Nimkanye nani kati yangu na wewe? Ok nakukanya wewe!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Kwamiaka kadhaa, Tumejikusanya katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika majukwaa ya kisiasa, kiharakati na humu mitandaoni kutoka kila upande wa dunia. Tukiwa na mvuto wa Gandhi, Nyerere, Mandela, Churchill, Roosevelt, Nkrumah, Toure, Bandaranaike, Somoza, Lenin, Mao, Reagan, Gorbachev, Morales, Lula, Ghadafi, Seretse Khama, Kenyatta, Khamenei na kila mvuto, uwe ni wa kibepari, kijamaa, kijimaa, kikabaila hata leo kwenye soko huria.

Sisi kizazi chetu hakitwi cha mapinduzi ama cha ukombozi, Bali kizazi cha Mageuzi na kinaongozwa vizuri na Mbowe, Lissu, Bob Wine, Julius Malema nk na kwa Tanzania awali kiliongozwa na akina Mtei, Mrema, Lipumba kilionekana kitaiwezesha Tanzania iwe nchi yenye kufuata demokrasia ya kweli, bali utosi wa leo ni njugu 38 mwili mwa Lissu na Jela ya Freeman Mbowe hoja zao ni chukizo mbele ya wakombozi waliojigeuza miungu watu na kujenga daraja la watwana nchini.

Hebu angalia jinsi Kuhani na FMES, wanavyoweza kubanjuana makonzi kwenye hoja moja, kisha wakaelewana kwenye hoja nyingine, pumbaaavu, ndoto za kimweri zikafia Chato, mazishi Segerea, matanga Ubelgiji kuhani msiba ukonga. Ati tutawale bila bughudha, Muulize muumba wako kwanini jogoo la masika alitoa sadaka tule wakati kuna matetea tunasubiri ya tage?

Angalia tulivyogawanyika katika suala la Katiba Mpya, Demokrasia, Utawala wa sheria, Utu na haki, mfumo wa siasa, nk kila mmoja akifafanua upande wake na kuutetea. Yes kimeibuka kikundi cha wadwanzi kinashirikiana na watawala sasa wanadai TUME HURU, yes serikali inadai tume huru ya Uchaguzi, hutaki?hivi ndivyo taifa hukua, sio jogoo moja liwike utaraji mayai kwa matetea mia. Mitazamo tofauti ndio huzaa taifa imara, Nchi ya kauli na maagizo huzaa kizazi cha unafiki tena unafiki uliokomaa kama huu wa Jamhuri ya Mbanyawima.

Nakumbuka mfano wa jinsi gani Marekani ilivyoundwa na watu waliokuwa na "mitazamo" tofauti na bila kumiminiana risasi au kufungana katika viroba wala kutekana mithiri ya jamhuri ya wajinga, Marekani walikata shauri wakakaa chini wakajadili, wakawa na midahalo na mwishowe, wakazalisha Katiba moja ambayo inaiongoza nchi yao mpaka leo, Katiba hiyo ndio ikazaa taasisi imara ambazo haziingiliwi na mtawala yoyote miaka zaidi ya 200 sasa!

Kizazi hiki ilikuwa ni fursa yetu, katika kutumia nafasi hii ya mageuzi ya dunia, si kutengana na kuchukiana kwa kuwa hoja zetu zinapingana na kikundi kinachoamini kimebarikiwa kutawala Tanzania na uzao wao utakuwa wa kuzaa wagombea tu, huku sisi uzao wetu unabaki kuwa wa kuzaa wapiga kura tu, bali ni kufungamana na kuheshimu uhuru wetu wa maoni unaolindwa na katiba yetu, na kuidumisha Demokrasia inayoturuhusu kusikilizana na kubishana, huku tukinywa maji kwenye kisima kimoja na kukaa kwenye mkeka mmoja tukila chakula pamoja.

Tumeruhusu wahalifu waliojipa jukumu la kuwaza na kuamua juu yetu leo wanaamini, nasi tumeamini wao ndio wenye kustahili kuamua kesho yetu, ndio sisi wanafiki lazima tuishi kinafiki njia ya choo isiote nyasi. Hawa ni wale wenye kudai Tanzania ina wenyewe, kwamba hakuna mwingine kama wao, na wengine mkitoa maoni au mkihoji au kukosoa ama kushauri tu, watatumia mikono na nyenzo zao kuwashughulikia hadi msahaulike. Me

Mwanafalsafa Socrates alisema "The Unexamined life is not worth living", je sisi nasi tukubali kupokea ya Wazazi wetu ambao mpaka leo wanakataa kufanya tathmini ya kweli ya walichofanya na hata kukiri pale walipokosea?.

Ngoja nikurudishe nyuma, leo ufahamu unafiki wa Taifa hili ulianza lini, Tunasema haya ili kujitibu si ili kujitweza. Mwaka 1961-63 yaani miaka mitatu ya baada ya Uhuru taifa la Tanganyika halikuwa na unafiki, yaani lilikuwa na msimamo mmoja wa kiitikati na kifalsafa tukiwa ni Taifa la KIBEPARI kwa 💯. Rafiki mkubwa wa Tanganyika alikuwa ni Marekani chini ya JF Kennedy.

Mwaka 1963 baada ya kuuawa kwa Rais wa Marekani JF Kenned, ndipo unafiki wa taifa ulipozaliwa, Nyerere akiwa ndie baba wa taifa hili. Wajamaa wakamchombeza Mwalimu kwamba sasa tafuta mundo mpya wa kuongoza nchi, ukiendelea hivyo kuwaamini "mabeberu" watakuwa wanakuongoza kutoka Washington na London, yaani utakuwa umepata uhuru wa bendera tu.

Wajamaa hawa wakiongozwa na Mao wakafanikiwa, Nyerere akaingia upepo mkubwa akaanza kukaa mbali na USA na Uingereza, na hata lilipotokea tukio la uasi 1964, nikwamba alizidiwa tu ndipo wasaidizi wakamwambia oya ooohoo utaondoka kweli, muombe Malkia msaada wa jeshi akusaidie, ndipo Uingereza ikatuma kikosi cha makomandoo kuja kuzima uasi ule kutoka Colito Lugalo na Tabora

Miezi kadhaa tu baada ya Uingereza kuzima uasi ule, ni Nyerere yuleyule akawambia waondoke Waingereza na badala yake Jeshi la Nigeria likashika nafasi ya doria Tanzania kuhakikisha hakuna uasi tena zaidi ya mwaka mmoja.

Marekani na Uingereza wakaja nao na propaganda kwamba Nyerere ukiwa na Warusi/Wachina utapinduliwa sasahivi, unaona wenzio wanavyopinduliwa huko Afrika Magharibi? Basi na bajeti yako kamwe hatutasaidia.

Ilikuwa ni kazi ya Nyerere kuchekecha, ama awe kulia au kushoto, Nyerere na moja ya vinchi vingine hasa vile vinavyotembeza bakuli sana duniani, wakaja na jibu kuwa wao ni nchi isiyofungamana na upande wowote... Yaani Urusi/Uchina hawapo, USA/UK hawapo... Huu ulikuwa ndio UNAFIKI WA AWALI KABISA uliozaa taifa la leo lililosheheni wanafiki waliokubuhu. Mwasisi wa haya ni mzee wetu Julius Kambarage Nyerere. Kama taifa tukawa tunakula (misaada) ya Ubepari na Ujamaa.

Madhara take kila alichokifanya kilikuwa na athari za unafiki, mifano michache inaweza kukusukuma kuelewa hili, Kuhamia Dodoma ni azimio lililoasisiwa mwaka 1973, lakini hadi anafariki Mwalimu hakusema sababu zilizokwamisha tusihamie Dodoma, zaidi ilitolewa hoja nyepesi sana ya bajeti. Ukweli unabaki kuwa siasa za dunia (diplomasia) ndizo zilikwisha mji mkuu na makao ya serikali kuwa Dodoma. Leo viongozi waliofuata baada ya Mwalimu wakija na kile wanachokiita ndoto za mwalimu hawatafiti ni kwanini Mwalimu hakutekeleza mradi huo, na wakianza utekelezaji wanakumbana na siasa ya dunia, Siasa hiyo Magufuli aliionja, na Samia anaionja.

Mfano wa pili ni Katiba Mpya, Mwalimu amenukuliwa akiwa madarakani akionya ubovu wa katiba na akasema wazi siku huko mbeleni mkipata Rais kichaa ataitumia vibaya katiba hii, lakini kamwe hakuchukua jukumu la kuibadili ili iwe nzuri kwamba hata tungepata rais kichaa basi tuwe na uwezo wakumpeleka mirembe sisi wenyewe kabla ya yeye kutupeleka mochwari. Leo umma unahangaika kutaka kuandika Katiba mpya na watawala wa leo wamesema kwao sio kipaumbele...

Wanafalsafa wa Kifarao, Kilatini na Kigiriki kupitia kitabu chao cha kiroho wanasema wazi kuwa, Unafiki ni sumu. Filosofia ya kiroho kupitia kitabu kikuu cha kiroho imetanabaisha kuwa kinyonge hakitaiona pepo, siku ukipata kuiishi dunia yako utaamua juu ya yaliyo usoni pako.

Plato katika andiko lake la The Republic (Jamhuri ya Plato) anawasisitiza kwamba wanyonge ni daraja la wajinga na wapumba waliojitwalia madaraka. Na katika hili anaungana na Napoleon Hill katika andiko lake la "Outwitting The Devil" yeye akisema katikati ya wanyonge, wapo wajinga wachache ambao kula yao inategemea hisani ya watawala, hawa hawajui kuwa ni wajibu wa watawala, bali huamini ni hisani. Wapo tayari kumuua mnyonge apigae ukelele katika milo ya mtawala.

Himizeni mnyonge ajitambue, himizeni mnyonge amjue mpumbavu na mjinga, himizeni mnyonge atambue walioshiba si suluhu kwake. Himizeni mnyonge atambue mjinga na mpumbavu hampagi kibaba cha unga kama fadhila bali ni wajibu wake unaopunjwa.

Mkifanya hayo mnyonge pekee ndio hulibadili Taifa, hubadili majina ya miji na historia, hubadili fikiriko na hubadili sheria. Walioshiba hawaleti mageuzi, walioshiba hawafanyi maendeleo, walioshiba hawafikiri juu ya kufa kwao, ni ukweli usio na shaka kwamba masikini tu ndio hufikiri juu ya kifo.

Aminini nawaambia, kenge wa masika wataibuka wengi kuzuia msifunguliwe ujinga wenu, kwakuwa kwa ujinga wetu mwanakondoo wa thamani ameliwa kwa jasho la mjinga mie na wewe. Acheni magumu yenu ya mtu moja moja, unganeni katika magumu ya umma,

Tunabalehe, Tunapevuka...Tunakomaa... Na unafiki wa taifa, hutaki unaacha!!

Na Yericko Nyerere

______________________

Usikose Kusoma VITABU hivi:

1. Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Bei ni 80,000/= (Kitabu Maalumu kwa wafanyamaamumzi/waliopevuka kiakili)

2. Strategy: The Road to Power, Bei ni 1,700,000/= (Kitabu Maalumu kwa wagombea Ubunge na Urais)

3. Mapambano ya Madaraka, bei ni 30,000/= (Kitabu Maalumu kwa Wagombea uenyeviti Mitaa/vijiji, Udiwani na watu wote)

4. Mtu baada ya Mtu, Bei ni 80,000/= (Kitabu kwaajili ya wote). KIKO MITAMBONI.

Nunua kwa:

LIPA NAMBA TIGO 7489022
LIPA NAMBA VODA 5352627
TIGOPESA kawaida 0715865544

(YERICKO NYERERE)

CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE)

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

Kwamaelezo zaidi piga 0715865544

IMG_20220129_003532_925.jpg
 
2. Strategy: The Road to Power, Bei ni 1,700,000/= (Kitabu Maalumu kwa wagombea Ubunge na Urais)
Asante mleta mada.

Nadhani utakuwa umefafanua vizuri sana strategy ya Unafiki katika kuimarisha nguvu ya kupata madaraka. Maana, inasemwa unafiki na fitina ni nyenzo muhimu katika viunga vya siasa.
 
Tumeruhusu wahalifu waliojipa jukumu la kuwaza na kuamua juu yetu leo wanaamini, nasi tumeamini wao ndio wenye kustahili kuamua kesho yetu, ndio sisi wanafiki lazima tuishi kinafiki njia ya choo isiote nyasi. Asante
 
Mfano wa pili ni kuhusu katiba mpya,Nyerere amenukuliwa........hapo ndio utajua tofauti kubwa ya Madiba na Nyerere,mmoja ni ICON(aliliona tatizo na kuamua kulifanyia kazi)mwingine ni strong stateman (aliliona tatizo na akaamua kuinua zuria na kulipiga teke chini ya zuria)yaliyopo ni history!!!
 
Plato katika andiko lake la The Republic (Jamhuri ya Plato) anawasisitiza kwamba wanyonge ni daraja la wajinga na wapumba waliojitwalia madaraka. Na katika hili anaungana na Napoleon Hill katika andiko lake la "Outwitting The Devil" yeye akisema katikati ya wanyonge, wapo wajinga wachache ambao kula yao inategemea hisani ya watawala, hawa hawajui kuwa ni wajibu wa watawala, bali huamini ni hisani. Wapo tayari kumuua mnyonge apigae ukelele katika milo ya mtawala.
Duu!,inafikirisha Sana.
 
Ilikuwa ni kazi ya Nyerere kuchekecha, ama awe kulia au kushoto, Nyerere na moja ya vinchi vingine hasa vile vinavyotembeza bakuli sana duniani, wakaja na jibu kuwa wao ni nchi isiyofungamana na upande wowote... Yaani Urusi/Uchina hawapo, USA/UK hawapo... Huu ulikuwa ndio UNAFIKI WA AWALI KABISA uliozaa taifa la leo lililosheheni wanafiki waliokubuhu. Mwasisi wa haya ni mzee wetu Julius Kambarage Nyerere. Kama taifa tukawa tunakula (misaada) ya Ubepari na Ujamaa.
Mkuu, sikubaliani na ufafanuzi wako huu kuwa kitendo cha uamuzi aliochukua Mwalimu Nyerere na wenzake kuanzisha umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote kuwa ulikuwa ni UNAFIKI na ndicho kiliasisi unafiki nchini. Narudia sikubaliani na wewe katika hilo. Ninazo sababu.

Sababu zipo nyingi za kuunga juhudi hoja yangu ya kutokukubaliana na wewe.

Leo naanza na hii.
1. Unafiki ukiuchunguza sana uambatana na hila/uongo, nia ovu, kejeli, na mengine kama yale. Kwanza kwa ufafanuzi mwepesi wa maana ya neno Unafiki ni (sijarekea Kamusi ya Kiswahili iliyohakikiwa na BAKITA) ni kitendo cha kumuaminisha kuwa mwenzako kuwa unaamini akifanyacho ni sahihi kwa kumueleza wazi ama kwa kumuonyesha ishara nakadhali wakati kiukweli ndani ya moyo wako na nafsi hauamini kuwa akifanyacho ni sahihi bali unania ya kumuhujumu ama kujinufaisha binafsi kutokana akifanyacho mwenzako. Na kudhibitisha hili unaweza kuanza kumsema vibaya kwa wenzako kama hayupo juu ya udhaifu unaouona kwake.

Kwa maelezo niliyotoa juu ya unafiki, hakuna sifa hata moja ya unafiki ambayo inajionyesha wazi katika kuanzisha muungano wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM).

A) Uanzishwaji wa NAM hakuwa na hila/uongo ndani yake ndiyo maana ulitangazwa hadharani dunia ijue kuwa umoja huu upo na malengo ya NAM yaliwekwa wazi. Pia Tanzania ilikuwa inaweka wazi msimamo wake ndiyo maana Azimo la Arusha lilitangazwa hadharani. Hukukuwa na uongo katika hili.

B) NAM haikuambatana na nia ovu bali NAM ilibeba nia thabiti ya kutojiusisha na uhasimu vile vile ililenga kupunguza vurugu duniani. Niweza kukuhakishia kuwa NAM ni moja ya sababu ya kufanya "Vita baridi" kushidwa kupata joto nakuwa "Vita moto". Kitendo cha maasimu wa Mashariki na Magharibi kushindwa kuwashawishi hawa NAM kilitia wasiwasi pande zote. Ndiyo maana kulikuwa na hujuma kadhaa ama ghiriba kadhaa kufifisha umoja huu. Ni kulegalega kwa NAM ndiyo maana vurugu zimekuwa kubwa duniani.

C) NAM haikukejeli ama kumsema pembeni yeyote. Ndiyo maana waanzilishi wa NAM kila walipopata nafasi walikuwa wanaita waandishi wa habari na kueleza kinaga ubaga kinachoendelea juu ya NAM.

Nikipata muda wa kutosha nitakujana sababu zingine.
===

Nipo tayari kukosolewa kwa ajili ya kuhakikisha ukweli unasemwa hapa JF.
 
Jamii ya kiTanzania ni wanafiki balaa, kibaya zaidi unafiki wetu unarithishwa kizazi Hadi kizazi kuanzi kizazi Cha akina mzee prof. Issa , Kabudi, Lipumba, Dr. Mwakyembe, Mzee Sita (rip), ikafika kwa akina Ndugai...ikafika izazi Cha Kheri James, Mtatiro, Nasari.

Sasa imefika kizazi Cha wanafunzi wanaoacha Mambo ya masomo darasani wanamfanyia birth day Rais....sijajua Kama miaka ya 1990 wanafunzi hawakujua kua Rais wao anatakiwa kufanya birth day.
 
Back
Top Bottom