Umewahi kusafiri masaa mangapi na ndege

Nilisafiri Kwa saa 12 kutoka Johannesburg South Africa hadi Sydney Australia. Hakika ilikuwa amazing kwani tuliondoka saa 4 usiku na kuwasili saa 12 jioni kwa za Australia!
Nchi naikubali sana hiyo!ipo siku nitafika, Inshallah!
 
😂😂😂 Ndege hiyo balaa inakutoa Africa inakupeleka Asia kisha inakupeleka ulaya kisha Australia duh! kwenye mabasi kuna kamsemo chetu cha kufaulishwa na kwenye ndege kapo?😂😂😂
Mbona route iko sawa tu Mkuu? Hakuna mji wa ulaya hapo, ni AFRIKA-ASIA-Australia
 
Dunia ya ajabu sana Italy jua linazama saa nne usiku nilishangaa sana
Dar,Amsterdam,New York,Houston Texas makalio yote yanakufa ganzi,ingine Bongo,Bole Ethiopia,Bangkok,Ghuanzou ,ukifika masaa yanakuchanganya,hujui umeondoka lini,Marekani majimbo mengi yana muda wake,wakati wa majira kama haya saa kumi jioni tayari usiku na wakati wa kiangazi saa mbili usiku bado jioni na jua juu.Ama kweli tembea uone na ujifunze,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom