Umewahi kuuziwa kiwanja ambacho kina mgogoro?

Ni hatari sana,huwa wanajimegea taratibu Tena bila hofu
Mwingine sehemu aliniletea pigo za kwamba huu sio mpaka halisi kwamba mpaka wake ni kwenye miti hiyo iliyoko mpakani wkt yeye mwenyewe aliuziwa kiwanja kikiwa na miti tayari mpakani na alieniuzia hapo akaniambia mipaka ni hii miti( miarobaini)

Aisee nikaona hapana huyu mnyiramba hanijui nikamwita alieniuzia, mtendaji wa kata, mwenyekiti wa mtaa na majirani, akaitwa na aliyemuuzia, tukamwita na huyo jamaa kwa surprise. Mpaka tuliunyoosha kiheshima japo alikuwa mtata mpaka Leo hanisemeshi ni mwaka wa 3
 
Jamaa yangu mmoja hivi mzaliwa wa Tanga Handeni aliuziwa eneo huko mapinga bagamoyo mwaka 2021 mwishoni baada ya mwezi tukaenda kutembelea kwa ajili ya kusafisha eneo tukakuta kunajamaa amesha anza ujenzi kwa madai ya yeye ni eneo lake ameuziwa mwaka 2018 na mtu huyohuyo aliyemuuzia jamaa yangu.

Tukamtafuta muuzaji akawa anatupiga chenga kila wakati ilibidi tuulizie anapoishi na tulifanikiwa kufika kwake bahati nzuri tukamkuta, tulimuuliza swali moja tu je mmiliki halali wa eneo ni nani ni yule aliyeanza ujenzi au huyu jamaa, muuzaji akawa anajibu kwa dharau na kusema kamalizaneni wenyewe yeye hayamuhusu hayo.

Ilibidi tutoe tamko mbele ya mke wake na watoto wake kuwa chochote kitakachotokea tusije kulaumiwa na tukampa siku saba ajitafakari na atupe majibu yaneyoeleweka pia atupatie eneo lengine, jamaa akapuuza siku saba zikapita hatukuiona simu yake wala ujumbe wowote.

Ilitubidi tusafiri hadi Liwale mkoa wa lindi kusini mwa Tanzania huwezi kuamini ndani ya siku 7 baada ta kuisha zile siku saba tulizo mpa yule jamaa alipofuka akawa haoni ghafra tu hazikupita siku nyingi jamaa akapata ajali na kukatwa miguu yote miwili wakatati anaenda hospitali kuhangaikia macho yake, hapo ndipo jamaa zake wakaanza kupiga simu na kubembeleza tumsamehe ili aweze hata kuona kwani anaishi kwa shida sana tulicho wajibu ni kuwa mmesha chelewa, jamaa mpaka leo bado ni kipofu asiyekuwa na miguu

Dhulma haifai.
BAADA YA YEYE KUWA KIPOFU ASIYEKUWA NA MIGUU,NYIE HIYO HELA MLIYOLIPIA KIWANJA ILIRUDI?

AU KIWANJA KILIRUDI?
 
Wema uliniponza kujifanya mama Huruma!
Ni mama mtu mzima alikua anajitolea pale ofisini,mume wake alikua mgonjwa mgonjwa Sana,siku moja akaniambia mume wake anatakiwa kufanyiwa Operation na hawana hela,wanauza eneo lao!!
Nikamuuliza mara tatu tatu akanithibitishia Halina mgogoro,tukafuata taratibu zote nikamlipa tukamalizana kudadadekiii🙁🙁🙁🙁
Kumbe eneo linamgogoro Tena na serikali miaka mingi tu wanasumbuana mahakamani!
Niliumia Sana,tukaanza kuhangaishana Sasa na Yule mama,hela yenyewe ya kunilipa Hana,akaishia kunibadilishia eneo tu baada ya kusumbuana Sana!!!!!
 
Migororo ya ardhi ni mibaya sana , mwaka 2016 nilinunua eneo sehem kulikuwa bado pori mji ndio unaelekea huko ss sikuweka mipaka vzuri nikazembea kwenda kuwa nakagua aisee majirani wakawa wanajimegea tu wanajiogeza kakabaki kembabaa.

2024 nimekuja kupauza kwa hasara nikawaacha waendelee na maisha yao bhn maana ilikuwa full stress nikisogea eneo lile
pole sana
 
Usinunue kiwanja kisicho na hatimiliki iliyorekodiwa na manispaa au serikali ya kijiji. Kwa mkoa wa Dar es salaam, lazima kiwe na hati ya wizara.
Hamna umiliki zaidi ya hapo.
 
tufanye uchawi haupo mkuu...

swali...

ni nini kilifanya mti mkavu uliokuwa umeanguka usimame tena huko tabora?

hili ni tukio halisi sijatunga.
mkuu... huo ni mti wa aina gani?na ulikua ni mti wenye umri gani? ni sababu gani zilifanya uanguke? ulikatwa? mizizi yake yote ilitoka ardhini? ulipita muda gani toka uanguke au kung'oka na hali ya hewa ilikuwaje? ni Tabora sehemu gani na ilikua mwaka gani ili nifuatilie.

Niliwahi kuambiwa Sumbawanga ni hatari kwa kuwa na wataalam wa kutuma radi, nilipofika huko vijijini na kuuliza swali hili na wao waliishia kuniambia hata wao wanasikia hivyo na ni vigumu kuwajua hao watu mpaka radi iue mtu ndio wataalam watakuambia aliyetuma ni nani😀
 
mkuu... huo ni mti wa aina gani?na ulikua ni mti wenye umri gani? ni sababu gani zilifanya uanguke? ulikatwa? mizizi yake yote ilitoka ardhini? ulipita muda gani toka uanguke au kung'oka na hali ya hewa ilikuwaje? ni Tabora sehemu gani na ilikua mwaka gani ili nifuatilie.

Niliwahi kuambiwa Sumbawanga ni hatari kwa kuwa na wataalam wa kutuma radi, nilipofika huko vijijini na kuuliza swali hili na wao waliishia kuniambia hata wao wanasikia hivyo na ni vigumu kuwajua hao watu mpaka radi iue mtu ndio wataalam watakuambia aliyetuma ni nani😀
 
Jamaa yangu mmoja hivi mzaliwa wa Tanga Handeni aliuziwa eneo huko mapinga bagamoyo mwaka 2021 mwishoni baada ya mwezi tukaenda kutembelea kwa ajili ya kusafisha eneo tukakuta kunajamaa amesha anza ujenzi kwa madai ya yeye ni eneo lake ameuziwa mwaka 2018 na mtu huyohuyo aliyemuuzia jamaa yangu.

Tukamtafuta muuzaji akawa anatupiga chenga kila wakati ilibidi tuulizie anapoishi na tulifanikiwa kufika kwake bahati nzuri tukamkuta, tulimuuliza swali moja tu je mmiliki halali wa eneo ni nani ni yule aliyeanza ujenzi au huyu jamaa, muuzaji akawa anajibu kwa dharau na kusema kamalizaneni wenyewe yeye hayamuhusu hayo.

Ilibidi tutoe tamko mbele ya mke wake na watoto wake kuwa chochote kitakachotokea tusije kulaumiwa na tukampa siku saba ajitafakari na atupe majibu yaneyoeleweka pia atupatie eneo lengine, jamaa akapuuza siku saba zikapita hatukuiona simu yake wala ujumbe wowote.

Ilitubidi tusafiri hadi Liwale mkoa wa lindi kusini mwa Tanzania huwezi kuamini ndani ya siku 7 baada ta kuisha zile siku saba tulizo mpa yule jamaa alipofuka akawa haoni ghafra tu hazikupita siku nyingi jamaa akapata ajali na kukatwa miguu yote miwili wakatati anaenda hospitali kuhangaikia macho yake, hapo ndipo jamaa zake wakaanza kupiga simu na kubembeleza tumsamehe ili aweze hata kuona kwani anaishi kwa shida sana tulicho wajibu ni kuwa mmesha chelewa, jamaa mpaka leo bado ni kipofu asiyekuwa na miguu

Dhulma haifai.
Kiongozi umesahau kuweka namba wateja tukutafute 😹
 
Kuna mtu alisogeza mpaka kama huyo jirani yako. akajenga nyumba, hayo mauza uza aliyokuwa anayapata alitamani kukimbia nyumba.

Akaleta wataalam wakamwambia kumbe kipande kidogo alichomega kwa jirani kilikuwa namaagano. yan kiwanja cha jirani kilikuwa kinalindwa na maagano sasa kitendo cha yeye kuhamishia sehemu kwake lazima asumbuke.
Dhuluma sio nzuri.
Pacha Lamomy uki nidhulumu ujue naku nyongea ndumu😅😂
 
Back
Top Bottom