Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
 
Naunga mkono hoja
emoji817.png
 
1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananch...
Ooooh!
Huyu ni dokta na Profesa, kweli?

Nchi yetu hii imepoptea kweli kweli.
Hajui Famasia kazi yake ni nini, na wala hajui kwamba kuna sheria kabisa inayotambua kazi ya Famasia duniani kote?

Andiko lote toka mwanzo halionyeshi kuwa huyu ni mtaalam kama inavyoonyesha katika utambulisho wake, MD, Ph.D. n.k.
Ni kama andiko la mtu ambaye kamaliza kidato cha nne? Leo hii anatafuta kujitambulisha kwa waziri naye awe mshauri wa waziri?

Dr Koboko, kama wewe kweli ni daktari, udaktari wako ni wa shaka sana, na huo uProfesa unaojitangaza nao sijui umeupata wapi kama hata hujui kazi za mtaalam ambaye unapaswa kushirikiana naye wakati wa kumhudumia mgonjwa. Kama umesomea Muhimbili, kuna chuo cha maFamaciia hapo hapo na wote mpo chuoni hapo, utashindwa hata kudadisi na kujua famaciia anasoma nini?

Unasema "administration of drugs" hiyo ni kazi ya daktari? Na huko kumpa mgonjwa dawa, ina maana wagonjwa wote wapo hospitalini wamelazwa wakisubiri kupewa dawa wakiwa mahtuti?

Hujui sehemu nyingine nyingi ambako dawa nyingi zaidi hutolewa bila uwepo wa nesi wala daktari?

Hata historia ya hizi taaluma huijui ilikotokea?
 
HITOMISHO.
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu
Wapi duniani kote ulikoona muundo wa namna hiyo?
 
Ooooh!
Huyu ni dokta na Profesa, kweli?

Nchi yetu hii imepoptea kweli kweli.
Hajui Famasia kazi yake ni nini, na wala hajui kwamba kuna sheria kabisa inayotambua kazi ya Famasia duniani kote?

Andiko lote toka mwanzo halionyeshi kuwa huyu ni mtaalam kama inavyoonyesha katika utambulisho wake, MD, Ph.D. n.k.
Ni kama andiko la mtu ambaye kamaliza kidato cha nne? Leo hii anatafuta kujitambulisha kwa waziri naye awe mshauri wa waziri?

Dr Koboko, kama wewe kweli ni daktari, udaktari wako ni wa shaka sana, na huo uProfesa unaojitangaza nao sijui umeupata wapi kama hata hujui kazi za mtaalam ambaye unapaswa kushirikiana naye wakati wa kumhudumia mgonjwa. Kama umesomea Muhimbili, kuna chuo cha maFamaciia hapo hapo na wote mpo chuoni hapo, utashindwa hata kudadisi na kujua famaciia anasoma nini?

Unasema "administration of drugs" hiyo ni kazi ya daktari? Na huko kumpa mgonjwa dawa, ina maana wagonjwa wote wapo hospitalini wamelazwa wakisubiri kupewa dawa wakiwa mahtuti?

Hujui sehemu nyingine nyingi ambako dawa nyingi zaidi hutolewa bila uwepo wa nesi wala daktari?

Hata historia ya hizi taaluma huijui ilikotokea?
Drugs administration na drugs dispensing ni kitu kimoja?
 
Nawe hujaandika la maana, you are bitting around the Bush. Sijaona concrete take home msg! Ainisha kazi za Hawa watu:
1. Nesi
2. Daktari
3. Mfamasia
 
Hiii ligi ya Pharmacy Vs MD +Nursing huwa haiishi. Wafamasia huwa hawataki kukubali kuwa MD yupo juu ya yote, mtu mwenye Bachelor ya Medicine doctor kwenye masters anaweza chepukia course karbia zote za Pharmacy, Ila mtu mwenye Bachelor of Pharmacy yupo limited Sana kuchepukia course za MD
 
Drugs administration na drugs dispensing ni kitu kimoja?
Hapana, siyo kitu kimoja ni vitu viwili tofauti.
Drug administration ni kumpa mgonjwa dawa au mgonjwa mwenyewe kutumia dawa kwa maelekezo aliyopewa. Si lazima nesi ampe dawa (administer) dawa kwa kila mgonjwa.

Nesi atampa mgonjwa dawa ya sindano kwa mfano, kama mgonjwa yupo hospitalini. Lakini dawa nyingi huwa self-administered na mgonjwa mwenyewe.

Daktari ha'dispense wala ha'adaminister' dawa.

Dispensing ni kutoa dawa kwa mgonjwa kunakofanywa na mfanyakazi wa afya, iwe hospitalini au madukani
 
Hiii ligi ya Pharmacy Vs MD +Nursing huwa haiishi ....!! Wafamasia huwa hawataki kukubali kuwa MD yupo juu ya yote, mtu mwenye Bachelor ya Medicine doctor kwenye masters anaweza chepukia course karbia zote za Pharmacy, Ila mtu mwenye Bachelor of Pharmacy yupo limited Sana kuchepukia course za MD
Wazo potofu kabisa ambalo linaonyesha huna ufahamu na haya mambo.

Matibabu ya mgonjwa yeyote ni 'teamwork' hakuna aliye na uwezo juu ya mwingine katika timu hiyo. Kila mtu ana majukumu yake yanayofahamika vizuri kabisa.

Hiyo kasumba ya Daktari kuwa juu ya wengine ilishapitwa na wakati zamani sana.
 
Nawe hujaandika la maana, you are bitting around the Bush. Sijaona concrete take home msg! Ainisha kazi za Hawa watu:
1. Nesi
2. Daktari
3. Mfamasia
Ukitaka nitakupa shule kabisa, nina hakika na hilo.

Ila sahihisha hili la "bitting about the bush" kwanza.

BTW, unataka niandike la maana vipi, lile linalokufurahisha wewe?
 
Ina maana mgonjwa anaweza kwenda pharmacy bila ya prescription ya daktari akapewa ata dawa za B.P, kisukari na magonjwa mengine ambayo dawa zake kalikali sio tu zina side effects ambapo inabidi umchagulie mgonjwa mwenye complex health need dawa sahihi kupunguza effects kulingana na condition zake; jumlisha na dawa zenyewe pia zinatofautiana on amount of contents za milligram ya ingridients unapewa based on the level of deterioration ya health condition yenyewe.

Hii ni hatari sana; pharmacies huku kijijini kwetu dawa wanazoweza uza bila ya prescription ni pain killers tu na creams ambazo hazina kemikali nyingi; vinginevyo dawa zote zilizobaki wanauza kwa prescription za daktari tu kutoka kituo cha afya; ata nesi awezi mwandikia mtu dawa.

Halafu ndio maana watu usomea health management au baadhi ya medics ujengewa uwezo huo kupitia succession planning as they are given supervision and planning roles ndani taasisi. Japo umeelezea kwa kina inaonekana hujui ata role ya pharmacy kwenye administration of medicine in a health system uwezi kutoa dawa ata ukiwa Dr ukafanya kazi pharmacy; mwenye kuandika dawa ni Daktari kutoka kituo cha afya tu ata kama ni repetitive prescription.

Tatizo la msingi ni kumtoa mtaalamu wa hali ya juu kwenye wizara na kutaka kuleta mambo yenu.

Mmemuongopea Ummy Mwalimu hiyo kazi ni rahisi na kweli anaamini anaiweza hajui changamoto zenyewe technically kipi kina tija kipi hakina, matokeo maamuzi yake ni ya ubishani wa pande mbili nani katumia nguvu kushika sikio lake badala ya maamuzi ambayo anaweza yafanyia technical assessment yeye mwenyewe kwa uelewa wa health care provision na kuamua ata akiulizwa anaweza tetea msimamo wake.

Na kwenye afya katika vitu vitano vya kuzingatia kwenye process za delegation uwezi ku delegate majukumu kwa mtu asie na sifa wala skills za kufanya hiyo kazi; so hiyo kozi itakuwa inafuata misingi ya afya kuwapa watu basic knowledge lakini sio kozi inayotakiwa apewe daktari wala nurse maana wao wapo above a pharmacist level they are clinically trained to diagnose and treat patients that includes deciding what medicine (pamoja na hayo awawezi toa wakiwa wafanyakazi wa pharmacy bila prescription kutoka kituo cha afya).
 
Wafamasia Tanzania wanaonekana hawana tofauti na wauza mizizi na magome ya dawa za kienyeji .

Angalau babu Dr. Idris Mtulia alijitahidi na kuacha legacy ktk fani ya pharmacology:
Pharmacology & therapeutics: A manual for medical assistants and ...
Pharmacology & therapeutics: A manual for medical assistants and other rural health workers (Rural health series) [Mtulia, I. A. T]

Wafamasia wanashindwa kueleweka umuhimu wao ktk jamii ya kiTanzania tofauti na fani zingine zinazoheshimika na kufahamika kama za manesi na madaktari wa binadamu . Na hii inajionesha Hata ka website cha school of pharmacy MUHAS Publications kana sikitisha.
 
Hapana, siyo kitu kimoja ni vitu viwili tofauti.
Drug administration ni kumpa mgonjwa dawa au mgonjwa mwenyewe kutumia dawa kwa maelekezo aliyopewa. Si lazima nesi ampe dawa (administer) dawa kwa kila mgonjwa. Nesi atampa mgonjwa dawa ya sindano kwa mfano, kama mgonjwa yupo hospitalini. Lakini dawa nyingi huwa self-administered na mgonjwa mwenyewe.

Daktari ha'dispense wala ha'adaminister' dawa.

Dispensing ni kutoa dawa kwa mgonjwa kunakofanywa na mfanyakazi wa afya, iwe hospitalini au madukani
Maelekezo ya drugs administration mgonjwa anapashwa kupewa na nani incase of self administration?
 
Hapana, siyo kitu kimoja ni vitu viwili tofauti.
Drug administration ni kumpa mgonjwa dawa au mgonjwa mwenyewe kutumia dawa kwa maelekezo aliyopewa. Si lazima nesi ampe dawa (administer) dawa kwa kila mgonjwa. Nesi atampa mgonjwa dawa ya sindano kwa mfano, kama mgonjwa yupo hospitalini. Lakini dawa nyingi huwa self-administered na mgonjwa mwenyewe.

Daktari ha'dispense wala ha'adaminister' dawa.

Dispensing ni kutoa dawa kwa mgonjwa kunakofanywa na mfanyakazi wa afya, iwe hospitalini au madukani
Mfamasia anapashwa kudispensi dawa kwa kufuata maelekezo ya nani?
 
Back
Top Bottom