Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Miaka hiyo nipo darasa la nne kijijin. Nikajilimia mahindi ya maji. Yaan unalima mahindi baada ya msimu unayanyweshea kwa mfereji. Sasa maji mara nyingi ni ya kugombania. So mi nikawa naamka saa saba naenda kujifungulia maji namwagilia mahindi. Sasa ile namwagilia nimemaliza nikasema ngoja nikafunge maji. Mida hiyo saa tisa giza kama lote halafu kimyaa mbaya kabisa. Ile natoka kwenye mahindi ebwana kuna mdudu cjui alikuwa fisi au nini Anakimbia alishika break mguuni ile cjui nini kakatiza kwenye mahindi nilihic nywele zimesimama. Sasa Wakat natoka pale nafika tena barabaran mbele yangu nawaona wazee wa kaz wana mafurush kama yote wako mdogo mdogo Nikapiga kelele kamata hiyo Walirusha mafurush mbio kwenye mahindi na Mimi nikala kona home.
 
Kobla alinipitia kwa kifua nkiwa nmelala ghafla wakati anashuka Kuna jamaa yangu alikua macho anakula bange akawa amemuona akamuua ndo kuniamsha kumbe mwamba alimuona wakati anaingiza alikua anafukuza panya mpaka anapanda kitandani ananipita juu ya mwili wangu jamaa anamuona sema aliogopa kupiga kelele maana ningestuka angeningonga. Lilikua bonge la dude
 
Nilikoswa koswa na nyoka nimeenda Kwa jirani kama saa moja hiv wakat naingia nasikia kitu kinafoka sikuwa na toch na umeme ulikuwa hakuna nikasimama bahat nzuri walikuwa na tochi wakamulika aisee bonge la joka wakamuua hatujakaa vizuri mwingine anakuja wakamuua nae nafikir ni wale wanatembeaga wawili wawil
Spitting Cobra
 
Kwenye kuchunga tunakutana na vitu vya kutisha sana.

Tuliendaga kuchunga polini( kuweka kambi )kwa wale wenzangu wa Kanda ya ziwa wanalijua hili, sasa mkifika huko mnachagua eneo mnamwaga dawa kwa kuzungushia na nyie mnaoga dawa,usiku simba na wanyama wakali wanakuja mpaka hapo kwenu halafu wanaunguruma ila hawawezi kuwaona ila ukitoka tu eneo lenye dawa umeisha.
 
Nishawah kuogelea sehem hivi.. kuzamia chini nikaona kitu sikielewi nimekipiga na mkono.. nikaibuka juu kimya.

Nikazamia tena nikagusana nacho miguuni.

Kuibuka juu, nikaona si kweli.. nikazamia huku macho nimeacha wazi nione kuna nini..

Kumbe Mamba yupo humo tunapishana tu..

Aisee sikumbuki nilipaa kwa kutumia mabawa ya aina gani.
 
Mimi kuna siku niko na Pikipiki nimetoka site huko Nyengedi napanda Milima ya Rondo mida ya saa 2 usiku aisee Mara simba huyu hapa nilianguka na Pikipiki nikainyanyua sikugeuka nyuma nilipofika kijijini palepale nilizimia.

Kuna siku tena natoka Makangaka naelekea Kiranjeranje kupanda basi saa 12 Asubuhi niko na miguu aisee ghafla naona simba dume na jike huwezi amini simba Walikuwa hawana njaa walinisindikiza ila Mimi begi nilitupa na Viatu nilikimbia baadae akaja jamaa wa baiskeli aliokota viatu na begi kauliza nani mwenye begi nikamtajia vitu vilivyopo ndani kitambulisho na nguo akanipa begi.

Kuna siku tena niko speed natoka kinyope nakuja Rutamba pale katikati chui huyu hapa kainua miguu aisee nilinyosha wanguwangu akaruka pembeni.

Siku nyingine tuko na gari Tukaona tembo wanne ruangwa wanapita.

Kiboko ashanikosa kwenye mtumbwi mto Ruvuma daraja la Mkenda hakuwa na mtoto alikuwa anaibuka nasikia akiwa na mtoto ndio anakuwa mkali.

Nyoka ndio sana barabarani nishakutana nao zaidi ya Mara tatu ila wadogo wadogo sijawahi kukutana na joka kubwa na kuna siku tumekaa kwenye mti ghafla nyoka kadondoka.

Aisee tunaoishi huku Lindi tumepakana karibu sana na pori kubwa la selous yaani tunapocheza Cheza huku njiani tunakutana na viumbe machachari hapa ninahamu tu kuja kukutana na mamba live ndio sijawahi kumuona.
Aisee kuna mnyama mkali zaidi ya mwanamke?
 
Usikutane na Mamba huyo ni mjusi tu, kutana na Chatu.
 
Tulikuwa tunawinda usiku, tumepaki landrover tunatembea kutafuta wanyama? Mwendo mrefu bila kuoma mnyama yeyote! , master akasema lazima kuna chui au simba anayewafukuza wanyama ili tusiwapate.

Ikabidi mission ibadilike! Tuanze kwanza kumuwimda huyu anaewafukuza wanyama!
Ni stor ndefu ila tulimuua chui mkubwa sijawai ona!
Baada ya hapo yulipata wanyama wakutosha!
 
Unachanganya bro, kuna nyoka mwenye sumu kali na nyoka mwenye uwezo wa kugonga mara nyingi. Koboko anagonga hata mara 50 bro kwani akigonga, meno yake hayatoki baada ya kugonga ila.kifutu ndio nyoka mwenye sumu zaidi duniani.

Koboko wapo kanda ya ziwa na waliletwa (Imported) na wazungu ili kukabiliana na Panya kwenye Plantations za Karanga. Nilikutana nao sana kwenye majiko(Maburn) ya Tumbaku huko katavi.
Nyoka mwenye sumu zaidi duniani yupo Australia. Koboko (black mamba) ana sumu zaidi ya kifutu. Sumu ya kifutu hushambulia cells katika eneo alilong'ata, hii huweza kusababishwa mtu kukatwa eneo lililoathiriwa.
Black mamba wana sumu za aina tatu, inayoshambulia cells, neva za fahamu na moyo. Ndio maana inaelezwa kuwa, black akingata mara moja, ile sumu anayoachia inaweza ua hata watu 4 ikiwa hawatapata matibabu ya haraka.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Nimetoka kuua joka hili nyumbani
 
Attachments

  • 20211227_222814.jpg
    20211227_222814.jpg
    958.7 KB · Views: 6
Simba mara nyingi
Chatu
Majoko
Fisi
Nfuruwe pori mara nyingi
Nyani
Ngedere
Twiga
Tembo
Hao wanyama wote tulikutana.
Siku Wamarekani wakamtwanga risasi Nyati huko porini,wamemkosakosa.
Nyati kaja camp kuwatafuta.
Uliwaka moto ilibidi tuwaondoe pale porini.
Siku ingine tunachoma Nyama kumbe yuko hapo jirani tu anaskilizia harufu.

WaKaja fisi kadhaa kumsumbua aisee walipigwa pale sehemu tunachoma nyama wote tumekimbia.
Siku ingine jamaa walimjeruhi Simba huko porini wakarudi kulala.
Simba wakike si wakaja usiku camp,
Habari kutoka nje haipo
Wanaunguruma pale.
Siku ingine Simba na mbwa mwitu,
Simba anaogopa sana Mbwa mwitu watu hawajui tu.
Simba kazama kwenye tent letu kageuka
si wala hatuoni😂😂😂,
si hapo tunaangalia tutakimbia vipi,kumbe nae anakimbia kichapo cha mbwa mwitu.
Aisee kuna mambo humu duniani yanachekesha sana.
Ile movie
God Must be Crazy naielewa sana.
 
Nyoka mwenye sumu zaidi duniani yupo Australia. Koboko (black mamba) ana sumu zaidi ya kifutu. Sumu ya kifutu hushambulia cells katika eneo alilong'ata, hii huweza kusababishwa mtu kukatwa eneo lililoathiriwa.
Black mamba wana sumu za aina tatu, inayoshambulia cells, neva za fahamu na moyo. Ndio maana inaelezwa kuwa, black akingata mara moja, ile sumu anayoachia inaweza ua hata watu 4 ikiwa hawatapata matibabu ya haraka.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app

Hii ni kweli nimeshaangalia sana documentaries zinazohusu black mamba,pia kile kipindi cha Snake in the City kwa Africa Black Mamba ndio nyoka hatari zaidi akikuuma.
 
Nyoka mwenye sumu zaidi duniani yupo Australia. Koboko (black mamba) ana sumu zaidi ya kifutu. Sumu ya kifutu hushambulia cells katika eneo alilong'ata, hii huweza kusababishwa mtu kukatwa eneo lililoathiriwa.
Black mamba wana sumu za aina tatu, inayoshambulia cells, neva za fahamu na moyo. Ndio maana inaelezwa kuwa, black akingata mara moja, ile sumu anayoachia inaweza ua hata watu 4 ikiwa hawatapata matibabu ya haraka.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Sawa bro, umeeleweka kaka. Nashukuru kwa elimu hii mujarabu.
 
Kwenye kuchunga tunakutana na vitu vya kutisha sana.

Tuliendaga kuchunga polini( kuweka kambi )kwa wale wenzangu wa Kanda ya ziwa wanalijua hili, sasa mkifika huko mnachagua eneo mnamwaga dawa kwa kuzungushia na nyie mnaoga dawa,usiku simba na wanyama wakali wanakuja mpaka hapo kwenu halafu wanaunguluma ila hawawezi kuwaoana ila ukitoka tu eneo lenye dawa umeisha.
Hii ni kweli kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom