Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

FOREVER YOUNG 🥹

Umewahi kutamani usizeeke, yaani forever uwe young?

Mimi natamani forever niwe young

Lakini je ni kwamba tunaogopa kuzeeka au tunaogopa kua wa dhaifu kutokana na uzee ?

Kipindi cha nyuma nilikuwa najiona mtoto au kijana, lakini sasa naanza kutambua kwamba siku za mbele, uhai ukiwepo, nitakuwa mzee

Na fikiria kama nikiwa mzee nitakua na nguvu kweli au itabidi nisaidiwe baadhi ya mambo ambayo kwa sasa nayamudu mwenyewe bila kuitaji msaada

Zamani nikiona mtu ana miaka 30 nilihisi ni mtu aliyezaliwa zamani sana
Leo hii nimebakiza ngazi chache kuingia floor ya 3, yaani miaka 30!
Nafikiria muda umekimbia hivi lini?

Hivi tunatamani kua young forever
Au tunauhofia uzee na kashkash zake😢

Maana uzee unakuja na mengi
Sote tunaona kijana na mzee wanatofautiana vingi sana

Ukiwa mzee na kama hukua mtu wa kuzingatia mazoezi na chakula cha afya enzi za ujana wako uzee unakua ni mateso

Haya hapa ni miongoni mwa magonjwa yanayoweza kuwapata wazee

Na haina maana vijana hayawapati magonjwa haya

Na pia sio kila mzee hupata haya magonjwa
👇

Presha, kisukari, magonjwa ya moyo, Tezi dume kwa wanaume
maumivu ya viungoo, udhaifu wa mifupa matatizo ya kuona na kusikia pamoja na matatizo ya kumbukumbu

Kwenye mjadala👇

1. Kama ungepewa nafasi ya kubaki na umri mmoja milele, ungechagua miaka mingapi, na kwa nini?

2. Unajisikiaje unapojiangalia kwenye kioo na kuona mabadiliko ya umri?
Mvi zikianza kuota, utazikubali (Unazikubali )au utapambana nazo kwa Super Black na kunyoa upara?

3. Unafanya nini ili kudumisha muonekano na afya yako?
Gym, skincare, kula vizuri ?

4. Unaogopa kuzeeka kwa sababu ya kupoteza ujana na nguvu, au unaona ni sehemu ya kawaida ya maisha?

5. Kama ungekuwa na option ya kubaki kijana milele ungechagua kutokuzeeka?

Karibuni Great Thinkers🤗

ShesRise_1 ✋️
Mdogo wangu ShesRise_1 hii mada sikuiona kabisa, halafu ipo toka juzi kwanini hukuni tag ?

Kimsingi 🤔

Mimi sijawahi kutamani hilo jambo, kwa sababu viumbe hai tuna sifa saba za msingi, ikiwemo Movement, Respiration, Growth, Reproduction, Excretion, Nutrition na Sensitivity

Sasa, kama nitqtamani nisizeeke kabisa, wakati Growth ni mojawapo ya sifa za viumbe hai, nitakuwa kiumbe hai kweli au nitakuwa nimeanza kuishi nje ya mfumo wa biolojia? 😂😂

Halafu, ukitamani kubaki palepale maisha yako yote, si utakuwa OLD FASHIONED wakati dunia yenyewe inabadilika kila siku? 🤣

Kuna mambo mengine kuyatamani ni zaidi ya tamaa, ni kama unataka kuomba ruhusa ya kubishana na Mungu kuhusu kanuni za uumbaji!

TUKUBALI TU TUZEEKE LAKINI UZEE WETU UWE NA MWISHO MZURI KAMA MZEE WARIOBA, BABA WA TAIFA JK NYERERE etc
 
Kaka huja ni follow kwani?

Kwani unadhani hii mifumo ingekua kinyume na ilivyo sasa dunia ingekuwa mbaya ?

Ni kwa vile tumezoea mifuno iliyopo
Lakini kama kungekuwa na mfumo mwingine basi tungezoea huo mfumo kama tulivyozoea huu wa sasa

Old fashioned? kwamba kadri unavyozeeka ndio unaenda na fashione labda kama sielewi mie

Kuingiza swala la Mungu hapa ni kutaka kuhamisha mjadala
TUKUBALI TU TUZEEKE LAKINI UZEE WETU UWE NA MWISHO MZURI KAMA MZEE WARIOBA, BABA WA TAIFA JK NYERERE etc
Shukran sana bro
 
Kaka huja ni follow kwani?

Kwani unadhani hii mifumo ingekua kinyume na ilivyo sasa dunia ingekuwa mbaya ?

Ni kwa vile tumezoea mifuno iliyopo
Lakini kama kungekuwa na mfumo mwingine basi tungezoea huo mfumo kama tulivyozoea huu wa sasa
Daaah 😂, Sasa hapo umehamisha mjadala kutoka kwenye biolojia kwenda kwenye falsafa ya mazoea ya binadamu
Nakubaliana nawewe kwamba binadamu huzoea mazingira na mifumo wanayoishi ndani yake lakini kuzoea mfumo fulani hakumaanishi kwamba kanuni za asili zinazotawala mfumo huo zinabadilika kwa sababu tu tumeuzoea. Kumbuka mifumo inaweza ikabadilika lakin kanuni za asili haziwezi kubadilika.

Kwa mfano unaweza ukala mikate daily lakini chooni utaenda tu ?
 
Tokea hapo mada ilikua ya falsafa
Nakubaliana nawewe kwamba binadamu huzoea mazingira na mifumo wanayoishi ndani yake lakini kuzoea mfumo fulani hakumaanishi kwamba kanuni za asili zinazotawala mfumo huo zinabadilika kwa sababu tu tumeuzoea. Kumbuka mifumo inaweza ikabadilika lakin kanuni za asili haziwezi kubadilika.
Nilimaanisha kama asili ingeumbwa vingine tofauti na ilivyo ingezoeleka tu
Kwa mfano unaweza ukala mikate daily lakini chooni utaenda tu ?
Hii mifano hata sielewi bro
 
Old fashioned? kwamba kadri unavyozeeka ndio unaenda na fashione labda kama sielewi mie
😂😂 Sijamaanisha kwamba kadri unavyozeeka ndivyo unavyoendana na fashion! Nimetumia Old fashioned kumaanisha kitu kilichobaki katika hali ileile wakati mazingira yanabadilika

Angalia fashion yenyewe leo unavaa size M, miaka inaenda baadaye unavaa XL! 🤣 Mwili nao unapitia mabadiliko, kutoka utoto hadi ujana na uzee.

Sasa fikiria dunia inabadilika kila siku, lakini wewe unabaki vilevile milele (FOREVER YOUNG)Si utakuwa bidhaa ya zamani kwenye soko la viumbe hai? 😂😂

Au ulikuwa unataka ubaki kama Mende 🪳 tu ? Kubali biology ichukue nafasi yake japo ni ngumu kumeza
 
Duh noma aisee naona lugha gongana mimi sidhani kama kutokuzeeka kuna tatizo aisee

Kwahiyo ukizeeka ndio unaendana na dunia?
 
Back
Top Bottom