Umoja ni nguvu: CHADEMA wachangishana fedha ili kumtoa jela kiongozi wao aliyehukumiwa kifungo huko Mwanza

View attachment 1690755

Ili kuweka kumbukumbu vizuri , Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Kamanda Mwakihaba alishitakiwa kwa makosa ya mtandao baada ya kusambaza taarifa za ofisa kipenyo aliyeonekana karibu na Hospitali aliyolazwa Mh Tundu Lissu jijini Nairobi baada ya kushambuliwa kwenye eneo la bunge mwaka 2017 , inasemekana ofisa huyo alitumwa kwenda Nairobi kummalizia Tundu Lissu baada ya kushindikana kumuua Dodoma.

Taarifa ya Mwakihaba iliishitua Serikali ya Kenya ambapo ikaamua kuongeza ulinzi kwenye hospitali hiyo jambo lililowaudhi baadhi ya wakuda wa Tanzania , Mwakihaba akakamatwa na kushitakiwa mahakamani ambapo amehukumiwa kifungo au kulipa faini ya tsh mil 5.

Kampeni ya kulipa faini hiyo inayoendeshwa na Chadema kanda ya Victoria inakaribia kukamilika , ambapo mfungwa huyo anatarajiwa kutolewa gerezani kesho .

Mungu ibariki Chadema.
Sumu ya nyigu ameishia wap?
 
Mhhh! Badala ya kuchangashina kwajili ya maendeleo, tumebaki kuwahangaikia wanasiasa, sijui lini tutabadalika. Kwa nini wanasiasa wasichangishane wao kwa wao? Watu kama nyinyi ndo wa kwanza kuleta nyuzi za maisha magumu. Ila tunamshukuru mola kwa kutupa rais aliyeleta mabadiliko mengi
Hukumu ya kukomoana. Watu tunachangia kwa kujua wazi ni kukomoana. Na sisi tunawakomoana kwa kuchangia kuwapa ujumbe kuwa hamuiwezi CHADEMA kwa upuuzi huo.
 
John Heche. "Tunawashukuru sana Watanzania, tumevuka lengo. Kesho kamanda wetu Mwakiaba atashughuliwa na bila shaka atatoka. Tumetuma ujumbe mzito sana kwa kitendo hiki tulichokifanya."
"Ndugu zangu WATANZANIA, kwa niaba ya CHADEMA Kanda ya VICTORIA tunawashukuru sana kwa michango yenu. TUMEFIKIA lengo letu na sasa tunayo zaidi ya MILIONI 5. Hivyo tunasitisha zoezi rasmi. Tunaanda UPDATE. ASANTENI sana. MUNGU AWABARIKI.

Zacharia T. Obad.
Katibu Kanda ya Victoria"

Iwashuke Mataga
 
Mleta uzi,
Hapo kiasi kilichopatikana ni zaidi ya hapo, kwa waliochangia kupitia namba iliyotahwa anzisheni pettion ya kuomba mtadao wa simu inayodaiwa kupokea mchango wawape hesabu kamili ya kiasi kilichopitia akaunti hiyo na muamala wa mkupuo au kidogo kidogo tangu kampeni ianzishweili mjue mbivu na mbichi. Mtabaki vinywa wazi lakini kiasi kianchodaiwa kuchangishwa ni Tsh 4,774,289/00 kasoro laki
mbili na ushee kufikia lengo.

'Zimwi likujualo halikuli likakwisha' Guilty minds are always frustrated and exposed by illusions features.
Sasa umeongea nn na ww kakojoe ulale tu
 
John Heche. "Tunawashukuru sana Watanzania, tumevuka lengo. Kesho kamanda wetu Mwakiaba atashughuliwa na bila shaka atatoka. Tumetuma ujumbe mzito sana kwa kitendo hiki tulichokifanya."
"Ndugu zangu WATANZANIA, kwa niaba ya CHADEMA Kanda ya VICTORIA tunawashukuru sana kwa michango yenu. TUMEFIKIA lengo letu na sasa tunayo zaidi ya MILIONI 5. Hivyo tunasitisha zoezi rasmi. Tunaanda UPDATE. ASANTENI sana. MUNGU AWABARIKI.

Zacharia T. Obad.
Katibu Kanda ya Victoria"

Iwashuke Mataga
Mungu ibariki Chadema
 
Raha yako ni kuona waTz wa itikadi tofauti wakihangaika na vyesi , vifungo na kupotezewa uhai siyo ?!

Odhis *
No, it is more than that. Kumchangia mwizi, jambazi, muhaini, ni sawa tu na wewe mchangiaji ni jambazi. Ukisema majambazi kwa majambazi wanatoa msaada kusaidiana pindi wanapobambwa na polisi
 
Huna maana yeyote wewe. Au labda ndiyo jamaa alitoa taarifa zako ?!. Si nasikia hamuidhinishi hukumu za vifo !!. Mbona yeye mlimfuata mpaka ughaibuni ?!.

Kuwaona wafuasi wa vyama vingine kama majambazi sishangai kwani ni kanuni za ki communist

Odhis *
 
Mpaka sasa imepatikana 60m, ila tutaendelea kuchanga zaidi. Je una ushauri mwingine tena?
Bora wewe angalau umeelekea kwenye ukweli; ushauri ni kwamba msiishie kwa mwenyekiti huyo pekee wapo wengine ambao sio viongozi lakini ni wanachama kindakindaki wana kesi au wamefungwa hawana msaada wowote ile kutoka kwa viongozi wao.

Kinachobaki, kiwekezwe kwenye maeneo ya kiuchumi, kiafya, kielimu na kusaidia wenye uhitaji wa yakini kwenye jamii masikini hapo chama kitakuwa kimewekeza kwa tija.

Sina shida yoyote zaidi ya hapo labda kama unajihisi kuzitumia isivyo.
 
Kiwekezwe kwenye afya, elimu etc halafu kodi zetu zifanye nini?
 
Bora wewe angalau umeelekea kwenye ukweli; ushauri ni kwamba msiishie kwa mwenyekiti huyo pekee wapo wengine ambao sio viongozi lakini ni wanachama kindakindaki wana kesi au wamefungwa hawana msaada wowote ile kutoka kwa viongozi wao.

Kinachobaki, kiwekezwe kwenye maeneo ya kiuchumi, kiafya, kielimu na kusaidia wenye uhitaji wa yakini kwenye jamii masikini hapo chama kitakuwa kimewekeza kwa tija.

Sina shida yoyote zaidi ya hapo labda kama unajihisi kuzitumia isivyo.

Afya, elimu nk michango yetu ipo kwenye kodi. Ama unataka zaidi ya hayo? Badala ya kutaka tuwachangie hao wanacdm walaiobambikiziwa kesi, waambie viongozi wako wa ccm waache kutumia vibaya madaraka kwa kuwabambikizia kesi watu wasiowasujudia.
 
Swadakta !
 
Back
Top Bottom