Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Yuko jamaa yangu toka Shy alikuja Dar kununua gari. Basi nikamtembeza show room kadhaa akachagua gari na kulipia. Sasa tukawa tunasubiri usajili na gari ifanyiwe service tayari kwa safari ya kurudi Shinyanga.
Sasa tuko pale Magomeni mapipa tunasubiri usajiliili jamaa aanze safari ya shy kesho Yake. Jamaa yangu akaamua aende kariakoo akanunue vijizawadi vya kupeleka Shy. Nikamwambia panda daladala yule mjinga akasema, Kariakoo si pale napaona, niharibu Mia nne ? Basi akaamua kutembea. Pale Jangwani mtakumbuka kulikua na viwanja vya mpira mbali na kile Cha YANGA. Basi baada ya kuvuka daraja jamaa akakatiza kwenye vile viwanja na wahuni walikua wanacheza mpira mida ya saa kumi na moja.
Sijui wahuni walimstukiaje jamaa yangu, maana walimpelekea mpira halafu wakaufuata Kama naye jamaa Ni mchezaji wa timu pinzani katika Ile hali walimuangusha Kama mwenzao tu huku wakiendelea kucheka.
Kuja kustuka kila mchezaji anaendelea na hamsini zake na kucheza mpira, jamaa yangu Yuko chini Hana hata Mia.
Nimejikuta nacheka Sana!!
 
Nakumbuka nikiwa Arusha nasoma chuo cha uhasibu miaka ya 2013 kama sijakosea, kuna siku nlishuka kituo cha SDA pale Njiro ili niende ghetto.

Basi nimetembea kama mita kumi hivi njia nzima nipo peke yangu mara nasikia kuna mtu kama anatembeaa ila kwa vishindo kidogo sana, kucheki nyuma kuna njemba hata sijui ilikotokea, kwa hatua za kiusalama akili ilifunguka nikaongeza mwendo ila nikienda kushoto nae anakuja kushoto nikienda kulia nae ni kulia anakuja kwa kuongeza mwendo, mara mbele yangu akatokea mwengine kama anataka anizibe flani hivi.

Nilitoka mbio, sikuruhusu kuwa ndani ya 18 zao maana kwa stori tulizokuwa tukiskia ni kwamba wale vijana ni hatari tupu, nlijidai kama nmesimama flani hivi, akilini nikawa nachora ramani nikimbilie wapi, basi ile nakariba kuwa ndani ya 18 nlitoka spidi nadhani ile siku ndio nlikimbia tangu nizaliwe, wakati nataka nianze kukimbia moja wao alinipiga na kitu kama ubao, nilivyofika geto nilikuwa na kanundu kwa mbali, walinifukuza kidogo ila kwa mbio nilizotoka naona walisanda huku wakinisindikiza na matusi mazito ila nashukuru niliwakwepa.
Uchochoro wa Mango tandika,kuna kauchochoro flani pale Kituo cha Mango kama unaelekea tandika ni shortcut,mwaka 2009 nilikula roba moja matata ya ghafla sikujua ilipotokea,ghafla mbele wakaja jamaa wawili mmoja akainua miguu mmoja ananipiga ngumi za tumbo huku anasema "tulia kum**ko",wakanichukulia kisimu vhangu siemens na buku mbili ya nauli,
 
Uchochoro wa Mango tandika,kuna kauchochoro flani pale Kituo cha Mango kama unaelekea tandika ni shortcut,mwaka 2009 nilikula roba moja matata ya ghafla sikujua ilipotokea,ghafla mbele wakaja jamaa wawili mmoja akainua miguu mmoja ananipiga ngumi za tumbo huku anasema "tulia kum**ko",wakanichukulia kisimu vhangu siemens na buku mbili ya nauli,
wahuni sio watu
 
Ila kukabwa kusikie tu

Nakumbuka nilikabwa njia ya kuingia nyumbani kwangu

Mpaka naamka asubuhi nahisi kama ni ndoto

Jamaa wakaondoka na kipochi changu, bahati pesa niliweka mfuko wa suruali hawakuzichukua
Ila nilikitwa kisu kwenye paja Nna alama mpaka leo

Wahuni siyo watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom