Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

39 na kuendelea huu umri mtamu sana
wakati niko early 30 nilianza kuogopa sana kuhusu uzee lakini kadri
ninavyoenda nagundua mambo mazuri zaidi.

Nikijiangalia kwenye kioo na umri wangu halisi ni vitu viwili tofauti, kiuhalisia mabadiliko yangu si makubwa sana, japo najiona mkubwa huwa nikikutana na watu wanaonifahamu huwa wananiuliza natumia nini au surgery.

skin care nilijaribu nikaona shida tu nimerudi kwenye kitu ambayo nilikuwa natumia.

nina mvi mbili upande wa kulia sasa sijui zitaongeza au la.

Staki uzee wa magonjwa nilishakataa kabisa, na wanangu nilishawambia ikitokea nimepata ugonjwa au tatizo ambalo litahitaji uangalizi au usumbufu kwao basi waangalie namna ya kuniua! kama ni sindano wanichome nife
Naomba utengue kauli ya mwisho, tuzidi kuomba mwisho mwema.
 
Ipo hivyo kwa sababu sote tunajua kawaida umri unavyosonga ndio na mauti una ya karibia

Licha ya kua vijana nao hufa mapema
Kwahiyo mtu hua karibu na kifo chake mwenyewe kwa namna fulani ni vile huwezi kujua tu
ni kweli kbs lakn misiba ya vijana huwa inamasikitiko sana tofauti wa wazee kifo kwa kijana ni kama emergenc marehemu mwenyew humkuta akiwa hata hana habari tofauti na wazee ambao akiri yao hujiwewa tayari kwa lolote
 
Mda wa kuishi mwanadamu ni mchache sana.

Nakumbuka jana tu nilikua a boy with a lot of dreams, nikifikiri nina muda mwingi wa kufanya kila kitu.

But in the blink of an eye I'm left with just 3 years before stepping into the 4th floor of life and sometimes I wonder where all the time went.


Mda unaenda, unapoteza company, real connections zinapotea, watu unaowazoea wanakua strangers.

Mwisho wa siku unatakiwa ubaki wewe kama wewe.

Kuna kipindi unafika una realize kwamba not everyone you started with will be there until the end.


Na kuna siku itafika watoto wako watakua, watajitegemea, wataanzisha maisha yao na kuondoka nyumbani kufuata dreams zao.

Then tabaki wewe kama wewe, kwenye nyumba ambayo zamani ilikua na sauti za watu unaowapenda, lakini sasa imebaki silence na memories za maisha uliyowahi kuishi.


Na kuna mda mpaka nnawaza kwamba soon tu ntakuwa sipo kwenye hii dunia 😄.

Tuache majivuno jamani... we all gonna die
Para ya mwisho waambie maccm, maana yanajikutaga kama yataishi milele.
 
Kisaikolojia, watu wengi hawataki kuzeeka kwa sababu kuzeeka kunawakumbusha kuhusu kupoteza ujana, mabadiliko ya maisha na hatimaye kifo. Hata hivyo, si kila mtu anaogopa kuzeeka kwa kiwango sawa. Wengine hukubali uzee kwa amani, huku wengine wakihangaika sana kuuficha.

Hizi ndio sababu kuu za kisaikolojia.
1. 🧠 Hofu ya kifo (Fear of Death)
Hii ni mojawapo ya sababu kubwa zinazoweza kufanya watu waogope kuzeeka.
Mtu anapoona nywele zikibadilika rangi, ngozi ikianza kuwa na mikunjo au mwili ukipoteza nguvu, anaweza kuanza kutambua kwamba maisha yana kikomo.
Kisaikolojia, baadhi ya watu huona kuzeeka kama ishara kwamba wanakaribia mwisho wa maisha yao. Hali hii inaweza kuwafanya watamani kubaki vijana milele.
Mfano: Mtu anayetimiza miaka 50 anaweza kuanza kujiuliza, "Je, nimeishi maisha niliyotaka? Nina muda gani uliobaki wa kutimiza ndoto zangu?"

2. Kupoteza mvuto wa kimwili
Jamii nyingi huusifu ujana kwa kuhusisha na uzuri, nguvu na mvuto wa kimapenzi.
Kwa hiyo, baadhi ya watu huamini kwamba wanapozeeka, watapoteza uzuri wao na kuvutia watu wachache.
Hali hii inaweza kuwafanya:
Watumie pesa nyingi kuficha dalili za uzee.
Waogope mikunjo ya ngozi na mabadiliko ya mwili.
Wajilinganishe na watu vijana.
Wajisikie hawavutii tena.
Hata hivyo, kuzeeka hakumaanishi kupoteza uzuri au uwezo wa kuvutia watu. Tatizo linaweza kuwa namna mtu anavyouhusisha mwonekano wake na thamani yake binafsi.
3. Hofu ya kupoteza thamani katika jamii
Baadhi ya watu huamini kwamba thamani yao inategemea ujana, nguvu, fedha au mafanikio yao.
Wanapozeeka, wanaweza kuogopa kwamba jamii haitawaheshimu tena au haitawapa nafasi kama zamani.
Kwa mfano, mtu anaweza kujiuliza:
Je, watu bado wataniheshimu?
Je, bado nitakuwa muhimu kazini?
Je, vijana wataniona kuwa mtu wa maana?
Hofu hii inaweza kuwa kubwa zaidi kwa mtu ambaye amejenga utambulisho wake katika mafanikio na uwezo wa kufanya mambo ambayo wengine hawawezi.
4. Majuto kuhusu maisha yaliyopita
Watu wengine hawaogopi uzee wenyewe. Wanaogopa kutambua kwamba muda umepita bila wao kufanya mambo waliyotamani.
Mtu anapofikisha miaka 40, 50 au 60, anaweza kuanza kutathmini maisha yake.
Anaweza kufikiria kuhusu:
Ndoto ambazo hakuzitimiza.
Fursa alizopoteza.
Mahusiano yaliyovunjika.
Muda aliotumia kufanya mambo ambayo hayakuwa na maana kwake.
Hapo, kuzeeka kunakuwa kama kioo kinachomkumbusha kuhusu muda aliopoteza.
Wengine huanza kutamani kurudi ujana ili wapate nafasi nyingine ya kufanya maamuzi tofauti.
5. Hofu ya kupoteza uwezo wa mwili
Uzee unaweza kuambatana na kupungua kwa nguvu za mwili, mabadiliko ya afya na wakati mwingine utegemezi kwa watu wengine.
Kwa mtu anayethamini sana uhuru wake, wazo la kushindwa kujihudumia linaweza kuleta hofu kubwa.
Anaweza kuogopa:
Kushindwa kufanya kazi alizokuwa akizifanya.
Kutegemea watoto au ndugu.
Kupoteza uwezo wa kufanya maamuzi kwa uhuru.
Kushindwa kushiriki katika shughuli anazozipenda.
Kwa hiyo, wakati mwingine mtu hapambani na uzee wenyewe, bali anapambana na mambo anayohofia kwamba uzee utamnyang'anya.
6. Shinikizo la mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii inaweza kuongeza hofu ya kuzeeka kwa kuonyesha picha za watu wenye miili inayovutia, ngozi laini na maisha yanayoonekana kuwa makamilifu.
Mtu anapojilinganisha na picha hizo mara kwa mara, anaweza kuanza kuona mabadiliko ya kawaida ya mwili wake kama kasoro.
Matokeo yake, anaweza kuamini kwamba ili akubalike, lazima aendelee kuonekana kijana.
Tatizo ni kwamba mara nyingi tunajilinganisha na picha zilizochaguliwa kwa uangalifu, zilizohaririwa au zinazoonyesha upande mmoja tu wa maisha ya mtu.
7. Kutaka kudhibiti maisha
Kuna watu ambao hawapendi jambo lolote linalowafanya wajisikie hawana udhibiti.
Wanaweza kudhibiti chakula wanachokula, mazoezi wanayofanya, mavazi yao na namna wanavyoonekana. Lakini hawawezi kuzuia kabisa kupita kwa muda.
Hapo ndipo mgongano wa kisaikolojia unapotokea.
Mtu anaposhindwa kudhibiti jambo analolipa umuhimu mkubwa, anaweza kutumia nguvu nyingi zaidi kujaribu kulidhibiti.
Ndiyo maana baadhi ya watu hutumia muda mwingi na fedha nyingi kupambana na dalili za uzee.
Hata hivyo, kujitunza si tatizo. Changamoto huanza pale hofu ya kuzeeka inapokuwa kubwa kiasi cha kuathiri furaha, mahusiano au maisha ya kila siku.
8. Kisaikolojia, ni watu wa aina gani wanaoweza kuogopa kuzeeka zaidi?
Si rahisi kuwagawa watu katika makundi maalumu, lakini tabia na mazingira fulani yanaweza kuchangia hofu hiyo.
A. Mtu anayepima thamani yake kwa mwonekano
Ikiwa mtu anaamini kwamba thamani yake inategemea uzuri wa uso au umbo la mwili, mabadiliko ya uzee yanaweza kumuumiza kihisia.
B. Mtu anayehitaji sana kuthaminiwa na wengine
Mtu anayehitaji uthibitisho wa mara kwa mara kwamba anavutia, ana nguvu au ni bora anaweza kuogopa kupoteza sifa hizo kadiri anavyozeeka.
C. Mtu anayejuta kuhusu maisha yake
Mtu asiye na furaha na maisha aliyoyaishi anaweza kuuona uzee kama ukumbusho wa fursa zinazopungua.
D. Mtu anayehusisha ujana na furaha
Ikiwa mtu anaamini kwamba furaha, mapenzi na mafanikio vinapatikana zaidi wakati wa ujana, anaweza kuhisi kwamba maisha yake yatapoteza maana anapozeeka.
Lakini kumbuka: haya ni maelezo yanayowezekana, si sheria zinazotumika kwa kila mtu.
9. Je, kutotaka kuzeeka kunaonyesha udhaifu wa kisaikolojia?
Hapana.
Ni jambo la kawaida kutaka kubaki na afya njema, nguvu za mwili na mwonekano unaoupenda. Pia, ni kawaida kuhuzunika unapogundua kwamba mwili wako unabadilika.
Jambo muhimu ni kutofautisha kati ya kutaka kubaki kijana na kushindwa kukubali kwamba unaendelea kuzeeka.
Mtu anaweza kujitunza, kufanya mazoezi na kuonekana vizuri huku akikubali mabadiliko ya maisha.
Lakini ikiwa hofu hiyo inamfanya ajichukie, aepuke watu, atumie fedha kupita uwezo wake au ashindwe kufurahia maisha, anaweza kunufaika kwa kuzungumza na mtaalamu wa afya ya akili.
10. Ukweli wa ndani zaidi: Watu wengine hawataki kuzeeka kwa sababu hawataki kupoteza utambulisho wao
Fikiria mtu ambaye maisha yake yote amejulikana kwa kuwa kijana mwenye nguvu, mwenye mvuto na anayependwa na watu.
Miaka inapopita, anaanza kuona mabadiliko katika mwili wake na namna watu wanavyomchukulia.
Anaweza kuhisi kana kwamba anapoteza sehemu ya yeye mwenyewe.
Kwa hiyo, anaposema, "Sitaki kuzeeka," huenda anamaanisha:
Sitaki kupoteza mvuto wangu.
Sitaki kusahaulika.
Sitaki kuhisi kwamba maisha yangu bora yamepita.
Sitaki kuwa mtu asiye na umuhimu kwa wengine.
Sitaki kukabiliana na ukweli kwamba siwezi kurudisha muda.
Hapa kuna jambo muhimu sana: Wakati mwingine mtu haogopi idadi ya miaka aliyoishi; anaogopa maana anayoiweka katika miaka hiyo.
Swali la kutafakari
Nikuulize jambo moja la kisaikolojia:
Unapomwona mtu ambaye hataki kabisa kuzeeka, anakataa kukubali umri wake na anajitahidi sana kuonekana kijana, unadhani anajaribu kuficha nini zaidi?
Hofu ya kifo — anajua muda unapita na anaogopa mwisho wa maisha.
Hofu ya kupoteza mvuto — anaamini kwamba akizeeka, hatavutia tena.
Hofu ya kupoteza thamani — anaogopa kutoheshimiwa au kutohitajika tena.
Majuto ya maisha — anahisi kwamba muda umepita bila kutimiza mambo aliyotaka.

NB:nime edit kwa hisani ya akili mnemba
MUNGU atujalie mwisho mwema
 
FOREVER YOUNG 🥹

Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

Mimi natamani forever niwe young

Lakini je ni kwamba tunaogopa kuzeeka au tunaogopa kua wa dhaifu kutokana na uzee ?

Kipindi cha nyuma nilikuwa najiona mtoto au kijana, lakini sasa naanza kutambua kwamba siku za mbele, uhai ukiwepo, nitakuwa mzee

Na fikiria kama nikiwa mzee nitakua na nguvu kweli au itabidi nisaidiwe baadhi ya mambo ambayo kwa sasa nayamudu mwenyewe bila kuitaji msaada

Zamani nikiona mtu ana miaka 30 nilihisi ni mtu aliyezaliwa zamani sana
Leo hii nimebakiza ngazi chache kuingia floor ya 3, yaani miaka 30!
Nafikiria muda umekimbia hivi lini?

Hivi tunatamani kua young forever
Au tunauhofia uzee na kashkash zake😢

Maana uzee unakuja na mengi
Sote tunaona kijana na mzee wanatofautiana vingi sana

Ukiwa mzee na kama hukua mtu wa kuzingatia mazoezi na chakula cha afya enzi za ujana wako uzee unakua ni mateso

Haya hapa ni miongoni mwa magonjwa yanayoweza kuwapata wazee

Na haina maana vijana hayawapati magonjwa haya

Na pia sio kila mzee hupata haya magonjwa
👇

Presha, kisukari, magonjwa ya moyo, Tezi dume kwa wanaume
maumivu ya viungoo, udhaifu wa mifupa matatizo ya kuona na kusikia pamoja na matatizo ya kumbukumbu


Kwenye mjadala👇

1. Kama ungepewa nafasi ya kubaki na umri mmoja milele, ungechagua miaka mingapi, na kwa nini?

2. Unajisikiaje unapojiangalia kwenye kioo na kuona mabadiliko ya umri?
Mvi zikianza kuota, utazikubali (Unazikubali )au utapambana nazo kwa Super Black na kunyoa upara?

3. Unafanya nini ili kudumisha muonekano na afya yako?
Gym, skincare, kula vizuri ?

4. Unaogopa kuzeeka kwa sababu ya kupoteza ujana na nguvu, au unaona ni sehemu ya kawaida ya maisha?

5. Kama ungekuwa na option ya kubaki kijana milele ungechagua kutokuzeeka?


Karibuni Great Thinkers🤗

ShesRise_1 ✋️
Sitaki kuwa kijana milele na wala sitaki kuwa mzee, Lakini kama itakuwa ni kwa mapenzi ya MUNGU basi yatimizwe.
 
39 na kuendelea huu umri mtamu sana
wakati niko early 30 nilianza kuogopa sana kuhusu uzee lakini kadri
ninavyoenda nagundua mambo mazuri zaidi.
Mbona mna tutamanisha dear😊
Enjoy mamaa🔥🔥
Nikijiangalia kwenye kioo na umri wangu halisi ni vitu viwili tofauti, kiuhalisia mabadiliko yangu si makubwa sana, japo najiona mkubwa huwa nikikutana na watu wanaonifahamu huwa wananiuliza natumia nini au surgery.
Hongera sana 🤗
skin care nilijaribu nikaona shida tu nimerudi kwenye kitu ambayo nilikuwa natumia.
Aisee wengine skincare sio vitu vyao ni kama wewe hapo ukitumia unaona unabadili asili yako
nina mvi mbili upande wa kulia sasa sijui zitaongeza au la.
Wengine pia naona hua hawana mvi sana labda wazeeke sana
Staki uzee wa magonjwa nilishakataa kabisa, na wanangu nilishawambia ikitokea nimepata ugonjwa au tatizo ambalo litahitaji uangalizi au usumbufu kwao basi waangalie namna ya kuniua! kama ni sindano wanichome nife
Alooo walikuelewa?
Naamini hawawezi kufanya hivyo
 
Mda wa kuishi mwanadamu ni mchache sana.

Nakumbuka jana tu nilikua a boy with a lot of dreams, nikifikiri nina muda mwingi wa kufanya kila kitu.

But in the blink of an eye I'm left with just 3 years before stepping into the 4th floor of life and sometimes I wonder where all the time went.


Mda unaenda, unapoteza company, real connections zinapotea, watu unaowazoea wanakua strangers.

Mwisho wa siku unatakiwa ubaki wewe kama wewe.

Kuna kipindi unafika una realize kwamba not everyone you started with will be there until the end.


Na kuna siku itafika watoto wako watakua, watajitegemea, wataanzisha maisha yao na kuondoka nyumbani kufuata dreams zao.

Then tabaki wewe kama wewe, kwenye nyumba ambayo zamani ilikua na sauti za watu unaowapenda, lakini sasa imebaki silence na memories za maisha uliyowahi kuishi.


Na kuna mda mpaka nnawaza kwamba soon tu ntakuwa sipo kwenye hii dunia 😄.

Tuache majivuno jamani... we all gonna die
Tuache majivuno jamani... we all gonna die pin 📌
 
Tuliza komwe Eve, uzee unakuja tena kwa uhakika sana! Furahia kila umri ulionao na wala usijifiche kwa umri wako.
Ndiyo maana tukipata nafasi ya kuongea na vijana, huwa tunawakumbusha kujiandaa na Uzee

Uzee unamfikia Kila mmoja kwa wakati wake.

Muhimu kujiandaa nao tu.

Ukizeeka bila hela, ndiyo mwanzo wa kuitwa yule Babu mchawi, ama yule Bibi mchawi 🙌
 
Back
Top Bottom