Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Nilitaka kukabwa ila sio mtaani kwangu Ni kule jangwani nilikuwa natoka kwenye mkutano wa injili enzi zileee.....Bado Niko kijana nilikuwa mlokole wa nguvuuu

Basi bwana, Kuna siku nilienda hapo mahubiri tukashangweka weee mpka mida ya Kama saa 4 hivindio tukajongea kituoni kutafuta usafiri, Sasa usafiri wenyewe ulikuwa mgumu balaa na MIJITU nayo ilikuwa nyomiii
Basi mi nilivyoona pale sipaelewi nikaamua nitembee hadi kariakoo nikachukue usafiri
Basi bwana, nikachapa mwendo fasta nikifuata barabara ya lami ya kwenda kariakoo, nikafika sehemu Kuna km kidaraja hv halafu kumepoaa hamna watembea kwa miguu kauoga flani hv kaliniingia ghafla na akili ikaniambia geukaaa.....



Itaendelea kesho:'
Mchikidown

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Kilimanjaro,Moshi vijijini,Kibosho mtaa wa Kombo, Tumekaa kwenye gogo tunakula "kaya" na wanangu wawili mmoja mtoto wa Tandika (M'bongo) na (Nzige) huyu kwao Chunya-Mbeya , majira ya saa 12 jioni ghafla bin vuu ikatokea njemba moja hivi mbavu sana ikachomoa panga, hapo mi ndo nilikuwa naroli kitu, Nzige akataka kukimbia kwa uoga "oya chini ya ulinzi, kaa chini" mimi na huyo dogo wa Dsm ndo tulikuwa hatuna kitete, mi kwanza nikalipua "kitu" punde si punde zikaibuka njemba mbili kwa mtindo ule ule wa mapanga , sasa kati ya wale wawili waliokuja mmoja wao nilikuwa nakutana nae kwa pusha mara ingine namnunulia ganja au namuachia fegi, alivoniona tu akaja akatoa "tano" wale wenzake wawili wakakosa nguvu ya kutukaba, alafu mi hapo nishasizi siogopi chochote, nikamtembezea ganja yule mbavu nikawasha na fegi wakashusha mapanga yao tukaanza kupiga nao na stori nikawapa na ganja wakanyonga....

Wahuni hatukabwi kizembe, labda ukosee code


Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya 2013 naishi kigamboni ferry.
Nilikuwa nafanya shughuli za umeme Goba.
Siku Moja nimerudi ghetto mida ya night huku nimeweka tester (Screwdriver) flat mfuko wa shati.
Sasa wakati nakatizq chochoro za magenge ya urasa, mara ghafla , kibaka akanipiga roba matata. Pasipo kupoteza muda nikawahi ile pisipisi yangu iliyo mfuko wa shati. Nikamdunga nayo mitaa ya Mbavu. Ile anashituka kuniachia, mie nikakurupuka kukimbilia huku sokoni chini, kibaka akakimbilia kule juu.
Pisipisi nayo ilipotelea pale pale.
Tangu siku hiyo, mtaani wananiogopa , kwa kitendo kile. Nilichomfanya yule kibaka.

Mara zote Jaribu kuwa na zana shirikishi. Pindi inapofika usiku.
Huwa natembea na kisu Cha kukunja Kama Nina mizunguko ya mguu usiku mnene.

Jichanganye nikukite

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
NILIKABWA KIFALA SANA MCHANA TENA NYUMBANI NA MBELE YA WASHKAJI NA DOGO LANGU AKISHUHUDIA

Miaka ya nyuma nikiwa dodoma mitaa ya mailimbili hom tulikua na kimaskani nje ya nyumba yetu hapo nikiwa form 3

Siku moja tunapiga stori kama hizi za kwenye huu uzi bac kuna broo mmoja akatokea. Tulikua tunamfahamu tulisoma nae madrasa akaacha akawa anavuta mibangi cjui wapi uko

Baada ya kusikia stori tunazopiga akasogea karibu na mwendo wake wa kiteja teja

Akatwambia madogo mtu yyte akikupiga roba nawapa njia tatu za kutoa. Akanambia mimi nimpige roba nikawa nampiga bla kutumia nguvu lkn akawa anatoa mpaka style zote tatu zikaisha

Sasa akanambia anipige mimi then nitoe kutumia style alizotufundisha. Msenge c akanikamata roba matata sana mbwa yule. Tumia style zote pale waapi zinafeli msenge haniachii

Nikaona hapa sasa nakufa kweli jicho limenitoka na pumzi zinakata washkaji wao wanaona utani tu wanacheka

Basi yule boya akatumia mkono wake mwingine akanipiga sachi akakuta simu na buku mbili pesa akachukua simu akaniachia afu akaniacha nkaanguka huku nakohoa. Akasema "siwezi kufundisha mitoto misenge isiyoelewa bure bure"

Huyoo akasepa zake huku wana wakinicheka vbaya mno. Kwa hasira nikaingia ndani kulala

Popote ulipo Twalibu siku nkirudi Dom lazma nkutafte mbwa ww
Daaaaahh, Twalib kiboko
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Miezi kadhaa imepita ,mi nikishakulaga nyama choma na bia zangu huwa najiona Kama dume la nyani yaani confidence ya kutosha .Sasa baada ya kuchangamka nikapanda toyo kufika mitaa fulani nikamwambia dereva wa toyo nishushe njiani kwani dume la nyani haliwezi kupelekwa mpaka nyumbani bwana .Boda akaniambia mwanakwetu hii mitaa nishai Kuna watoto nuksi .Mi kwa kujiamini nikamwambia mwanakwetu siku nyingi sana sijacheza nao hao ndio haswa nawataka( ngumi zenyew sijawahi hata kuzijaribisha).Kutembea kidogo ghafla naona mkono ushazunguka kwenye shingo ,nikawaambia acheni utani wanangu,ngoma inazidi kutight tu .Ile roba ilikuwa kali mpaka nikayataja majina matatu ya bimkubwa wangu huku nikiwaambia madogo najuta kwanini sikusikiliza ushauri wake wa kuacha pombe.Madogo wakanilostisha mazaga na ngumi za uso za kutosha . Asubuhi naamka lips ya juu ndefuuu ya chini fupi.Sitasahau pia nilivyopigwa mpini wa jembe wa mgongo kwenye bodaboda mpaka nikashuka mwenyewe😀😀 mitaa hiyo hiyo.Acha nikamwagilie moyo ntarudi saa 9 lakin na bajaji.
😂😂😂😂
Watu wanakupiga mpini wa mgongoni mpaka unashuka, wanachukua vyao
 
  • Kicheko
Reactions: EEX

Uzi huu hapa mcheke mpaka muumize mbavu
 
😂😂😂😂
Watu wanakupiga mpini wa mgongoni mpaka unashuka, wanachukua vyao
Walianza na dereva wakamtandika wamkono akayumba akageuza chombo ilipotoka ,mi nikawa nimewapa mgongo nilipewa moja tu nikajikuta nimeruka niko chini.
 
Sijui ni kwanini kila nikipita maeneo hatarishi kwa Ukabaji na hata nikiwakuta Wakabaji wenyewe huwa hawanikabi. Sijui labda wananihisi nami ni Mwandamizi Mwenzao Kiukabaji au vipi.
Ni jilo jina lako mkuu,
nani anataka matatizo
 
Yes 2010
Fainali uefa baina ya asernal na Barcelona kumbukumbu golikipa asernal alipata kadi nyekundu mapema sana alimgusa unyayo samueli eto akienda kufunga goli

Najamaa yangu tunasiku mbili panaitwa bagamoyo unaelekea stend kuu yatukuyu panadispensari na bar moja hivi nalakitano kwenye waleti ,simu Samsung

Kumbe kunajamaa ananiwinda mana natumia pombe balaa
Ukafika muda wamechi bwana ukumbini nilazima upite kaunta ,upande wakulia kunachoo unavoelekea ukumbini
Niliingia choo gent kama kawa kumbe kibaka alikuja nyumayangu akaingia cha ke ili ufike choo cha wanaume nilazima uvuke mlango wa ke
Natoka hivi nataka kukunja niingie baa niliguswa begani kugeuka nikasukumwa kidogo ukutani nikanata pale

Jamaa akatoa kisu vile vyakufyatua akaniambia unaona watu wanapita kuingia kuangalia mechi nikasema ndio
Ukipiga kelele wananiua naomba zilehela zote na simu kila kitu tumeona kwanza mgeni hapa tokajana unakunywa tu bia hapa ukikaa hata kuinuka huinuki

Nikasema nimekwisha ghafla akili ikija yule jamaa niponae alikua ametoka bwana mungu mwema akili ikaja nilegeze mwili na kauli hapo kichwani nipo nahisi damu inamwagika nimeloa mwiliwote
Watu wanapita nawanamwita jamaa jinalake(),anaitikia poa napiga stories na big yetu hapa

Basi ,nikamuangalia alivo nikipande cha MTU mweusi harufu pia yabangi kwambali nasikia toka kwake
Kimo chake urefu kidogo tunalingana

Nawaza nipige wapi huyu usoni jibu ikawahapa
Ghafla wazo likaja nitagonga kichwa changuvu eneo lapua nilazima ainame kidogo niifaidi pua yake
Nikamwambia naomba laini nitoe nikuachie simu napesa zote nakupa

Jibu likawa
Sawa brother nyie ndo mabrother tunawataka hamna bugdha
Nikatoa laini ingia mfuko wanyuma to a waleti

Wakati natoa waleti aliinama ili aifadhi kisu anavoinuka niligonga kichwa puani alilia kwasauti kubwa mamaaaaa nakufa akadondoka chini paaa

RAIA kwenye ukumbi na bar wakatoka wanauliza imekuaje nikawambia wakati mnapita hapa nilikua nimepigwa tero amesema nimpe simu napesa pia Mimi mgeni nakaaje sikumbili nakunywa tu pombe

ndo nikasikia najina lake anaitwa God ,dereva vigali beba mizigo soko LA tukuyu stend pale



Kutoka ilesiku sijawahi kusekana nyumbani sambili kamili usiku labda niwe safarini

Usiombee ukutwe au ubananishwe na kibaka sikiaga tu

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Fainali ya Arsenal vs Barca ilikua 2010?
 
Hawa wajinga nishakutana nao Sana ila kucheza na akili zao ndo dawa,,nikikutana nao Huwa hawanielewi ni mwizi mwenzao au mpita njia tu
 
Nilipigwa ROBA kichochoro cha Mbagala Kiburugwa....

Kanuni ya ROBA si kung'ang'ania uutoe mkono....bali bila ya kupoteza muda nilijikunja na kuweka mikono katika mkono wake ulio shingoni mwangu na "kuning'ania"....

Kama umecheza MARTIAL ARTS hii ndio salama yako....

Kikanuni.....hakuna mkono unaoweza kuhimili UZITO WA KILO 70 za mwanadamu....

Yuke Sakala hakuhimili UZITO WA MNING'INIO WA MWILI WANGU....mkono wake ulichoka na akaniachia....Kama angeujua "mchezo" basi wakati NILIPOJIKUNJA NA KUINAMA angekwenda nami chini(naye angeinama).....angefanya hivyo NISINGEWEZA KUJIOKOA....

Baada ya kuchoka mkono wake ,nilimgeukia kwa haraka na KUMTIA VIDOLE VYA MACHO....huku nikikamata "MBUPU"zake na kuzifuvuta.... Alitoa ukelele mmoja matata....SIKUMSUBIRI NIKAKIMBIA MBIO ZA USAIN BOLT....
utakuja kuuwa ww
 
Miezi kadhaa imepita ,mi nikishakulaga nyama choma na bia zangu huwa najiona Kama dume la nyani yaani confidence ya kutosha .Sasa baada ya kuchangamka nikapanda toyo kufika mitaa fulani nikamwambia dereva wa toyo nishushe njiani kwani dume la nyani haliwezi kupelekwa mpaka nyumbani bwana .Boda akaniambia mwanakwetu hii mitaa nishai Kuna watoto nuksi .Mi kwa kujiamini nikamwambia mwanakwetu siku nyingi sana sijacheza nao hao ndio haswa nawataka( ngumi zenyew sijawahi hata kuzijaribisha).Kutembea kidogo ghafla naona mkono ushazunguka kwenye shingo ,nikawaambia acheni utani wanangu,ngoma inazidi kutight tu .Ile roba ilikuwa kali mpaka nikayataja majina matatu ya bimkubwa wangu huku nikiwaambia madogo najuta kwanini sikusikiliza ushauri wake wa kuacha pombe.Madogo wakanilostisha mazaga na ngumi za uso za kutosha . Asubuhi naamka lips ya juu ndefuuu ya chini fupi.Sitasahau pia nilivyopigwa mpini wa jembe wa mgongo kwenye bodaboda mpaka nikashuka mwenyewe mitaa hiyo hiyo.Acha nikamwagilie moyo ntarudi saa 9 lakin na bajaji.
 
Hawa waseng' huwa ni majasiri sana.Mwaka jana pale Zakhem Mbagala kama unaelekea kibonde Maji walinikabia mjeshi mmoja hivi,wakampora vyote na demu wake wakampoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom