Taja rafiki ambaye alifariki dunia mapema sana na huwezi kumsahau!

jamaikatz

Member
Jul 11, 2023
51
132
Mtaje rafiki yako ambaye alifariki mapema sana na hutawahi kumsahau, naanza na mimi kaka yangu mtoto wa mama mdogo.

Rest in peace broh.
1708068102581.jpg
 
Mgololo primary school 2005
wewe mdada tulikuwa tunakata nyasi ukaniongezea nyingine ili nisiadhibiwe nilikuwa mgeni shuleni.

Wewe mdada uliwasimulia wenzio hadithi nzuri sana haijawah simuliwa pale kijijini ukasema utaimalizia jioni ukitoka mtoni.

Kumbe ndio ulikuwa unayafuata mauti yako. Sikukufahamu sana ila nitaendelea kuumia daima dumu!
 
So sad mkuu.....Mgololo primary Kuna Moja ya Masanja Jr. Pia So sad.
 
Sio marafiki but ni mabraza wa rafiki zetu. So ni mabraza zetu pia.
-Huyu alinizidi 3yrs, kipindi tuko likizo ya form 2 alikua anatupa madili ya ujenzi yeye hakufika seko. Baadae akahamia kwenye boda.. Kapiga boda kazalisha demu akamchukua wakawa mke na mme.
2016 naenda home likizo nashuka basi usiku saa 2 naambiwa kapata ajali saa 12 na kafariki. Aisee Niliumia sana hata msibani sikwenda tulikua majirani nyumba kama 5 apart.

-Huyu kafa 2020 akiwa na 27yrs Kisukali ndio kilimuondoa, hakuacha mke wala mtoto. Nyumba ya tatu toka home afu wadogo zake ndo rafiki zangu damdam. Niliumia sana maana bro alikua mtulivu abd peace japo alikua anajihusisha na KuRap
 
Jamila… nilipigiwa simu na mama yako mdogo kunipa taarifa as urafiki wetu ulivuka urafiki na ndugu zetu wote walifahamu.

Binti mwema, ulifariki ukiwa huyajui ya dunia zaidi ya swala na funga zako.

Nililia sana baada ya kuingia msibani nyumbani kwenu, mama yako aliponiona alilia mno akilitaja jina langu kwani nilikuwa rafiki yako kipenzi na ulimwambia hilo mara nyingi.

Till we meet again, I miss you Jatrat.
 
Wewe mtoto wa miaka minne au mitatu..
Kijiji cha Ndola Mwaya kyela mwaka 2018. Mlikuja kubembea ofisini basi ukabaki kupiga story na mimi. Wewe mtoto uliniambia kwenu kutali (mbali) kwao kupipi (jirani) .

Wewe mtoto mama ako alipokuja kukuchukua ulilia sana nikakununulia biskuti ukaenda.

Wewe mtoto nilipopita kwenu siku ya pili uliniita sikusikia ukakimbia ukaidaka baskeli ukanionesha babu yako na bibi yako. Nikasafiri likizo mwezi ukapita.

Siku ya kwanza niliyorudi mama yako mkubwa alinipa taarifa ya kifo chako. Umeondoka kwaajali ya maji mtoto mdogo sana wewe na umeniachia ndugu huku kijijini. Ningekuwepo ningekuzika.
 
Ulale salama ndugu yangu Barnabas A siku nakupigia kukujulia hi unaniambia nasikia sasa una mtoto basi njoo na wife mwezi wa 12 tumwone mwanetu tukapiga soga sana na kucheka mwezi wa 12 hata hukuuona nikaja kukuzika mwezi wa 11 kumbe ndio ulikuwa unaniaga joh! sitokusahau arawa hukuacha hata mtoto miaka24 tuu tutaonana blood.
 
Pole sana
 
Back
Top Bottom