Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Pole sana mkuu. Maisha yana mambo mengi. Tunamshukuru MUNGU, uhai na utu wako ulibaki salama.
Yaani acha tuu ndugu yangu sijui wangeniharibu utu wangu ingekuwaje,.maana wakati ule nilikuwa nikikumbuka lile tukio mwili mzima unasisimka nabaki kuweweseka tuu.. huyu YESU aliyeniokoa pale nitamtumikia milele 🙌
 
Nilipigwa ROBA kichochoro cha Mbagala Kiburugwa....

Kanuni ya ROBA si kung'ang'ania uutoe mkono....bali bila ya kupoteza muda nilijikunja na kuweka mikono katika mkono wake ulio shingoni mwangu na "kuning'inia"....

Kama umecheza MARTIAL ARTS hii ndio salama yako....

Kikanuni.....hakuna mkono unaoweza kuhimili UZITO WA KILO 70 za mwanadamu....

Yuke Sakala hakuhimili UZITO WA MNING'INIO WA MWILI WANGU ,miguu nimeikunja pia ili niongeze uzito chini(gravity)....mkono wake ulichoka na akaniachia....Kama angeujua "mchezo" basi wakati NILIPOJIKUNJA NA KUINAMA angekwenda nami chini(naye angeinama).....angefanya hivyo NISINGEWEZA KUJIOKOA....

Baada ya kuchoka mkono wake ,nilimgeukia kwa haraka na KUMTIA VIDOLE VYA MACHO....huku nikikamata "MBUPU"zake na kuzivuta.... Alitoa ukelele mmoja matata....SIKUMSUBIRI NIKAKIMBIA MBIO ZA USAIN BOLT....
Unapenda kushika pumbu za wanaume wenzako utajageuzwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2004 natoka zangu mjini kuelekea home. Mjini daladala zikawa hakuna, bahati nikapata la Mabibo nikajisemea kimoyomoyo, ngoja nipande hili nitaunganisha Manzese la Kimara. Kufika manzese nikaona nikashukie CCM Kona ya Mabibo. Ile nashuka nikaona nipate bia mbili pale Rambo bar, wengi mtaikumbuka ilikua na Malaya wengii. Basi bwana nikapata siti pale nje na kuahiza safari ya baridi huku nikivizia daladala za Kimara. Nikipata bia za kutosha na simu yangu ya sony mlio polyphonic.
Ile nimelaza bia zangu nikaona pale kituoni Kuna watu Kama watano hivi. Nikaona na Mimi niungane nao tusubiri daladala. Kumbe wote vibaka. Aisee ilenafika kituoni sekunde nyingi nilijikuta nimelimwa mtama Niko chini Sina simu na mituko yoye iko nje.
Kipindi kile surualizilikuana mifuko ya Siri. Hivyo hakiba yangu nyingi hawakuiona. Baada ya kunipora huku mmoja amenikaba Koo wakaondoka. Nilivyo cheki hakiba yangu ipo nilirudi Tena Rambo na kuagiza beer nikiwa pale nje. Na wenyewe baadae walirudi kituoni wakaniona na gida bia. Naona Sasa walijiandaa kikamilifu. Nami nilitoa pesa na kuzihesabu nikiwa pale nje kwenye taa wazione Kisha nikaingia kwenye taxi.
Ukatulingishia bwana!! Kumbe Ni we
 
Taifa walinipora Camera,pesa na simu yangu wakati natoka taifa kuangalia mpira,then ile simu sikureneaw laini Kama wiki hivi,nikatuma message kwa namba nyingine chochote kibaya mikitokea wanitafute kwa namba hii,nikapanda Treni Hadi kigoma mjini,kuna eneo linaitwa Kitonga nikamtafuta mtaalam akafanya yake,huku wale vibaka walivimba vichwa kuja kunitafuta ,so far nilipata kahela kidogo..
Lipia tangazo mkuu
 
Hawa waseng' huwa ni majasiri sana.Mwaka jana pale Zakhem Mbagala kama unaelekea kibonde Maji walinikabia mjeshi mmoja hivi,wakampora vyote na demu wake wakampoka.
Kumpoka ndio nini mkuu,au ulitaka kumaanisha kumbaka
 
Yes 2010
Fainali uefa baina ya asernal na Barcelona kumbukumbu golikipa asernal alipata kadi nyekundu mapema sana alimgusa unyayo samueli eto akienda kufunga goli

Najamaa yangu tunasiku mbili panaitwa bagamoyo unaelekea stend kuu yatukuyu panadispensari na bar moja hivi nalakitano kwenye waleti ,simu Samsung

Kumbe kunajamaa ananiwinda mana natumia pombe balaa
Ukafika muda wamechi bwana ukumbini nilazima upite kaunta ,upande wakulia kunachoo unavoelekea ukumbini
Niliingia choo gent kama kawa kumbe kibaka alikuja nyumayangu akaingia cha ke ili ufike choo cha wanaume nilazima uvuke mlango wa ke
Natoka hivi nataka kukunja niingie baa niliguswa begani kugeuka nikasukumwa kidogo ukutani nikanata pale

Jamaa akatoa kisu vile vyakufyatua akaniambia unaona watu wanapita kuingia kuangalia mechi nikasema ndio
Ukipiga kelele wananiua naomba zilehela zote na simu kila kitu tumeona kwanza mgeni hapa tokajana unakunywa tu bia hapa ukikaa hata kuinuka huinuki

Nikasema nimekwisha ghafla akili ikija yule jamaa niponae alikua ametoka bwana mungu mwema akili ikaja nilegeze mwili na kauli hapo kichwani nipo nahisi damu inamwagika nimeloa mwiliwote
Watu wanapita nawanamwita jamaa jinalake(),anaitikia poa napiga stories na big yetu hapa

Basi ,nikamuangalia alivo nikipande cha MTU mweusi harufu pia yabangi kwambali nasikia toka kwake
Kimo chake urefu kidogo tunalingana

Nawaza nipige wapi huyu usoni jibu ikawahapa
Ghafla wazo likaja nitagonga kichwa changuvu eneo lapua nilazima ainame kidogo niifaidi pua yake
Nikamwambia naomba laini nitoe nikuachie simu napesa zote nakupa

Jibu likawa
Sawa brother nyie ndo mabrother tunawataka hamna bugdha
Nikatoa laini ingia mfuko wanyuma to a waleti

Wakati natoa waleti aliinama ili aifadhi kisu anavoinuka niligonga kichwa puani alilia kwasauti kubwa mamaaaaa nakufa akadondoka chini paaa

RAIA kwenye ukumbi na bar wakatoka wanauliza imekuaje nikawambia wakati mnapita hapa nilikua nimepigwa tero amesema nimpe simu napesa pia Mimi mgeni nakaaje sikumbili nakunywa tu pombe

ndo nikasikia najina lake anaitwa God ,dereva vigali beba mizigo soko LA tukuyu stend pale



Kutoka ilesiku sijawahi kusekana nyumbani sambili kamili usiku labda niwe safarini

Usiombee ukutwe au ubananishwe na kibaka sikiaga tu

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Final ya uefa arsenal na Barcelona ni 2006. Acha uongo
 
Miezi kadhaa imepita ,mi nikishakulaga nyama choma na bia zangu huwa najiona Kama dume la nyani yaani confidence ya kutosha .Sasa baada ya kuchangamka nikapanda toyo kufika mitaa fulani nikamwambia dereva wa toyo nishushe njiani kwani dume la nyani haliwezi kupelekwa mpaka nyumbani bwana .Boda akaniambia mwanakwetu hii mitaa nishai Kuna watoto nuksi .Mi kwa kujiamini nikamwambia mwanakwetu siku nyingi sana sijacheza nao hao ndio haswa nawataka( ngumi zenyew sijawahi hata kuzijaribisha).Kutembea kidogo ghafla naona mkono ushazunguka kwenye shingo ,nikawaambia acheni utani wanangu,ngoma inazidi kutight tu .Ile roba ilikuwa kali mpaka nikayataja majina matatu ya bimkubwa wangu huku nikiwaambia madogo najuta kwanini sikusikiliza ushauri wake wa kuacha pombe.Madogo wakanilostisha mazaga na ngumi za uso za kutosha . Asubuhi naamka lips ya juu ndefuuu ya chini fupi.Sitasahau pia nilivyopigwa mpini wa jembe wa mgongo kwenye bodaboda mpaka nikashuka mwenyewe😀😀 mitaa hiyo hiyo.Acha nikamwagilie moyo ntarudi saa 9 lakin na bajaji.
Unaniua mbavu zangu😂😂😂
 
Yuko jamaa yangu toka Shy alikuja Dar kununua gari. Basi nikamtembeza show room kadhaa akachagua gari na kulipia. Sasa tukawa tunasubiri usajili na gari ifanyiwe service tayari kwa safari ya kurudi Shinyanga.
Sasa tuko pale Magomeni mapipa tunasubiri usajiliili jamaa aanze safari ya shy kesho Yake. Jamaa yangu akaamua aende kariakoo akanunue vijizawadi vya kupeleka Shy. Nikamwambia panda daladala yule mjinga akasema, Kariakoo si pale napaona, niharibu Mia nne ? Basi akaamua kutembea. Pale Jangwani mtakumbuka kulikua na viwanja vya mpira mbali na kile Cha YANGA. Basi baada ya kuvuka daraja jamaa akakatiza kwenye vile viwanja na wahuni walikua wanacheza mpira mida ya saa kumi na moja.
Sijui wahuni walimstukiaje jamaa yangu, maana walimpelekea mpira halafu wakaufuata Kama naye jamaa Ni mchezaji wa timu pinzani katika Ile hali walimuangusha Kama mwenzao tu huku wakiendelea kucheka.
Kuja kustuka kila mchezaji anaendelea na hamsini zake na kucheza mpira, jamaa yangu Yuko chini Hana hata Mia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom