Umewahi Kusoma kitabu hiki?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,888
20,076
Ninafikiria kununu kitabu hiki ila bei yake ni kubwa sana kuliko vitabu vya aina hiyo ambavyo huwa ninanunua. Bei yake inafikia karibu $200 wakati nimeshanunua na kusoma vitabu kama vya Mandela, Reagan, Churchill, Thatcher. Kenyatta, MLK, JFK, na vingine vingi vinavyohusu viongozi mbalimbali kwa bei isyozidi $20. Kama umeshakisoma, naomba unipe perspective yako kabla sijamwaga hela nyingi hivyo.

1597864061229.png
 
Ukiona bei ni kubwa ujue mlengwa sio wewe. Endelea kutafuta hela ya kula maisha yaende
Hilo siyo jibu na wala halikunisaidia; elewa kuwa sishindwi kulipa hizo hela ila nilikuwa najaribu kuangalia thamani ya kitabu na bei yake kwa vile hakina reviews zozote mtandaoni. Inawezekana kuna waliowahi kukisoma kupitia public Library na wanakijua; kama wewe hukijui, hukua na haja ya kujibu. Idadi ya vitabu nilivyo navyo sasa pamoja na vile vya kitaaluma vina thamani zaidi ya dola 35,000; vingine huwa navinunua hata kwa dola zaidi ya 350 na vingine huwa napata bure kwa kueletewa na publisher wake: ninajua thamani ya vitabu. na ungesoma vizuri ungejua kuwa niko tayari kumwaga hela hizo ila nilikuwa ninataka perspective ya mtu mwingine anayekijua vizuri.

Yaani kuna watanzania siku hizi wamepoteza kabisa chembe za busara katika mawasiliano; kila sehemu wanaona ni mahali pa kukejeliana na kutukanana tu.
 
Kiranga hiki haujasoma?
Hapana, hicho sijapata nafasi ya kukisoma.

Ila nimemaliza kukisoma cha Paul Bjerk "Julius Nyerere". Nikakipenda mpaka nikakitafuta kitabu chake kingine "Building_A_Peaceful_Nation-Julius_Nyerere_And_The_Establishment_Of_Sovereignty_In_Tanzania_1960-1964".

Nakiweka hapa kina historia nzuri sana.
 
Attachments

  • Building_A_Peaceful_Nation-Julius_Nyerere_And_The_Establishment_Of_Sovereignty_In_Tanzania_196...pdf
    10 MB · Views: 21
Hapana, hicho sijapata nafasi ya kukisoma.

Ila nimemaliza kukisoma cha Paul Bjerk "Julius Nyerere". Nikakipenda mpaka nikakitafuta kitabu chake kingine "Building_A_Peaceful_Nation-Julius_Nyerere_And_The_Establishment_Of_Sovereignty_In_Tanzania_1960-1964".

Nakiweka hapa kina historia nzuri sana.
Asante sana.
 
Thanks for sharing! Mimi kwa sehemu kubwa bado ni old school; kwa vitabu kama hivi uwa napenda kusoma ukurasa mmoja mmoja na pengine kupigia mistali point. Kwa hiyo huwa husoma zaidi vitabu vya makaratsi kuliko vitabu vya electrons.

Again! thanks for sharing; nitakisoma pole pole, nikishindwa nitatafuta cha makaratasi.
 
Hiki kitabu ni muhimu sana ukitaka kuielewa historia ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania. Ukikisoma utafaidi habari nyingi sana ambazo kwa sasa ama zimesahaulika, ama hazikujulikana.

Kuna mambo mengi sana kuhusu historia ya Tanzania nimejifunza kwenye kitabu hiki.
 
Back
Top Bottom