vitavyowekwa dhidi ya nishati za Russia. Vice-chancellor Robert Habeck alionya kuwa vikwazo hivyo vitahatarisha utulivu wa raia wa Ujerumani na kuhatarisha upungufu mkubwa wa nishati ktk sekta kadhaa nchini.
  • Mwaka 2021 Germany ilinunua 55% ya gesi yake toka Russia, ambayo ni takribani mita za ujazo bilioni 140.
  • 35% ya mafuta ghafi yake na 50% ya makaa yake ya mawe hutegemea toka Russia.
Hungary, Waziri Mkuu Viktor Orbán amesema kinagaubaga kuwa atapinga vikwazo dhidi ya nishati za Russia ktk Umoja wa Ulaya. “Pamoja na kuwa tunalaani Russia kuivamia kijeshi Ukraine, hatutaruhusu familia za WaHungary kubebeshwa mzigo wa dhambi ya vita vya Russia (kuadhibiwa WaHungary kwa kuzuiliwa kupata mafuta na gesi za Russia),” Alisema Orbán Jumanne (8 March).

Bulgaria, Waziri Mkuu Kiril Petkov amesema serikali yake inasapoti vikwazo vyote dhidi ya Russia lakini vikwazo hivyo visiwe tu ktk mafuta na gesi za Russia. Waziri huyo akaongezea kuwa "Hatuna mbadala wa nishati hizo kwa sasa, tunategemea zaidi (mafuta na gesi za Russia)"
  • 70% ya gesi nchini Bulgaria hutoka Russia
  • 60% ya mafuta yatumikayo Bulgaria hutoka Russia
  • Bulgaria inaitegemea Russia kwa 100% ktk nishati ya nyuklia (nuclear fuel)
Finland, serikali haikubaliani na vikwazo dhidi ya nishati za Russia kwa sababu vitaathiri upatikanaji wa nishati hizo muhimu nchini.
  • 50% ya makaa ya mawe yatumikayo Finland hutoka Russia
  • Zaidi ya 60% ya gesi itumikayo Finland hutoka Russi
  • Zaidi ya 60% ya mafuta yatumikayo Finland hutoka Russia
3: Nchi zilizoamua kukaa kimya (kutokubali wala kupinga vikwazo hivyo): Italy, Czechia, Greece, Slovenia, Romania

Nchi hizo zimeamua kukalia kimya mjadala huo, na pia zategemea nishati toka Russia. Mfano:
  • 90% ya gesi asilia itumikayo Czechia hutoka Russia
  • 50% ya mafuta nchini Czechia hutoka Russia
Kiunganishi cha habari hiyo:

 
Back
Top Bottom