Jamaa yangu mmoja hivi mzaliwa wa Tanga Handeni aliuziwa eneo huko mapinga bagamoyo mwaka 2021 mwishoni baada ya mwezi tukaenda kutembelea kwa ajili ya kusafisha eneo tukakuta kunajamaa amesha anza ujenzi kwa madai ya yeye ni eneo lake ameuziwa mwaka 2018 na mtu huyohuyo aliyemuuzia jamaa yangu.
Tukamtafuta muuzaji akawa anatupiga chenga kila wakati ilibidi tuulizie anapoishi na tulifanikiwa kufika kwake bahati nzuri tukamkuta, tulimuuliza swali moja tu je mmiliki halali wa eneo ni nani ni yule aliyeanza ujenzi au huyu jamaa, muuzaji akawa anajibu kwa dharau na kusema kamalizaneni wenyewe yeye hayamuhusu hayo.
Ilibidi tutoe tamko mbele ya mke wake na watoto wake kuwa chochote kitakachotokea tusije kulaumiwa na tukampa siku saba ajitafakari na atupe majibu yaneyoeleweka pia atupatie eneo lengine, jamaa akapuuza siku saba zikapita hatukuiona simu yake wala ujumbe wowote.
Ilitubidi tusafiri hadi Liwale mkoa wa lindi kusini mwa Tanzania huwezi kuamini ndani ya siku 7 baada ta kuisha zile siku saba tulizo mpa yule jamaa alipofuka akawa haoni ghafra tu hazikupita siku nyingi jamaa akapata ajali na kukatwa miguu yote miwili wakatati anaenda hospitali kuhangaikia macho yake, hapo ndipo jamaa zake wakaanza kupiga simu na kubembeleza tumsamehe ili aweze hata kuona kwani anaishi kwa shida sana tulicho wajibu ni kuwa mmesha chelewa, jamaa mpaka leo bado ni kipofu asiyekuwa na miguu
Dhulma haifai.