Umewahi kuwa na rafiki wa kweli ambaye huwezi kumsahau kamwe?

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Habari zenu waungwana,

Katika ulimwengu wa sasa ni nadra sana kupata rafiki wa kweli ambaye unaweza kumuamini,

Nakumbuka miaka kadhaa nyuma niliwahi kuwa na rafiki, huyu alikuwa ni zaidi ya ndugu, tulielewana sana.

Tulishirikiana kwa kila jambo, Popote alipo nami nilikuwepo, jamaa alikuwa mpambanaji sana,
hakuchagua kazi ya kufanya ili mradi apate pesa,

Katika harakati za upambanaji, mimi nilibahatika kupata kazi kwenye kampuni moja ya utalii iliyopo mjini Arusha, yeye alienda mererani kwenye machimbo ya Tanzanite. Tuliendelea kuwasiliana huku tukiwa na mipango mingi,

Kuna siku mvua ilinyesha kubwa mno, maji yakajaa kwenye mashimo huko Mererani, watu wengi walipoteza maisha akiwepo rafiki yangu, ilikuwa siku ya huzuni sana kwangu, nikiri sijawahi kuwa na rafiki wa kweli kama huyu.😢😢

Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu Amen🙏🙏,

Kazi ya MUNGU haina makosa. R.I.P Rafiki wa kweli.

Je wewe umewahi kubahatika kuwa na rafiki wa kweli?
 
Mimi mwenyewe nakumbuka mwaka 2009 nilmpata rafiki was kweli sehemu moja inaitwa Makambako alikuwa Ni jamaa angu Sana kipindi tupo aAdvanced leve mara baada ya kuhitimu2011 jamaa yangu alipata mkasa wa kupigwa na nondo Kwa Mama Jonh Mbeya na kupoteza maisha mpaka leo cjawahi kupata rafiki RIP jamaa yangu Mungu akufanyie wepesi kwenye safar ya kaburi
 
kwa Uzoefu wangu kutokana na aina ya marafiki niliokutana nao kwa zaid nusu karne marafiki wa kweli na wa dhati huwa ni wale wa Utotoni na kadri umri unavyosonga utakutana na Wadau sio marafiki kulingana na hali yako na mazingira yako
 
Mimi rafiki yangu wa kweli alikua ni mtoto wa mama yangu mdogo. Jamani tulipendana na tulishibana siwezi kuelezea. Mwaka 2021 i lost her to covid 😭 sijawahi tena kuwa na rafiki kama yeye. Mpaka leo nina jeraha ambalo siwezi kulielezea. Grief is a lonely and painful journey 🙌🏾
 
Mimi mwenyewe nakumbuka mwaka 2009 nilmpata rafiki was kweli sehemu moja inaitwa Makambako alikuwa Ni jamaa angu Sana kipindi tupo aAdvanced leve mara baada ya kuhitimu2011 jamaa yangu alipata mkasa wa kupigwa na nondo Kwa Mama Jonh Mbeya na kupoteza maisha mpaka leo cjawahi kupata rafiki RIP jamaa yangu Mungu akufanyie wepesi kwenye safar ya kaburi
Pole sn
 
Wapo ndiyo roho zao ni nyeupe hazina doa ila wengine ni madoa doa tu na wengine ni nyeusi tiiii!!! Kama giza
 
Dah umenikumbusha rafiki yangu omary yahaya tulikuwa tunaenda wote shule na kurud wote dingi yake alikuwa mjeda na kwao kulikuwa na Yale malori ya zawani utundu wetu siku moja aliiba funguo tukapanda akaliwasha lilienda kukita mtaroni aisee tulichezea fimbo ,cha kushukuru rafiki yangu bado yupo tumepotezana sababu ya life ila ni rafiki yangu wa utotoni tulibond sana
 
Yale malori yenge pua
Dah umenikumbusha rafiki yangu omary yahaya tulikuwa tunaenda wote shule na kurud wote dingi yake alikuwa mjeda na kwao kulikuwa na Yale malori ya zawani utundu wetu siku moja aliiba funguo tukapanda akaliwasha lilienda kukita mtaroni aisee tulichezea fimbo ,cha kushukuru rafiki yangu bado yupo tumepotezana sababu ya life ila ni rafiki yangu wa utotoni tulibond sana
 
Rafiki wa kweli tunawapataga utotoni huko makwetu ama lah japo ni nadra mashuleni pia ila hawa wengi ni wachumia tumbo tu.

Ila kuna wale uko nao toka utotoni unaenda advance unarudi (kama yeye hakufaulu) bado mnakua wana tu, unaenda chuo unarudi kitaa bado ni wana tu haijalishi mna tofauti gani kielimu.
 
Dah Rafiki wa kweli nilimpata tukiwa advance aisee
Nilienda ile shule lkn nikakuta Advance walomaliza f4 ple wanapendana sana ila ss wapya kma wanatudharau hivi

Basi nikampata Rafiki wa kweli ambae nae pia aikua mgeni tukawa tunasoma pamoja haswa somo la chemistry tunatoleana maswali ple kwa kutumia Ngaiza katika Physical chemistry bhna weee Rafiki akaja kukutwa na shida ya Ada sasa mzazi wake hajui jinsi ya kulipa akamtumia hela shangazi yake ambae yupo Moshi akamlipie ada mwanawe dah hpa ndo mkasa wa kumpoteza Rafiki wa ukweli ulipoanza

Siku ya siku yule shangazi ya Rafiki kaja shule ila second master akamwambia ss hatupokei cash bali nenda bank ukalipie na mm siku hii niliomba ruhusa niende mjini kweli bhna shangazi mtu kaenda bank ila muda ulikua ushaenda hakuweza kulipa basi shangazi akasema atalipia kesho na risiti ataleta shule.

Heee kimbembe kilianza apo shangazi hakulipa ile ada na yule Rafiki akafukuzwa shule akaenda shule moja ipo town ivi ili amalize F6 akakubaliwa ila kinachonisikitisha kua rafiki angu huyu hakuweza kufanya mtihani wa Physics wa theory wa Necta hatimae kupelekea kupata div3 ambayo haikumuwezesha kuendelea na degree dah siku alivonambia ivo nililia kwakweli mana kila nikifikiria tulipotoka ila shangazi yake ndo akaja kua chanzo na Rafiki kutofanya vizuri kwenye masomo yake

Kwa upande wa shule yetu Rafiki angu asingeweza kupitwa na mtihani kisa usingizi yni mpaka leo tukiongea anamlaumu sana shangazi yake ila baba ake amemwachia Mungu mana katapeliwa na dada ake kabisaa
 
Tumekutana primary , ulisoma bukoba secondary , ukaenda Tabora boys then tukameet Dar es salaam ukiwa Muhimbili tukiwa chuo hakika tukarejesha urafiki wetu sana .

Najua hujui ila ww ni mtu ninayekukubali sana baada ya wazazi wangu , natamani kukuona hata leo niko mbali na wewe kwa mawasiliano mpaka sura ila jua kazi yangu ilifanya tupotezane .

Nakutafuta sana Don , kama upo hapa basi jua Ego bado sijakusahau nakumiss bro , sina namba yako wala ya mtu wa karibu yako ila jua sijawahi mpata rafiki mwingine kuliko wewe .

Nitafute doctor Don .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha mambo ya aldehyde na ketone aisee organic chemistry
Dah Rafiki wa kweli nilimpata tukiwa advance aisee
Nilienda ile shule lkn nikakuta Advance walomaliza f4 ple wanapendana sana ila ss wapya kma wanatudharau hivi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom