Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

Salamu napokea vema japo Kuna wengine naona too much jamani unakuta mtu ni mumama kabisa nae ananambia shkamoo 🤔
Hahaha...........hizo shikamoo we zipokee tu, hazina shida

Ila kama una mwili mnene mnene, anza kuupunguza kwa tizi

Kama huna kiingilio cha gym, tuarike Wazee tulipe namba 🤪
 
ni kweli kbs lakn misiba ya vijana huwa inamasikitiko sana tofauti wa wazee kifo kwa kijana ni kama emergenc marehemu mwenyew humkuta akiwa hata hana habari tofauti na wazee ambao akiri yao hujiwewa tayari kwa lolote
Ni kweli mkuu
Kifo cha uzeeni kinategemewa ila kijana so sad😔
 
Mi hata miaka 30 tu nlikua sitamani kufika achilia kuzeeka......

Yani sahivi nawaelewa wanaokataaga umri na wengine kuficha, kuna muda nkiwaza tu umri wangu nachoka mie
Mtu unakuta ka ng'ang'ania miaka 30 bongo movie hao

Yaani nimeanza kuawaona mimi ni mdogo nawakuta hapo hapo 😅😅🙌🏼
 
Maisha mazuri ni yale kabla hatujakuwa na fikra hizi tulizonazo,utoto yani...Uzee sio kitu cha kutamani,ukiangalia mfumo wa maisha na muda basi sidhani kama ingekuwa ni chaguo letu tungekubali kuwa duniani.
Aiseee ukubwa unakuja na mzigo
 
Mbona mna tutamanisha dear😊
Enjoy mamaa🔥🔥

Karibu ukiingia hapa utaelewa
Hongera sana 🤗

Aisee wengine skincare sio vitu vyao ni kama wewe hapo ukitumia unaona unabadili asili yako

kabisa yaani
Wengine pia naona hua hawana mvi sana labda wazeeke sana

Alooo walikuelewa?
Naamini hawawezi kufanya hivyo
Nikisema hivyo huwa naambiwa nimeanza kulewa.. naamini huko mbeleni watakuja kunielewa
 
36 -37 hivi - miaka ya raha sana hiyo, nina sababu nyingi sana za kutamani kurudi hapo!

Vimvi vimeanza ila nikienda kusuka nawaambia wavichomoe maana vimeanzia katikati ya kichwa 😂😂😂

Kupunguza uzito, kunywa maji sana, kula high fiber food na balanced diet kwa ujumla, gym mara 2 kwa wiki kumantain healthy muscles.

Kuzeeka hakukwepeki, tunasogeza muda tu maana inside bado we feel young.

Hapana nisingechagua, nikifikisha 70 nikavuta 🪦nitashukuru, sitaki kutembelea mkongojo!

Tumekaribia 😅
Mwadela ngikuru
 
Nimewahi kutamani kuwa mkubwa, Nilikuwa nikiwaona mama zangu wadogo natamani kweli, nadhani walikuwa around 27, baadae nilivyofikisha miaka 27 nikiwaona wadada wa miaka 36 natamani kweli nawaona wazuri wanavaa urembo halafu wamejipata, next nadhani natamani wamama wa miaka 42-45 (naona wameshasettle wana direction nzuri ya maisha) baada ya hapo sina uhakika kama ntatamani umri mwingine 😂😭😭

Watu walionizunguka wameni-inspire kukua, nilikuwaga najiuliza mtu unakuwa na hela yako kabisa umeitafuta mwenyewe, i was so excited.

Kufa ndio kitu sitaki hata kukisikia, niko kwenye denial kubwa na sijui cha kufanya 💔😂
 
Kuna mzee wa miaka 77 alisema kuwa yeye haogopi kufa kabisa
Kwani kama ni kufa ameisha kufa zaidi ya x100
Ndugu wengi wamekufa, wazazi wote na Ndugu zao wengi wamekufa, majirani wamekufa, marafiki wameondoka wengi, kwa hiyo siogopi kufa tena

Mimi ni miaka michache nitakuwa umri huo wala sitamani kurudi hata mwaka mmoja

Nashukuru Mungu sijawahi kupata shida na mda wote nilikuwa nakimbiza maisha na pia kutembea nchi nyingi na ni kumbukumbu zinazonifanya nizidi kupiga trainers 👟 na jeans yaani young at heart
Tuombe Mungu tuwe na afya njema ila maisha hayatabiriki
 
Kutamani kuwa forever young ni extremely selfish.

Yani unataka wewe tu ushikilie nafasi ya kuishi, wengine waishi wapi?

Ishi, zeeka, kufa, achia wengine nafasi ya kuishi.
Kuwa na akili nako ni mzigo mda mwingine maana ina geuka kuwa ego
 
Hayo si maoni, hizo ni facts za kisayansi.

Energy can neither be created nor destroyed.

In order for the energy trapped in your body to be released for others to use it, you need to grow old and die.

Ukitaka kuwa forever young unakuwa selfish kung'ang'ania kuishi.

Kitu cha muhimu ni kuishi maisha yenye maana hata kama yana mwisho.
Ila Kiranga bwana🤣🤣 kwamba akubaliane na hali kuwa kuzeeka na kufa tu sio
 
Back
Top Bottom