Kwa kuwa sisi ni Wazembe wa Kusoma Vitabu vya Kufikirisha Akili--Hiki nachoo Kitapita! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kuwa sisi ni Wazembe wa Kusoma Vitabu vya Kufikirisha Akili--Hiki nachoo Kitapita!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IsangulaKG, Feb 7, 2012.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Tanzania imekuwa na waandishi wa Vitabu wengi sana na mara nyingi Vitabu hivi huongelea matukio ya kihistoria kama vile Uhuru, Ujamaa n.k na wengine huandika 'novel' zilizojaa hadithi za kusisimua na kuogofya na mazingira ya 'kufikirika' tu ambayo hayawezi kumjengea babu yangu kule uwezo wa kufikiri.
  Wiki iliyopita katika kutafuta Vitabu vya Watanzania nikakutana na hiki kinachoitwa 'SINDANO INAYOVUJA-A leaking Needle, kitabu cha mtanzania ambacho kimechambua sekta ya Afya na Kupendekeza Mbinu Bora za kuiboresha, Mbinu ambazo kama zingetekelezwa labda tusingekuwa tunaongelea Mgomo wa madaktari sasa

  Bofya Hapa: Amazon.com: SINDANO INAYOVUJA (A Leaking Needle) (Swahili Edition) (9781468156898): Kahabi G Isangula: Books

  Jambo la kusikitisha ni kwamba Maarifa yaliyomo humu yaliyoandikwa na Mtaalamu huyu kwa Lugha ya KISWAHILI kwa kuwalenga Watanzania yatapita hivi hivi abda kwa kuwa sisi ni WAZEMBE wa kusoma VITABU vya KUFIKIRISHA akili zetu( Hii inadhihirika na watu humu JF wasivyopenda kusoma Post za kufikirisha akili zao kwa ushaidi kuwa watu wanao peruzi ukurasa wa 'Great Thinkers' ni wachache mno ukilinganishwa na kwenye 'mahusiano' 'Celebrity' na 'siasa') au kwa sababu ya DHARAU kwa waandishi wa Kitanzania na KUTOTHAMINI CHA NYUMBANI.

  Mimi nimeshanunua nakala yangu, shukrani kwa CRDB Tembocard Visa iliyoniwezesha kununua kitabu hiki toka Amazon.
  Waweza kuungana nami au ukaungana na kundi nililotaja hapo juu.
   
 2. M

  Maengo JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitupie basi humu jamvin tusome mkuu!
   
 3. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ok,ngoja nianze na vile vitabu vingine kwanza
   
 4. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huo ni ukweli ndiyo maana majibu ya wachangiaji wengi ni ya kupondana na siyo ya kutatua matatizo au kero zinazowasishwa humu. Lakini mkuu bado tunaweza kubadilika.
   
 5. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu ebu toa darasa jinsi ya kununua kitabu hicho kupitia amazon.com; mimi ni member wa amazon, na kuna vitabu vingi vizuri online kule, tatizo ni jinsi ya kununua.
   
 6. New2JF

  New2JF Senior Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kitabu hiko
   
 7. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Breaking news hapo ni nini?
  Du haya bwana tutanunua na tusome, ila jifunze jinsi ya kuwasilisha taarifa yako kwa umma
  Nashauri kwa maboresho ya baadae
   
 8. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  usilaumu tu watz. Hicho kitabu kimefanyiwa promo kiasi gani?
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ookay!
   
 10. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Fungua Amazon.com
  Search jina la kitabu mfano 'Sindano inayovuja'
  Bofya 'ADD TO CART'
  Bofya 'Proceed to Check Out'

  Chagua Sheeping Speed: Kila speed ina kiwango tofauti

  Chagua aina ya kadi ya Malipo, mimi natumia 'VISA'

  Ingiza Anwani yako "Shipping Address' unapotaka kitu kitumwe -Jina lako, Mtaa, Nyumba Number/ Ofisi, P.o.Box, Jiji, Mji, Nchi, Code ya Tanzania weka 00255 na simu yako.
  Weka Billing Address; Jina La Benki na Anwani uliyoandika wakati unafungua account mfano:
  Jina Kwenye Card: Joseph Pundamlia Malimoto
  P.o.Box ....DSM
  Tanzania
  Mwisho Bofya 'PLACE ORDER'

  Utapata confirmation E mail katika e mail uliyoandika yenye order number
  Order yako ikitumwa utajulishwa na kupewa Tracking namba kufuatilia kujua ilipo bidhaa uliyonunua

  Good luck
   
 11. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Chema Chajiuza... Kuna vitu Vingi vizuri vya Kitanzania visivyo hitaji Promo...Hii ni Imani Yangu!
   
 12. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kwangu mimi kupata dhahabu kama hii ni Breaking News!
   
 13. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mi namsubiri yule jamaa anayekuja na Amazon Kindles ili niki download hicho kitabu humo. posta zetu haziaminiki
   
 14. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Please upatikanaji wake...
  Novel idea kitakuwepo?
   
Loading...